Mwanaume ananipasua kichwa

Jina lako lilipaswa liwe CHIZI LA MILEMBE nilijua nimewahi kupendwa mpaka pale nilipokutana na mwehu kama wewe ,la kushukuru MUNGU wewe sio ndugu yangu, NB: Kuna chumba tabata baracuda self njoo nikupangishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyie mnaemponda huyu dada akiachikia mnauwezo wa kumfikisha??

mwenyewe anasoma comments zenu huku anajisema "tatizo hawa hawajui tu" 😂😂😂😂😂
 
Hivi hapa wazazi ndiyo wanakosea au vijana....wewe hauna wazazi! Au kaka waliokuzidi umri! Hawaoni uyafanyao kama yanakuletea matatizo?


Ishi kwenu kama mchumba atakuja kukufuata kwenu.
Hawa wa hivi huwa wanakuwa wajuaji kupitiliza, watu mwisho wa siku wanaamua kumkalia kimya. Huyu dada ni Msukuma aliyeenda shule kidogo,
 
Habari JF..mm ni binti nina boyfriend wa muda km miaka 7 now.

Bahati mbaya sn nilikoseaga nikaenda kuishi nae tena nyumbani kwao kabisa mamamkwe na wawifi wote wapo. Hajanitolea barua wala mahari. Wakati naishi nae familia yake ikawa hainipendi navumilia walikua wananiona km nimemroga mtoto wao kwa jinsi yuko karibu na mm. Tukaja kugombana na huyo mwanaume ugomvi mkubwa tu nikaondoka nikarudi kwetu huku nyuma familia yake ikafurahi kweli bora tumeachana.

Tumekaa miezi 6 mwanaume akanitafuta tukarudiana sasa changamoto ni kua anataka siku ambazo niko off kazini niwe naenda kushinda kwao. Jman nimekataa mwanaume haelewi nimemwambia siwezi kwenda kwao tena apange chumba tuwe free. Na kwao nitaenda atakapokua amenioa au kunitolea mahari..haelewi anasema km siendi kwao basi tuachane...

Je ni sahihi kweli baada ya yote hayo kutokea mm kutoelewana na familia yake niwe naenda kwao jamani? Nilikua nafikiria km yeye hataki kupanga chumba basi mm nipange kwa pesa yangu ili tuwe free je na hilo ni sawa.

Naombeni ushauri jamani mwenzenu nimekwama
Hapana kama unapanga akija kuhamia kwako utajuta, kama utaenda kukaa kwao utajuta. Akapange ndio akuite
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom