Mwanaume kakuzalisha halafu hataki kutoa barua

maguu

Member
Aug 12, 2011
12
35
mwanaume kakuzalisha mtoto halafu hataki kutoa barua,ukimwambia kajitambulishe kwa wazazi hataki na anataka kuendeleza uhusiano. Je, huyo mwanaume ni mkweli au anataka kunipotezea muda tu. Tuna miaka mitano kwenye uhusiano.
 
kama hataki ku-officiate lazma awe na sababu za msingi,muulize. na kama anasema bado hajawa tayari kwa ndoa,inaweza ikawa vizuri kama mngesitisha mahusiano hadi hapo atakapokuwa tayari kuwa mume ndo mtafutane. ila nadhani kuna kaukweli, 'if u can get milk,why kee a cow?'. i wouldnt,mie natumia maziwa ya unga kabisa,manake hamna haja ya kusugua sufuria wala kukimbilia yasimwagike!
 
mwanaume kakuzalisha mtoto halafu hataki kutoa barua,ukimwambia kajitambulishe kwa wazazi hataki na anataka kuendeleza uhusiano. Je, huyo mwanaume ni mkweli au anataka kunipotezea muda tu. Tuna miaka mitano kwenye uhusiano.
Achana nae haraka sana, amegundua hufai kwa kitendo cha wewe kumkubalia kuzaa naye ilihali si mmeo.
 
Kwani una hamu sana na yeye akuoe? mie naona raha mwanamme akikwambia will you merry me! kuliko ww ukamuonyesha kwenu inamaana hajui kama ww ni mwanamke na kama anakupenda kweli na yuko tayari kuishi na ww kama mke na mume, shosti huyo bwana sie endelea na maisha yako asikupotezee mda wako ....
 
kipi bora,kumuua mtoto au kutokupeleka barua?hapo ndo utajua mwanaume ana ubinadamu au hana.ndio maana ndoa siku hizi hazidumu.wanawake mnajilazimisha kuzaa mkifikili ukizaa utaolewa.hayo ni mawazo potofu.kwanini usingemuambia apeleke barua kabla hajakuzalisha?na hiyo tabia ya kuzaa mnaitumia kama fimbo ya kuforce ndoa ndo maana mabibi harusi wengi wanafunga ndoa wakiua na ujauzito au watoto wachanga.mnatulazimisha kuoa kabla hatujafikia malengo yetu.mia
 
hahahahahhahahahah yaani wewe ulitaka akuzalishe na akuoe ???? duh pole sana maana uliingia chaka..

ukishazaa mama thamani hupungua
 
Yes,
yawezekana hayuko tayari kweli.
Au hakuwa na mpango wa kukuoa lakini wewe
uli m-trick kupata mimba ukitegemea kwakua
una mimba yake basi atakuoa.

Hauoi mtu kwakua ana mtoto wako,unaoa kwakua mmepanga kuoana
na unaona mtaweza kuishi pamoja maishani.

Sijui kama nimejibu kwa ukali,this has happened to me as well.
 
mwanaume kakuzalisha mtoto halafu hataki kutoa barua,ukimwambia kajitambulishe kwa wazazi hataki na anataka kuendeleza uhusiano. Je, huyo mwanaume ni mkweli au anataka kunipotezea muda tu. Tuna miaka mitano kwenye uhusiano.


kwani kukuzalisha yeye amekuwa mkunga au! sasa hata kama mkunga kuna uhusiano gani barua na kuzalishwa hebu acheni zenu banaah
 
Kukaa kwenye mahusiano Miaka mitano is not a gurantee kua atakuoa.... Kwanza upande wangu naona mwanaume anapozidi kujivuta kukuoa ina maana kua hana hakika you are the gal for him hivo anataka awe na hakika kabla hajakuoa kua kweli hamna mwingine wa kumfaa... Kama hamkujadili kuhusu kupata mimba na Kuzaa basi hapo inakua ngumu kumlaumu.... ila inategemea... unataka barua ya kujitambulisha yeye ni baba then hapo i support... kama kwa ajili ya kukuoa.... then dear, mpaka umepost hii kitu hapa kubaliana na matokeo kua hana mpango wa kukuoa and move on....
 
Ulipokosea wewe ulitaka kuzaa naye kwanza ndio mjadili suala la NDOA, hebu fikiria dada yangu ndani ya miaka mitano hakuna cha kujitambulisha kwa wazazi, mpaka ndoa hakuna, alafu ukakubali kuzaa naye, umeshaharibu mamaaa sitegemei kama alishindwa kwenda kufunga ndoa wakati hule hamna mtoto, je??? wakati huu mna mtoto. Mwanaume anapokupenda ukiwa bado bint nina maanisha hajakuzalisha hapo ndipo muda wa kumuomba aende kwa wazazi mkafunge ndoa kwa sababu kama amekupenda kwa dhati atakubaliana na wewe kwani atakuwa hataki kukupoteza, Sasa muda huu wewe mama mtoto, majukumu kibao, labda endelea kumbembeleza uenda atakubali.
 
kubeba mimba au kumzalia mtu si kigezo cha kuchumbiwa au kuolewa mama pole ... cha muhimu kaa chini ujipange kuelea mwana na mshirikishe huyo kidume
 
Hana mtihani wowote yeye tu anajipa tabu, badala ya kufurahia mtoto wake ye anakazana kulazimisha bwana akatoe sijui posa sijui ndoa. Kama Mungu hakukupangia huyo kuwa mumeo tulia subiri wako unajikondesha bure tu bibie

si kila lengo lazima ufanikiwe
 
Back
Top Bottom