Mwanaume huko Senegal avalia kama msichana kumfanyia mpenzi wake mtihani

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,592
20,044


Mwanafunzi wa chuo kikuu huko Senegal yuko amejipata mashakani baada ya kuvalia kama mwanamke ili kumfanyia mpenzi wake mtihani wa somo la Kiingereza.

Picha za Khadim Mboup akiwa amevalia nguo za wanawake zimesambazwakatika mitandao ya kijamii na katika vyombo vya habari nchiniSenegal.

Mwanafunzi huyo wa miaka 22, ambaye alikamatwa mwishoni mwa wiki, alisema alikuwa akifanya hivyo kwa "kwa sababu ya mapenzi " kwa sababu mpenzi wake alikuwa na shida katika somo la Kiingereza, vyombo vya habari vya huko viliripoti.

Alifikishwa mbele ya korti Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa utambulisho na udanganyifu wa mitihani pamoja na mpenzi wake , ambaye alishtakiwa kuhusika katika uhalifu huo.
 
Sijui kati ya hao wawili nani ana akili?aliyekuwa anafanya mtihani au aliyekuwa anafanyiwa mtihani
 
Back
Top Bottom