Mwanaume: Ikotekea umejamba kwa sauti Mbele ya wakwe zako, kwa bahati mbaya Utafanyaje?

nelly nashon

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
242
521
Kuna mambo huwa hutuyafikiri lakini hutokea katika maisha yetu,

Katika jamii za kiafrika, Wakwe zetu ni watu wa heshima sana na mara nyingi tunapokutananao huwa tunajitahidi heshima hiyo tusivunje kwa namna yeyote ile.

Lakini kuna matukio mengine ya aibu sana kama utayafanya mbele ya wakwe zako, hasa kwa wanaume mbele ya mama mkwe.. Mfano ni Kujamba kwa sauti mithiri ya bomu...etc

Mfano kwa mira zetu, mama mkwe akiona unakojoa lazima faini yake iwe ng'ombe.

Je, utafanyeje kama kwa bahati mbaya ukiwa katikati ya Mazungumzo ukajamba tena kwa sauti kubwa?

Tililika, Tujifunze.
 
Kwani kujamba ni kufanya nini si kitu cha kawaida tu mie sioni tabu manake najua binadamu yeyote aliyekamilika lazima aifanye hiyo process hata hao wakwe wanajamba kwa sana sembuse wewe
 
Usisite ata kidogo
Mwangalie mkwe wako afu tingisha kichwa umwambie tumbo lilikuwa linakuuma
Kama kuna katoto pembeni ni mda wako oukasingizia, usiombee katoto kawe kaongeaji maana hakatokubali kuonewa
 
Kwanza anipongeze kwa kutoa hewa inayonisumbua tumboni. Ila kiuungwana inabidi usogee pembeni kwani unachafua mazingira, wewe sema samahani, ni aina ya starehe
 
Kwanza tafsiri ya "kujamba bahati mbaya" ni ipi mkuu???

Skurubu zote ziko timamu halafu useme bahati mbaya???

Sema umebanwa sana unaamua kuuachia tu....ila kama ni mzima kijambo kinazuilika na hakuna bahati mbaya ktk hilo
 
Kuna mambo huwa nawazaga sometimes kama binadamu tungekuwa tuna tofautiana baadhi ya "nature" sijui ingekuwaje aisee,.naona Mwenyezi alitambua hilo ndio maana akaweka baadhi ya vitu sawa kwa binadamu woootee kama kifo,na vingine vingi kikiwemo cha mleta mada..

Kwahiyo sioni tatizo kujamba tena umesema kwa "bahati mbaya" sio maksudi so kama ni wakwe wavunge tuu kwasababu ndio maumbile yetu wote hata wao wanapata hiyo raha.
 
Unaesema hakuna bahati mbaya, unacheka kwa raha zako unakuta umeachia, hiyo ndiyo bahati mbaya
 
Back
Top Bottom