The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,451
- 17,154
Mwanaume kabla hujaamua kuoa ama kuzaa, kabla hujaamua kuendeleza kizazi chako lazima ujiulize, je nikifa leo huyu mwanamke ataweza kuwalea wanangu sawasawa ama angalau vile ulivyokua unatarajia?
Tuachane na kifo, ujiulize nazaa na huyu mwanamke ama namuoa, je hali yangu ya kiuchumi ikibadilika ghafla sasa hivi je huyu mwanamke ataweza kusupoti familia/mtoto ama watoto kwa kipindi chote utakachokuwa unapambana kuweka mambo sawa?
Wanaume wenzangu lazima tuwe makini sana hasa kwenye kuendeleza bloodline zetu, tuchague wanawake ambao wataweza kuendeleza kizazi chetu sawa na vile ambavyo tungekuwa hai tungefanya ama angalau na matarajio yetu pale mambo yetu yanapovurugika.
Mwanaume unapoamua kuzaa ama kuoa tumia zaidi akili kuliko hisia, wewe ndie kichwa cha familia, wewe ndio injini ya gari.
Vijana wengi hukimbilia kuoa ama kuzaa na mabinti halafu mambo yakienda tofauti watoto wao wanalelewa kwa shida sana ama wanapata shida kubwa sana.
Mwanaume kabla ya kuamua kuzaa ama kuoa, fikiria maisha ya miaka 5 ama 10 ijayo hasa pale mambo yako yatakapokuwa sio mazuri.