Mwanaume kuombwa mahari kubwa ukweni kuliko ni dalili kuwa hupendwi

Jamaa angu alitajiwa mil 7 sasa cku anapeleka mzigo asubuh kafumania meseji dem kagegwedwa usiku wake aloo tulikesha bar cku 3 mfulululizo yani hadi muuza nyama akawa anaitwa we nyama leta nyama.
Aisee....
 
mim nilipangiwa 6m, nmetoa 3m nkaahidi wanivumilie ntarud, mi niliwaambia kama utani nikijua mahari huwa haiiashi, juzi juzi nataka tuanze mipango ya ndoa na harusi wameniambia hawaniruhusu coz sijamalizia mahari, sasa hivi nmefikiriaaa,, natafakari, nataka niwaambie wanirudishie pesa yangu wabaki na binti yao
Fanya hivyo hima meku
 
Habari za mchana wakuu, kwanza poleni na majumu mlionayo na mnayoendelea nao hadi sasa,

Kumekuwa na minongono mingi mitaani kuhusiana na swala zima la utoa mahari, kwamba kijana unakwenda ukweni kwa lengo la kutoa mahari (kuposa) kwa nia nzuri lakini cha kushangaza mahari utayoambiwa ukweni ni pasua kichwa, wakati wanajua fika kazi yako, kipato chako.

Familia yako na hata maisha yako kwa ujumla ni ya kawaida lakini mahari atayosema baba mkwe ni kubwa sana kiasi kwamba hata kusema nipunguzie baba yangu inakuwa kitendawili na nakwambia umalize mara moja siyo ado ado, wana JF wenzangu mnisaidie kunaupendo kweli upo au ndo kuniona sifai kumuoa binti yao?

Pia, kumekuwa na tetesi ya ndoa nyingi kufungwa na upande wa pili zikivunjika hali inayowachanganya na kuacha midomo wazi vijana wengi ambao ni mabachela na wakikaa na kutafakari hawapati jibu la kwanini hali hii inatokea? Lakini wakiulizwa baadhi wanandoa watakuambia ingia uone.

Je sababu yaweza kuongozwa na kichwa cha habari kinavyosema.

Tupeane uzoefu tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom