Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Nini madhumini na matumizi ya vitu vifuatavyo wavaapo wakina dada na akina mama katika jamii yetu?

1: Kipini cha puani a.k.a (Kishaufu) iwe kushoto au kulia
2: Kikuku iwe mguu wa kushoto au kulia au yote kwa pammoja
3: Na mwisho ni Shanga za kiunoni.

Je, waonaje? Vyapoteza maana halisi kwa wanaovaaa hole hole hole au?

Maoni yako tafadhali changia..


======================================
MAJIBU YALIYOPATIKANA
======================================

Nimeona nilete mada hii ili kuwekana sawa katika ishu ambayo inaongelewa pasipo kuwa na ufahamu wa kina. Katika mapambo yanayotumika sana ulimwenguni na tena na watu wa marika tofauti ni pamoja na vikuku na vishaufu.

=> Kuhusu vikuku miguuni

DSC07523.JPG


Kwa makabila ya kiafrika vikuku huvaliwa kuanzia na watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo na hata vikongwe.

Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi, au hata madini kama dhahabu, fedha na hata shaba. Vyaweza kuvaliwa mguu mmoja au hata miguu yote.

vikuku.jpg


Miongoni mwa mapambo yanayotumika zaidi na wanawake huku umaarufu wake ukiongezeka siku hadi siku ni urembo aina ya vikuku, ambavyo huvaliwa miguuni.

Awali urembo huu ulionekana zaidi katika baadhi ya makabila ya kiafrika ukivaliwa na watu wa rika zote; kuanzia watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo, hata wazee.

Kwa baadhi ya makabila hayo, vikuku vimekuwa vikivaliwa kama mila kwamba kila mwanamke anapozaliwa lazima avae urembo huo kwa kufuata desturi na tamaduni zao, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi huvaa kama urembo wa kawaida.

Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi au hata madini kama dhahabu, fedha na shaba. Kikuu kinaweza kuvaliwa mguu mmoja au miguu yote.

Wanajaamii wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu uvaaji wa vikuku wakihusisha na mambo yasiyofaa na kuonyesha kuwa wengi wanaovaa urembo huo wamepotoka, au kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.

Hata hivyo, wapo baadhi ya watu ambao ni wadau wa urembo wanafafanua kuwa pambo hilo halina maana yoyote livaliwapo kwenye miguu ya mwanamke zaidi ya urembo kama ilivyo kwa hereni na mikufu.

"Watu wanashindwa kuelewa kuwa kikuku ni urembo wa mwanamke kama ulivyo urembo mwingine, mfano bangili, hereni, cheni ya shingoni, pete ,vidani na mapambo mengine ambayo hupenda kujiweka mwilini, unajua mwanamke kujipamba,"anasema Nice Siema

Anafafanua kuwa uvaaji wa urembo huo hauwezi kutafsiri tabia ya mtu kwa kuwa ni pambo kama yalivyo mapambo mengine yanayotumiwa na wanawake.

"Unajua siku zote wanawake wanapenda kupendeza ndiyo maana huwa na furaha kama sehemu kubwa ya miili yao wataiweka urembo tunaona hata vidole vya miguu vinavalishwa pete hiyo yote ni urembo tu hakuna maana yoyote mbaya,"anasema Siema

Kwa mujibu wa wadau wa urembo kikuku kinapaswa kilegee kidogo katika mguu na kwamba hakipendezi kikiwa kimebana, kwani licha ya kusababisha matatizo katika kuruhusu damu kutembea, hakiwezi kuwa na mwonekano mzuri kikiwa katika hali hiyo.

Bila shaka katika mitindo inayoonekana kupokelewa vizuri na wanawake hasa wasichana ni pamoja na uvaaji wa vikuku ambao sasa umetikisa katika kila nyanja.


African-Ankle-Bracelet-1024x665.jpg


Suala la urembo kwa sisi wanawake linjumuisha mambo mengi sana kuanzia mavazi na hereni, vishaufu bangili vidani na makochokocho mengine.

Siku za karibuni kumeibuka mtindo wa wanawake kuvaa vikuku yaani cheni za miguuni. jambo hilo limekuwa likipigiwa kelele na baadhi ya watu wenye mrengo tofauti wakihusisha jambo hilo na tabia zisizofaa.

Lakini cha kushangaza nimewahi kuona baadhi ya wabunge wanawake na viongozi wa kike serikalini tena wenye mamlaka makubwa wakiwa wamevaa vikuku tena wengine walipata hata fursa ya kupiga picha na mkuu wetu na vikuku vyao.

Ninachofahamu mimi, bungeni ni mahali ambapo mavazi yanazingatiwa sana, na ninaamini wengi wetu tumewahi kushuhudia baadhi wabunge wakitolewa nje kwa sababu ya mavazi yao kuonekana kwenda kinyume na matakwa ya bunge, lakini pamoja na jamii huku nje kuwahukumu wanawake wanaovaa vikuku kama watu waliopotoka kimaadili, lakini kwenye eneo hilo la bunge inaonekana jambo hilo limepewa Baraka.

Sasa kwa kuwa suala la urembo kwa wanawake linaenda na wakati, hivi sasa tumerudi Kiafrika Zaidi, na sasa urembo wa shanga umechukua nafasi. licha ya shanga kutumika kama chachandu ya kunogesha mapenzi kwa kuvaliwa kiunoni na wanawake, lakini kwa miaka mingi urembo wa shanga umekuwa ukitumiwa na waafrika wake kwa waume katika kujipamba.

Mfano mzuri ni kwa Wamasai ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakijipamba kwa shanga wake kwa waume na wamekuwa wakipendeza haswa.




Sasa miye hivi karibuni nimeamua kujipamba Kiafrika Zaidi kwa kutupia urembo wa shanga mwilini kiunoni hadi mguuni.

Sasa sijui wenzangu mtanionaje?

CC: miss chagga, miss neddy, miss strong, Karucee, MankaM, DEMBA, Munkari, tinna cute, Tina, Paloma, sister, Ennie, Arabela, Preta, farkhina, Asprin, Mentor, watu8, charminglady, mwekundu, Fixed Point, Ruttashobolwa utafiti, Tyta, Kaunga, Neylu

=> Kuhusu uvaaji wa Vishaufu/kipini puani
attachment.php

Tukirudi kwa vishaufu, urembo huu ambao huvaliwa puani aghalabu hupatikana kwa makabila ya pwani lakini kwa miaka ya karibuni umeenea hata kwa makabila mengine hasa kwa wasichana.

=> Kuhusu uvaaji wa shanga kiunoni

Shanga ni topic tata sana kwangu kwa vile sina uzoefu nayo na kila ninapojaribu kuuliza watumiaji au wavaa huwa hawanipi majibu mazuri na yakuridhisha. Wanaume watakuambia wanapenda tu na wanawake watasema wanaume au wapenzi wao wanapenda wao wazivae.

Rafiki yangu wa Kighana alitoa maelezo ambayo nadhani yalikamilika japo hakugusua umuhimu wake kwenye ngono….aliniambia kuwa huko kwao Shanga ni muhimu kuonyesha kuwa wewe ni mwanamke wa shoka au uliyekamilika.

Ikiwa mwanamke huvai Shanga basi unaonekana hufai na hakuna mwanaume atataka kutoka na wewe/kuchumbia only kwa vile huna shanga kiuoni……hivyo wanawake wote wa Kighana wanavaa shanga no matter how beautiful, educated au westnized they are.
chachandu.jpg


Turudi Nyumbani……nakumbuka niliwahi kumuuliza mama yangu (wao wanavaa shanga) faida ya shanga na yeye akanijibu kuwa ni kama sehemu ya "romance"….nikauliza ni sawa sawa na kubusu au kushikana?

Akajibu "ndio"…..nikauliza inawezekanaje mtu asisimke kutokana na kuziona shanga tu au kuzishika-shika tu? Akanijibu kuwa "mwanaume anapozichezea humpa mwanake mtekenyo furani ambao hufamfanya ajisikie raha na hamu ya kungonoka (nyege) huanza kumpanda".

Mimi kama Dinah nikahisi kuwa mwanaume anaetegemea kuchezea shanga ili mwanamke "anyegeke" atakuwa hana utundu wa kutosha wa kutumia mikono na vidole vyake ktk kuuchezea mwili wa mwanamke hasa ukizingatia kuwa mwanamke "hanyegeki" kwakuchezewa na vidole kiunoni tu bali kona nyingi ktk mwili wake

Uvaaji wa shanga kiunoni ni moja kati ya tamaduni zetu waafrika, nakumbuka katika jamii ya Wanyamwezi (nadhani na Wasukuma pia as far as I remember miaka hiyo niliyoishi kona hizo za Tz ) shanga zilikuwa zikivishwa mtoto wa kike kiunoni na yule wa kiume alivalishwa kijikamba/uzi mweusi ambao huwa na vipande vidogo viwili au vinne vya mti akiwa mdogo.

Ssina hakika kwanini ilikuwa hivyo ila nakumbuka niliwahi kuambia kuwa vijiti vile ni kumlinda mtoto dhidi ya malaika wabaya (kama ilivyo kwa tamaduni nyingine kuwapaka watoto wanja ili watishe) na shanga ni kuonyesha kuwa mtoto ni wa kike.

Mtoto napofikia umri Fulani vikorokoro hivyo huondolewa na binti huvalishwa tena pale anapokua (vunja ungo/balehe), kule kwetu kila rangi ya shanga huwa na maana yake nikiwa na maana kama binti ni Bikira anavaa rangi Fulani, kama uliolewa ukaachika wavaa rangi Fulani, kama umeolewa wavalishwa rangi husika, kama siku hiyo wataka kufanywa (unanyege) basi wamvalia mumeo rangi husika,ikiwa ni mjamzito pia unapaswa kutuma ujumbe kwa kumvalia mumeo rangi fulani (ilikuwa mwiko kungonoka na mtoto tumboni) kama uko hedhini basi utalazimika kuongezea rangi nyekundu juu ya ile uliyonayo.

Itasaidia kama watakuja na rangi inayoashiria kuwa mtu kaukwaa a.k.a ana ngoma a.k.a UKIMWI.....wewe unaonaje?

Ilikuwa ni mwiko kuachia shanga hizo zionekane au zionwe na watu wengine ambao hauko karibu nao kama mzazi, mume, kungwi (shangazi au bibi) n.k. tofauti na sasa ambapo shanga huvaliwa kama mtindo na huning'inizwa hovyo bila kujali maana au ujumbe unaotumwa na rangi za shanga wazivaazo.

Ni wazi kuwa wanawake hawa wanaojivalia shanga hizo na kuzionyesha hovyo huwapa wakati mgumu watu au jamii ambayo inathamini nakutunza utamaduni halisi wa mwanamke kutilia shanga kiunoni na maana ya rangi husika.

Baadhi ya watu huwadhania wanawake wanaovaa shanga ovyo ni wapenda mambo ya ngono……hivi kuna mtu hapendi ngono hapa Duniani?

Bila ngono si dhani kama mimi na wewe tungekuwepo, ngono ni muhimu ktk maisha ya mwanadamu…..au jina lake ndio linawatisha watu? Haya basi tuseme kukutanisha na kuingiza uume ukeni…..bado halijakaa vema….kufanya mapenzi….aaah kufurahia utukufu na uumbaji wake mwenyezi Mungu.

Swala muhimu hapo sio kuwashutumu na kuwahukumu wavaaji hao wa shanga bali ni kuwaeleza kwa uwazi swala zima la shanga……tuache utamaduni wa kubana-bana yale tuyajuayo ili sote tubaki kwenye mstari na ikiwa moja kati yetu atatoka mstarini at least atakuwa anajua nini anafanya au niseme ujumbe gani anaufikisha kwa watamzamaji wa shanga hizo.

Hii yote inatokana na wakuwa (bibi, shangazi, mama) ktk jamii kujisahau na kung'ang'ania mijini na kushindwa kuwatambulisha watoto wao tamaduni za huko watokako (asili yao) hivyo wanakuwa hawajui au wanajifanya "wazungu" na kutofuata tamaduni na badala yake wanafanya watakavyo…..

Mimi nimezaliwa Jijini Dar ila kule kwetu (asili yangu) wanavaa shanga na ninajua mambo mengi kuhusu tamaduni ya kwetu ikiwa ni pamoja na kutambulishwa maana halisi ya shanga na rangi zake……lakini mimi kama mimi sivai shanga sio tu kutokana na mtindo wangu wa mavazi bali pia sivutiwi au sijisikii vema ikiwa nitavaa shanga au hata nikiziona (hasa lundo) zinaning'inia kwa mtu mwingine (kama hiyo picha hapo juu) huwa naona ka' uchafu vile….kama ni kijiuzi kimoja cha shanga au cheni poa ili kuongezea/ziba "kizugaji" uwazi fulani wa vazi lako if u know what I mean.

*Wewe mwanaume kwanini unapenda mpenzi avae shanga kiunoni? Unazitumia vipi zikiwa kiunoni na zinakufanya ujisikie vipi?

*Na wewe mwanamke ikiwa unavaa shanga mpenzi wako huzitumia vipi wakati wa kufanya mapenzi?

Kumbuka hapa sote tunajifunza hivyo maelezo yako ya uwazi yatasaidia sana watu wengine hasa wale wasiojua utamaduni wa shanga na maana yake halisi.


Hitimisho:
Kwanini basi naleta hii ishu tuijadili ni kwamba, hapa JF nimesoma baadhi ya wachangiaji wakihusisha hasa vikuku na mienendo isiyofaa na kuleta dhana kuwa wenye kutumia mapambo hayo basi wana ajenda nyingine.

Binafsi napenda kusema kuwa urembo wowote waweza kutafsiriwa vyovyote - kwa ubaya au uzuri ila mwisho wa siku mtumiaji/mvaaji tu ndiyo mwenye kujua maana.

Wenzangu sijui mnasemaje?

 

Attachments

  • pini.jpg
    pini.jpg
    11.4 KB · Views: 30,622
Nakumbuka mada kama hii imewahi kujadiliwa hapa kitambo kidogo.... Well, mimi bado nasema kuwa kikuku kina maanisha kitu fulani... na anayejipamba kwa kikuku huwa analengo la kufikisha ujumbe kuwa mambo fulani hapo kwake ni ruksa...!
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka mada kama hii imewahi kujadiliwa hapa kitambo kidogo.... Well, mimi bado nasema kuwa kikuku kina maanisha kitu fulani... na anayejipamba kwa kikuku huwa analengo la kufikisha ujumbe kuwa mambo fulani hapo kwake ni ruska...!

Nijuavyo mimi kikuku ni pambo kama kuvaa hereni, bangili au mkufu.Je hicho kitu kingine unachosema wewe ni kipi maana tunaelimishana hapa.

Nimewahi kusikia pia kupaka wanja,kupaka hina, au kuvaa kofia zile za wenzetu watu wa pwani kuna maana yake.Je hizo maana ni of universal application?
 
Hapa naomba mtu yeyote aniambie kila pambo analovaa mtu wa jinsia hasa ya kike na maana yake;ikibidi hata jinsi ya kiume pia.

Binafsi sina la kusema zaidi ya hapo,labda nikisha pata maelezo ya awali inaweza kunisaidia mimi na wengine pia.
 
Dada zetu, wake zetu, wapenzi wetu na mama zetu, mapambo ni kwa kiasi yakizidi ni tatizo. Kwa upande wa vikuku mimi sikujua ni batili mpaka pale Mwana FA katika wimbo wa 'Mabinti' aliposema 'Unaona shanga za miguuni naita vikuku, japo kwa wenye ufahamu ni batili'.

Ukweli unabaki kuwa wadada wamama jipambeni kwa kiasi. Naamini hata wewe ukiona mapambo yanazidi yanageuka kero. Mimi naomba nikupeleke deep zaidi kwenye saikolojia ya mapambo. Kwa vile lengo la mapambo toka enzi na enzi ni kumfanya mwanamke apendeze na mwanamke akishapendeza amini usiamini anakolea zaidi katika mambo fulani.

Wanawake walioongoza kwa kuvaa dhahabu walikuwa wanawake wa Kimisri enzi za Malkia Cleopatra. Mapambo haya yalifikia kilele chumbani wakati wanawake hawa walipojifunua miili yao na kubaki kama walivyozaliwa na walianza kucheza kila aina za mikatiko huku wakisaula kimoja kimoja hatimaye walibakisha shanga za kiunoni, vipini na vikuu na shughuli ilifuatia.

Mpaka leo wanaoongoza kuvaa mapambo hswa dhahabu ni wanawake wa kiarabu lakini mapambo yote ndani ya baibui mpaka muda muafaka wa kujifunua tena kwa mlengwa pekee.

Kutokana na dhahabu kuwa ghali, wadada zetu ili kuonyesha jeuri ya pesa sasa ni kupanga macheni, mapete na mahereni lukuki tena wengine mpaka shanga za dhahabu!. Na asienavyo si haba shurti aazime.

Hapa ndipo kwenye matatizo. Mapambo yakizidi ni dalili ya inferiority complex kwa baadhi ya wanawake kujipamba kupindukia ili kujiridhisha nafsi zao kwa sasa wamependeza. Wajipambao kwa madhahabu mengi kupindukia ni ama wametoka familia duni na sasa wamepata wanataka kuutangazia ulimwengu wote hiyo sasa ndio thamani yao. Wanawake matajiri wa kiukweli wanavaa mapambo simple tuu halafu nenda kwenye mkesha wa mdundiko
Uone mijimama inavyoshindana kwa dhahabu.

Namalizia na pambo la ndani la shanga za kiuno. Baadhi ya wanawake wanaamini shanga hizo huwapagawisha wenzi wao. Basi utawakuta wengine wanafikiri ukizidisha idadi unakuwa bingwa zaidi. Niliwahi kuzihesabu za bingwa mmoja a Tanga, alinivalia 40!. Kwa vile mie sio hoi kwa somo hilo, huyo dada japo ulikuwa bingwa hilo zigo la maashanga kwangu lilikuwa kero kiasi cha kuharibu ladha yote ya somo zima!.

Na sasa hivi visichana vinavyochipukia, vinavaa lundo la shanga mikononi kama bangili ili kukupa nafasi ya kujiuliza kama mkononi ndio hivyo, huko kwenyewe itakuwaje?!.
Mapambo ni kwa kiasi tuu yakizidi inakuwa taabu.

Pasco
 
Nijuavyo mimi kikuku ni pambo kama kuvaa hereni, bangili au mkufu.Je hicho kitu kingine unachosema wewe ni kipi maana tunaelimishana hapa.

Nimewahi kusikia pia kupaka wanja,kupaka hina, au kuvaa kofia zile za wenzetu watu wa pwani kuna maana yake.Je hizo maana ni of universal application?
Kwa wanawake wa mwambao wa pwani kikuku ni zaidi ya pambo ni alama kuwa anakwenda zaidi ya mwanamke wa kawaida katika shughuli nyeti... Kwa wadosi sijui kama wana maana nyingine zaidi ya kujipamba kwani wao huwa na vikuku katika miguu yote miwili.

Kupaka wanja na hina kwa wanaume wa Pwani ni suna, kwa kina dada hina ina sifa zake kutokana na shughuli inayokusudiwa ikiwa ni pamoja na arusi na mambo mengine katika mapenzi.
 
Nijuavyo mimi kikuku ni pambo kama kuvaa hereni, bangili au mkufu.Je hicho kitu kingine unachosema wewe ni kipi maana tunaelimishana hapa.

Nimewahi kusikia pia kupaka wanja,kupaka hina, au kuvaa kofia zile za wenzetu watu wa pwani kuna maana yake.Je hizo maana ni of universal application?

Ni vizuri umerudisha nyuzi hii. Kwa ufahamu wangu mdogo niliopata kwenye maelezo niliyopewa na mtu anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja, hivyo vipambo vina maana tofauti kwa watu tofauti. Sijui kwa watu wa pwani vina maana gani.

Lakini kwa wanawake wanaovaa vikuku mguuni ishara yake ni kuwa hawana tatizo kwenda na kinyume na maumbile au wanafurahia zaidi kwenda hivyo(sijui kama hii ndio maana ya kina dada wetu hapa Tanzania), na kwa wanaume wanaovaa aina fulani ya hereni au kwenye sikio la kulia nao wanatoa ishara fulani kwa wanaume wanaovutiwa na watu wa jinsia yao, nakumbuka niliambiwa kuna ishara nyingi, nyingine ni natural zinatokana na physical appearence hasa kwa wanaume ambao ni feminine, na kwa wanawake ambao ni masculine, hii inatambulisha kwa urahisi kuwa wao ni homos, au uki-initiate kitu fulani basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata response fulani.

Kwa wanaovaa vipambo hivyo, kama wanaiga watu wa magharibi basi naamini kuwa wanatoa ujumbe kama wanaoutoa watu wa magharibi kwa kuvaa vipambo vya namna hiyo, kama sivyo basi watakuwa ni kama vijana wetu ambao wanajisifu kwa kujiita nigger bila kujua maana ya neno lenyewe.

I am sure kuna members humu wanaofanya hivi na wanaojua kwa undani zaidi.
 
Kikukuu najua kuwa kikivaliwa miguu yote na maana mvaaji anacheza Middle,foward na pia ana deffend kwa watu Kibunango nisaidie.
 
Nijuavyo mimi kikuku ni pambo kama kuvaa hereni, bangili au mkufu.Je hicho kitu kingine unachosema wewe ni kipi maana tunaelimishana hapa.
Unakosea woman ukivaa miguu yote wajuvi tunajua unacheza pande zoote kwamba unakaba unashambulia na vinginevyo...ukivaa kushoto pia kuna maana yake na ukivaa kulia kuna maana pia pia

Rita Mlaki alivaa kushoto kulia?
 
Ni kweli hivi vitu vilikuwa mambo ya kawaida tu hapo kitambo.Sasa inakuwaje kama kipindi cha leo wanao tumia vikuku kuwa ni wengi wao wanaujumbe fulani na wanatoa huduma fulani kunako faragha?Basi ndio imekuwa hivyo kuwa vikuku leo vina mana pana tu!

Ndio maana watu wengine wakiona vikuku kama vya kina Rita mishipa inashtuka maana ndio imekuwa hivyo. Kwa hivyo kama wewe unavaa hujui vinamaanisha nini ni kama kutumia new code bila kujua maana yake,mnawatesa mabazazi tu.
 
Ni kweli hivi vitu vilikuwa mambo ya kawaida tu hapo kitambo.Sasa inakuwaje kama kipindi cha leo wanao tumia vikuku kuwa ni wengi wao wanaujumbe fulani na wanatoa huduma fulani kunako faragha?Basi ndio imekuwa hivyo kuwa vikuku leo vina mana pana tu!

Ndio maana watu wengine wakiona vikuku kama vya kina Rita mishipa inashtuka maana ndio imekuwa hivyo. Kwa hivyo kama wewe unavaa hujui vinamaanisha nini ni kama kutumia new code bila kujua maana yake,mnawatesa mabazazi tu.

Mkuu,
Binafsi sidhani kuna haja ya kujitia kiwewe ati mtu atakutafsiri vibaya kama hushiriki vitendo hivyo.The bottom line ni kuwa na kiasi.
Kama mtu ataamua kujitafsiria vingine hiyo itakuwa juu yake.

Najua kwa mfano, kuna wenye kutoa tafsiri hata ya wanja! Ati kuna ujumbe kama " sina mwenyewe" n.k. je tumefikia mahali pa kuwa waoga wa kufanya ile roho inataka kisa ati wajuzi wa kutafsiri watatafsiri?
Na je kwa wale wenye kununuliwa mapambo hayo na waume au wachumba zao ikoje hiyo?
 
Unakosea woman ukivaa miguu yote wajuvi tunajua unacheza pande zoote kwamba unakaba unashambulia na vinginevyo...ukivaa kushoto pia kuna maana yake na ukivaa kulia kuna maana pia pia

Rita Mlaki alivaa kushoto kulia?

Interesting !!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa mantiki ya hoja yako. Wanawake wa kimasai ni mahiri kwa kucheza pande zote.
icon10.gif
 
Kama ambavyo binadamu tunavaa pete zinazoonyesha kwamba msichana yuko engaged au Mwanaume au Mwanamke ameowa au kuolewa.

Nimeona katika baadhi ya nchi hivi vikuku wameviwekea maana maalum inayokubalika.

Nakumbuka nilikuwa na email inayoonyesha maana ya hivi vikuku vinavyovaliwa miguuni (kuna maana tofauti kati ya kuvaa mguu wa kushoto na mguu wa kulia na kuvaa miguu yote) vina maana gani lakini bahati mbaya inaelekea niliifuta.

Kwa Tanzania miaka ya nyuma wengi walikuwa wanavaa kama urembo tu lakini kwa miaka ya karibuni baadhi ya wavaaji hukusudia pia kupeleka message fulani kwa wale waangaliaji wa hivyo vikuku na vibata
 
Interesting !!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa mantiki ya hoja yako. Wanawake wa kimasai ni mahiri kwa kucheza pande zote.
icon10.gif

Hawa bado wanafuata mila zao za kuvaa hizo shanga miguuni. Hakuna ujumbe wowote wanaopeleka zaidi ya kufuata mila zao walizorithi kwa mababu na mabibi zao.
 
Katika mavazi au mapambo yeyote kuna wale wanaovaa kwa kujifurahisha wao au wenzao na wale wanaovaa ili kutuma ujumbe kwa wale wanaoelewana lugha. Ubaya ni kuwahukumu wote kwa matendo ya wachache.

Mwanamke ana uhuru wa kuvaa anavyotaka na kujipamba atakavyo ili mradi conscience yake haimshtaki. Sisi wengine inabidi tuangalie na kushukuru Mungu kuwa ameumba watu wa jinsia tofauti.

Kama tunaona wafanyavyo hakutufurahishi, basi tugeuze macho na kupitia kwengine. Mimi sijali hizo maana zinazosemekana bali nafurahi kuona mguu ulioumbika umerembwa ipasavyo. Hayo mengine nawaachia nyie.

Amandla.....
 
Unakosea woman ukivaa miguu yote wajuvi tunajua unacheza pande zoote kwamba unakaba unashambulia na vinginevyo...ukivaa kushoto pia kuna maana yake na ukivaa kulia kuna maana pia pia

Rita Mlaki alivaa kushoto kulia?

Nadhani kuna wanaovaa urembo huu bila kujua maana hizi... lakini na Rita naye hafahamu maana yake au alikuwa anatuma ujumbe fulani???
 
Interesting !!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa mantiki ya hoja yako. Wanawake wa kimasai ni mahiri kwa kucheza pande zote.
icon10.gif

Mkuu nina hakika wamasai kuvaa wanavyovaa kunatoa ujumbe fulani, na kuvaa kwao sio kuiga ni kitu ambacho wamekuwa nacho toka enzi kabila lao lilipoanza na mapambo hayo yalipopatikana. Sio waigaji wanadumisha utamaduni wao na identity yao, ingawa mimi sio mmasai na sijui maana ya wanavyovaa, na ingawa kuna baadhi ya mambo ambayo wamasai wanafanya yanayoniudhi, lakini ukweli ni kuwa I AM VERY VERY PROUD of these fellow country people of mine.

Kama Mlaki naye anavaa kutokana na utamaduni wa kabila lake i can be proud of her as well. Lakini kama anavaa kwa kuiga watu wa magharibi ambao maana yao ni kucheza kotekote, sitapinga kwa sababu ana uhuru wa kuvaa anachopenda na kutoa ujumbe anaopenda, this is all what democracy is about.
 
Mkuu,
Binafsi sidhani kuna haja ya kujitia kiwewe ati mtu atakutafsiri vibaya kama hushiriki vitendo hivyo.The bottom line ni kuwa na kiasi.
Kama mtu ataamua kujitafsiria vingine hiyo itakuwa juu yake.

Najua kwa mfano, kuna wenye kutoa tafsiri hata ya wanja! Ati kuna ujumbe kama " sina mwenyewe" n.k. je tumefikia mahali pa kuwa waoga wa kufanya ile roho inataka kisa ati wajuzi wa kutafsiri watatafsiri?
Na je kwa wale wenye kununuliwa mapambo hayo na waume au wachumba zao ikoje hiyo?


Yah hainatatizo kama hutojari nani atakuhisi vipi ilimradi wewe unajua unachofanya and you find it urembo.Binafsi mimi naona vinapendeza,sijuhi kwa nini hizi tafsiri zimekuja!

Kuhusu wanja ahaaaaaaaaa sio wanja wote una matatizo kuna ile wanaopaka wale mashankupe unakuwa mithili ya chui kisha unakuwa mrefu sana kupanda juu,sasa ule wenyewe wanaopaka wanakwambia unaitwa "sina bwana" sasa sisi tusemeje!?
 
Interesting !!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa mantiki ya hoja yako. Wanawake wa kimasai ni mahiri kwa kucheza pande zote.
icon10.gif
Wanapenda vikuku inabidi wang'ang'anie hapa ahaaaaaaaaaa kweli lakini wanawanyima raha watu na urembo wao kwa upuuzi wa watu wa tigo!
 
Back
Top Bottom