Mwanaume kuombwa mahari kubwa ukweni kuliko ni dalili kuwa hupendwi

Ukiona mahari ni kubwa jaribu kuolewa wewe very simple.

Subiri upate mtoto wako ndio utajuwa wazazi wanagharamia vipi mtoto mpaka amekuwa akapendeza mpaka wewe kimborodinda ukamtamani. Shwaini kabisa.
thamani ya mtoto haifananishwi na pesa, ndoa ni taasisi kongwe kuliko zote dunian, mbona wazee wetu hawakukomoana kiasi hiki, siku hizi wazazi wamejaa tamaa tu, wakiona umemfata binti yao wanahisi una shida sana na mke, wanaona hiyo ni fursa ya kutatulia matatizo yao, huwezi mpangia mtu mahari milion 6 na unamkomalia amalize mahari huku unataka pia muunganishe undugu, hivi roho na moyo wa kuwasaidia mbeleni wakikwama utakuwepo kweli!
 
mim nilipangiwa 6m, nmetoa 3m nkaahidi wanivumilie ntarud, mi niliwaambia kama utani nikijua mahari huwa haiiashi, juzi juzi nataka tuanze mipango ya ndoa na harusi wameniambia hawaniruhusu coz sijamalizia mahari, sasa hivi nmefikiriaaa,, natafakari, nataka niwaambie wanirudishie pesa yangu wabaki na binti yao
Hongera sana mkuu kiukweli hata km ninayo sitoi usawa huu.
 
Hongera sana mkuu kiukweli hata km ninayo sitoi usawa huu.
yani, wangejua kwenda tu kwao ni heshima tosha, nisingewaheshimu ningempa mimba binti yao mapemaaa, na wasingepata jeuri ya kuropoka mahari hiyo, 6m! nilimaindi sana
 
Wakwe zako pasua bongo.
yani, nilipaniki sana siku ile, afu nadhani kitu kilichochangia waropoke vile ni watu walivyojazana siku ile, walialika watu wengi sana , ndugu, majirani nk, yani hata nilivyoingia kutambulishwa niliona njia ya kupita siioni
 
Kuanzia mwanzo najua kuwa nimeuziwa mtoto wao kwahiyo baadaye mahusiano yangu na familia ya wakwe zangu ni kibiashara tu! misaada ya kijinga kama sioni inalipa hakuna kudadadeki na kama noma na iwe noma mambo ni kuuziana tu......
Habari za mchana wakuu, kwanza poleni na majumu mlionayo na mnayoendelea nao hadi sasa,

Kumekuwa na minongono mingi mitaani kuhusiana na swala zima la utoa mahari, kwamba kijana unakwenda ukweni kwa lengo la kutoa mahari (kuposa) kwa nia nzuri lakini cha kushangaza mahari utayoambiwa ukweni ni pasua kichwa, wakati wanajua fika kazi yako, kipato chako.

Familia yako na hata maisha yako kwa ujumla ni ya kawaida lakini mahari atayosema baba mkwe ni kubwa sana kiasi kwamba hata kusema nipunguzie baba yangu inakuwa kitendawili na nakwambia umalize mara moja siyo ado ado, wana JF wenzangu mnisaidie kunaupendo kweli upo au ndo kuniona sifai kumuoa binti yao?

Pia, kumekuwa na tetesi ya ndoa nyingi kufungwa na upande wa pili zikivunjika hali inayowachanganya na kuacha midomo wazi vijana wengi ambao ni mabachela na wakikaa na kutafakari hawapati jibu la kwanini hali hii inatokea? Lakini wakiulizwa baadhi wanandoa watakuambia ingia uone.

Je sababu yaweza kuongozwa na kichwa cha habari kinavyosema.

Tupeane uzoefu tafadhali.
 
Nendeni mkaowe kwa Mengi au kwa Bakhressa mnatupigia kelele za kitoto tu hapa.

Hivi nyinyi mnajuwa hata kulipa school fees kweli?
Mbona mkali sana. Mambo ya kawaida haya. Hivi ukitoa milion 7 then kesho ukamfumania si utaua kabisa. Na inawezekana aliechepuka nae katoa buku 20 tu. Heb tuweni fare basi. Mabinti hawauzwi.

Cha maana ni kuona kama wanapendana, bas unawapa baraka zako wanaenda kuanza maisha na unawapa na support ya kuanza maisha pia.

Hatuna biashara ya utumwa ujue.
 
yan inauma kinoma, kuna vitu waliweka kwenye karatasi lao wakasema ni lazima, no bargaining, posa walinambia 200k, mkaja wa mama M 1, mbuz 10, ng'ombe 4 , fedha taslimu na makorokoro kibao, hivyo vyote tuliomba watuthaminishie katika fedha taslimu ikaja m 6 na chenji
Napita.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom