Mwanaume kurudi nyumbani saa 2 usiku ni ushamba na utoto

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,492
Mwanaume uwe umeoa au upo bachela kurudi home mapema ni ushamba. Mwanaume unatakiwa kurudi walau saa 4 au 5! Issue za kuwahi kurudi home kuangalia tamthiria za Sultan sijui Siri za familia na mkeo ni utumwa.

Mwanaume kaa kiwanja na wana huku mnaangalia mpira au vipindi vigumu. Kaa viwanja huku mnaongea dili za kuingiza mapesa. Unaporudi home mpe mkeo 50 then wajibika kisha lala uitafute kesho.

Mara moja moja toka na kids au kaa nao uwaoneshe upendo wa ubaba kisha wacheki washkaji wako wapi mkachore ramani za Vita. Kama kuna mechi ya saa 7 usikae home hata kama Una DSTV hautaenjoy, njoo hapa kwenye kibanda-umiza cha Mgosi tushangilie then nenda home kawike kama jogoo la huko Didia au Mzilakulima.
 
Alafu ukizeeka au ukiumwa serious au ukipata shida huko kitaa ndio utajua hao unaowaita wana wana msaada gani. We jidanganye tu. Unadhani wataacha kuangalia huo mpira kibandani kwa mgosi waje kukuvisha pampers?
 
Mwisho nijikute natumia hela kwa matumizi yasiyo na ulazima

nikae zaidi ya saa mbili usiku nnje na washkaji mmoja apate majanga tuanze kuchangishana

aah weeee mimi saaa 11 nisharudisha mpira kwa kipa

hata nisipoangalia sultani ntakua zangu chumbani nimelala au naperuzi JF.

Unataka nirudi saa 5 mke namgonga saa ngapi? au ndio unataka npige kimoja nilale

Asubuhi naamka saa ngapi? we eeee bana we weeeee acha hiyo maneno banaaaa
 
Napenda sana kuwa nnyumbani, nicheze na watoto, tusome hadithi, niperuzi jf, niagize Konyagi au Kilimanjaro baridi nikanywe hapa hapa......nikienda club huwa naona kama kuna kitu hakipo sawa....huwa naona kama itarushwa chupa kuja upande wangu, ila pia totozi huwa zinapenda kuniangalia sana. Napenda sana kukaa nyumbani japo wakati mwingi mama Kayayii huwa anazingua. Tangu nikiwa mtoto nyumbani ndipo ilipo furaha yangu!
 
Back
Top Bottom