Mwanaume kumtupia lawama Mwanamke kulianzia mwanzo kwa Adam na Hawa

Safi, ujumbe ni mzuri.
Ila umeshindwa kukaa katikati, in short umeuwasilisha kifeminisms zaidi....sijui kuna nini kinakusibu Karma.

Anyway, mpaka hapo message delivered.
Thank you.
Habari zenu wanajukwaa, natumai mu wazima wa afya.

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza, mwanaume kumtupia lawama mwanamke kulianzia kwa Adam na Hawa kwenye bustani ya Eden.

Kwa wale tunaomuamini Mungu na tunaoamini katika uumbaji, tunajua kwamba Shetani alimshawishi mwanamke kula tunda, kisha mwanamke akamshawishi mwanaume naye ale tunda, kitu ambacho kilikuwa ni kinyume na maagizo ya Mungu.

Baadaye Mungu aliporudi bustanini na kuwakuta wamejificha kwa kuwa waligundua ya kuwa wako uchi, ndipo akamuuliza Adam kwanza kwamba kwanini walikula tunda ambalo aliwakataza kula, pale Adam alipojibu kwamba "ni huyu mwanamke uliyenipa ndiye aliyenishawishi", hiyo kauli ndiyo ikawa chanzo cha wanaume kutupa lawama kwa wanawake

Kwanza kabisa kitendo cha Adam kujibu hivyo kinaonesha ni jinsi gani alijiona hana hatia, yaani alijiona hana kosa kabisa yeye kukubali kushawishiwa na Hawa kula tunda, kitu ambacho Mungu hakuona kama ni sababu ya kujitetea na ndiyo maana aliwapa adhabu wote wawili, kwa sababu laiti kama Adam angekuwa hana kosa lolote basi sidhani kama angepewa adhabu yoyote.

Hii inatuonesha kwamba kumbe Mungu ameruhusu vishawishi, lakini pia ametupa wanadamu uwezo wa kuvishinda hivyo vishawishi ili kwamba kusiwepo mtu yeyote wa kusingizia kwamba eti alishawishiwa.

Na ndiyo maana alimruhusu Shetani kuja duniani kutujaribu ili kutupima imani zetu na watakaofanikiwa kumshinda Shetani ndiyo watakauona ufalme wa mbinguni, lakini wale ambao Shetani atawashinda na kufanikiwa kuwaingiza kwenye dhambi basi Mungu atamhukumu Shetani pamoja na hao wenye dhambi na hakutakuwepo hata mmoja kati yao wa kusingizia kwamba eti Shetani ndiyo alimshawishi.

Sasa tukirudi kwa Adam na Hawa tunaona ya kuwa Mungu alijua kabisa kwamba amemuumba mwanadamu na uwezo wa kukataa vishawishi, hivyo hata Adam pamoja na kwamba alishawishiwa na Hawa kula tunda lakini alikuwa na uwezo wa kukataa, kwa sababu hakuumbwa na akili za kushikiwa hivyo alipoulizwa kwanini alikula tunda hakutakiwa kujiona kwamba hana makosa, bali alitakiwa akubali kwamba hata yeye pale alifanya kosa na ndiyo maana hata yeye pia alipewa adhabu.

Sasa tukirudi kwenye dunia ya leo, siyo mitandaoni, siyo mitaani, siyo wapi, wanaume wengi wanapofanya makosa huwa hawataki kukubali kwamba wamefanya makosa, bali wamekuwa ni watu wa kuwatupia lawama wanawake kwenye kila kitu hasa linapokuja kwenye suala la mapenzi na mahusiano.

Mfano leo hii ukiongelea kuhusu maovu ya wanaume na wanawake kwenye jamii utasikia mwanaume anakuambia eti maovu yote ya wanaume yanasababishwa na maovu yote ya wanawake hivyo wanawake wakibadilika na wanaume watabadilika, imagine hapo mtu anajiona na yeye katoa sababu ya maana.

Sikilizeni niwaambie, jinsia moja kufanya maovu siyo sababu ya jinsia nyingine kufanya maovu na vile vile jinsia moja kuacha maovu siyo sababu ya jinsia nyingine kuacha maovu (ukizingatia pia hakuna andiko linalosema hivyo).

Ikitokea mwanamke amemshawishi mwanaume akamtamani haina maana kwamba huyo mwanaume ndiyo akubali kushawishika na kumbaka au kumtongoza kwa kisingizio cha kwamba eti kaumbwa na tamaa, hivyo atakuja kujitetea kwamba mwanamke ndiye kamshawishi wakati hata yeye mwanaume alikuwa na uwezo wa kukataa, sikatai kwamba mwanamke ana makosa kumshawishi mwanaume, lakini kitendo cha mwanaume naye kukubali kushawishika hapo kosa linakuwa ni la aliyeshawishi na aliyekubali kushawishika wakati kama mwanaume angekataa kushawishika kosa lingebaki kuwa la aliyeshawishi tu.

Haijalishi mwanaume ana hoja kiasi gani za kujitetea kuhusu kushawishiwa na mwanamke lakini ukweli unabaki pale pale, kwamba hapa duniani tunapita tu hivyo tusijisahau sana kwamba kunaye mmoja tu ambaye ndiyo tutaenda kumjibu kwa haya tunayoyatenda hapa duniani, pengine huku duniani mtajitetea sana na kujiona mko sahihi, na wanawake tunaweza tukaamua kukubali tu kwamba mko sahihi tukawaacha muendelee kututupia lawama.

Lakini je itawasaidia nini kama mkiendelea kujitutumua hivyo halafu mwisho wa siku mkajikuta mnaenda kuhukumiwa sawa sawa tu na hao wanawake mnaosema wanawashawishi?? Maana kumbukeni hata Adam pamoja na kujitetea kwa Mungu kwamba Hawa ndiye aliyemshawishi kula tunda bado Mungu alimpa adhabu na ukizingatia katika maandiko hakuna jinsia inayoruhusiwa kufanya maovu na maandiko yanajieleza wazi kabisa namna wanaume na wanawake wanavyotakiwa kujitunza!!

Kujitetea sana na kushinda kwa hoja haimaanishi kwamba ndiyo mko sahihi na wala haibadilishi ukweli, maana hata mahakamani wapo wanaoshinda kesi ilihali wao ndiyo wenye hatia na wapo wanaoshindwa kesi ilihali wao ndiyo wenye haki, jifunzeni kukubali makosa, tatizo linapotokea msikurupuke kutupa lawama kwa wanawake jaribuni kujiangalia na ninyi mnakosea wapi.

Na mwanaume hata kama unajua kwamba mwenye kosa ni mwanamke hiyo haikuhalalishii na wewe kufanya makosa au haikupi ticket ya wewe kufanya makosa eti kwa sababu mwanamke ndiye kaanzisha au kasababisha, maana kumbuka hatahukumiwa mwanamke tu aliyesababisha bali hata wewe mwanaume uliyefuatisha utahukumiwa vile vile.

Mind you hapa siyo kwamba natetea wanawake maana hata sisi wanawake tuna matatizo yetu mengi tu, ila ninachojaribu kusema ni kwamba wanaume muache ile tabia ya kusema kwamba "ni mwanamke ndiye kasababisha ndiyo maana mimi nikafanya hivi" maana hii tabia mara nyingi wanaume ndiyo mnayo.

Wanawake tuna maovu yetu lakini pia wanaume hamtakiwi kutumia maovu ya wanawake kuhalalisha maovu yenu ninyi, kitu ambacho mtakitetea kwa wanadamu tu ambao hawana mamlaka yoyote lakini kwa muumba hakutakuwa na utetezi wa aina hiyo, na hata wanawake pia hatutakiwi kutumia maovu ya wanaume kuhalalisha maovu yetu sisi, kiufupi ni kwamba kila jinsia ina maovu yake na kila jinsia ibadilike kwa nafasi yake na siyo kubaki kutupiana lawama tu kitu ambacho hakisaidii na hakitakuja kusaidia.

Naomba niishie hapa kwa leo, nawatakia weekend njema.
 
Siyo feminism, ila ni kwa sababu mada ya leo inawahusu wanaume kwa asilimia kubwa, ila ipo siku nitaanzisha inayowahusu wanawake kwa asilimia kubwa japo wote tunatakiwa kujifunza, lakini la zaidi nashukuru kwa kunielewa.
 
ni kusudi la mungu kutaka kuonesha udhaifu wa kila kiumbe kwamba udhaifu wa mwanamke ni kurubuniwa na udhaifu wa mwananume ni mwanamke ili tusiju kurudia tena hayo mambo ..halafu kama adam angekataa kula tunda maana nyie ndo mgetupwa huku kwenye shida pekeyenu je sisi wanaume tungeumbiwa kiumbe kingine tofauti na wanawke? je ninyi mgeishi vipi bila wanaume na huku...hiyo haditi ilikuwa inatupa tuu mwanga wa maisha yatakavyo kuwa
 
Okay.

Sawa lakini hakuna hadithi kwenye biblia ambayo inabaki kuwa hadithi tu, lazima kuna funzo ndani yake na hilo nililotoa ni funzo mojawapo.
 
Woii hawa wanaume huwa ni wajinga sana. Eti mwanamke akivaa nguo fupi sijui akipendeza sana ndo vishawishi vya huyo mwanaume kutenda dhambi.
Kama ulivyosema jamii yetu imewaendekeza sana wanaume kutokuwa responsible na makosa yao wenyewe.
Ndo hapo unashangaa hata wale wanawake wanajistiri wanabakwa na kutamaniwa bado.
Na walivyo hawatosheki wana lawiti hadi wanaume wenzao. Sasa hapo sijui wanawake tuna kuwa tumesababishaje. 😂😂😂
 
Woii hawa wanaume huwa ni wajinga sana. Eti mwanamke akivaa nguo fupi sijui akipendeza sana ndo vishawishi vya huyo mwanaume kutenda dhambi.
Kama ulivyosema jamii yetu imewaendekeza sana wanaume kutokuwa responsible na makosa yao wenyewe.
Ndo hapo unashangaa hata wale wanawake wanajistiri wanabakwa na kutamaniwa bado.
Na walivyo hawatosheki wana lawiti hadi wanaume wenzao. Sasa hapo sijui wanawake tuna kuwa tumesababishaje.
Sijui wana matatizo gani kwa kweli, na ukiwaambia hili hawatakuelewa kamwe watasema unataka usawa na ushindani na kwamba wewe ni feminist.
 
Back
Top Bottom