Mwanaume epuka haya itakuongezea heshima na kujiamini

M

mathabane

JF-Expert Member
2,174
2,000
A salaam aleyqum wakuu.

Hongereni sana na michakariko ya kutwa.

Naomba radhi kwa nitakaowakwaza japo sina nia ovu moyoni bali katika hali ya kushea na kujengana na kushikana mikono ili kila mmoja wetu aishi katika hali ya heshima na thamani ya kibinadamu.

Wanaume majumbani kwenye familia, makazini, mtaani na kwenye jamii yote inayotuzunguka tunapambana na kila aina ya changamoto.

Nyingi ya changamoto hizo ni zile za mahusiano zinazopelekwa kwa nje tuonekane nadhifu na waadilifu ila linapokuja suala la kutumia akili na utashi kwenye mahusiano tunaonekana watu wa hovyo sana mbele ya familia na jamii.

Mwisho wa yote ni kudhalilika na kuishi kwa majuto makubwa na laana juu yake.

Bandiko langu limejikita kijamii zaidi kuliko kidini maana kila mtu ana dini yake humu.

Mwanaume hasa ulie katika ndoa kwa maana ya kuwa na mke/wake jitahidi sana kuepuka haya makundi na hutojuta maishani mwako.

1. Kufanya mapenzi na housegirl wako.
Vibinti vya kazi vya siku hizi ni hatari tupu, haviogopi baba mwenye nyumba. Ndugu yangu jitahidi siku zote usiingie mtego wa majuto.

Bora ujute kumkosa kuliko ujute kumpata . Ukijijengea roho ya kutofanya mapenzi na mabinti wa kazi itakujengea heshima kubwa sana kwa familia yako na jamii unayoishi.

2. Usifanye mapenzi na rafiki wa mkeo ama ndugu wa mkeo.

Epuka sana kufanya mapenzi na hilo kundi kama wewe ni mwanaume wa kweli maana kinyume chake utaonekana ni mtu wa hovyo na mchafu mbele ya jamii.

3. Usifanye mapenzi na mtu wa jirani yako, mtaani kwako ilihali wanamfahamu mkeo. Ukiweza kudhibiti hisia zako na nidhamu utaonekana we mwanaume wa maana sana.

Itakujengea kujiamini na kuaminiwa na watu wanaokuzunguka. Hutojutia maishani mwako.

4. Usifanye mapenzi na mfanyakazi mwenzako ofisini.

Hii itakuepusha na migogoro isiyo ya lazima na kukufanya mtu smart na mwenye kujiamimi sana mbele ya jamii yako. Huwezi jutia maishani mwako.

5. Usifanye mapenzi na boss wako ama subordinate wako mahala pa kazi.

Hutojutia uamuzi wa kutofanya hivyo sanasana itakuongezea kuaminiwa na heshima na utaonekana ni mwanaume wa kweli kwa familia yako na jamii yako.

6. Usifanye mapenzi na mwenye nyumba/mpangaji wako.

Hapa wengi wamedhalilika mbele ya familia zao kwa kurndekeza ujinga huu.

Ukijidhibiti na hii tabia itakujengea heshima sana.

Yapo mengi waweza kuweka na ya kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
THE BREED

THE BREED

JF-Expert Member
1,134
2,000
Well said!japo mitego kibao kutoka kwa housegirls wanataka kupanda cheo!!!!
 
DiasporaUSA

DiasporaUSA

JF-Expert Member
22,835
2,000
Neno "Usifanye Mapenzi " ni ngumu sana kulikwepa mkuu kwa watu wa sasa..ila hata wa zamani pia! Haijalishi unafanya na nani.

Ipo aplicable kwa Dada na mama tu!
Hata wewe
 
caryeda

caryeda

Senior Member
103
500
Nafikiri kichwa cha thread ungeandika USIFANYE MAPENZI
 
barafuyamoto

barafuyamoto

JF-Expert Member
28,156
2,000
mathabane,
Yaani haya ya ngono tu ndio yanaleta heshima sio heshima?
acha kufikiria ngono mkuu.
 
Z

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
5,413
2,000
Umenena vyema. Kimsingi, usifanye mapenzi na mwanamke asiye mke wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Haswaa.
Mtu pekee wa kufanya naye mapenzi ni mke wako tu, mwanamke mwingine yoyote mkwepe kama moto. Ukifanya hayo utapata heshima kwa Muumba wako na watu wote. Na yote kwa yote utaishi kwa amani na furaha fulani hivi.
 

Forum statistics


Threads
1,424,795

Messages
35,072,712

Members
538,098
Top Bottom