Mwanaume anahitaji mwanamke malaika wakiwa sebuleni na mwanamke mtundu wakiwa chumban

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,601
2,000
Wanaume wanahitaji mwanamke mtundu, tendo la ndoa ambalo linaleta msisimko, linalofurahisha na kutia hamasa mpya kila siku.
Jaribu vitu vipya, mikao, miguso, busu, na michezo ya uwaja wa 6x6 au chochote umejifunza, acha woga kwamba atakuuliza nani kakufundisha, dunia ya leo tunaishi dunia ambayo wanaaiita information society, hivyo watu tunapashana habari na kufundishana kupitia magazeti, radio, TV, movie, internet nk.
Usiache kufanya kitu kipya huko chumbani eti kuogopa atakuuliza umejifunza wapi.
Kazi kubwa kwako ni kuhakikisha uwanja wa 6x6 unakuwa moto siku zote na pia kumpa vitu vya uhakika ili asitembeze macho nje kutokana na kuwa bored na mapishi ya aina hiyohiyo miaka nenda miaka rudi.
Ni kweli kama umri umekwenda sana hamwezi kufanya kama ile miaka ya nyuma lakini isiwe sababu ya kutokuwa na mambo yenye kuridhisha na mwanamke kuwa moto uwanjani.
Miili yetu ni hekalu la Mungu la ajabu na la aina yake hapa duniani.
Mwili ni laini, una harufu nzuri, ukiguswa unapata raha ya ajabu, hivyo kama mwanamke unahitaji kujiweka safi na hot muda wote bila kujali umri.
Kitu cha msingi ni kwamba mume wako anakuhitaji wewe, anahitaji ladha mpya na utamu kila siku kutoka kwako iwe ni kukugusa kwa mikono yake, au kukuangalia kwa macho yake au kukunusua mwili wako kwa pua yake au kukusikia unaongea maneno matamu kwa masikio yake na kukuonja mwili wako kwa ulimi wake.
Ni kweli anakuhitaji wewe na si mwingine na kwa kuwa anakuhitaji wewe basi
Mpe raha
Keep it hot,
steam it up
and you both will come back wanting more time and time again.

Mwisho
Kuna mambo ya msingi ambayo mwanaume anahitaji kwako na kuna kitu anataka kwako, kuna mambo mengi sana mwanaume anahitaji kwako kitu cha msingi timiza hizi ndoto kwa kuzifanyia kazi.
Kama utakuwa ni mtu unayekuwa mbunifu na mwenye kufanya mambo tofauti bila mazoea basi uhusiano wako na umpendaye utakuwa imara na mzuri kila iitwapo leo.

Mungu akubariki sana.
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,601
2,000
Waache kupiga piga kelele ooh sijui wanaume nini oooh mara lile
Imebidi niwape ka ukweli kidogo
Ngoja waje wasome:A S-alert1:
 
Pearl

JF-Expert Member
Nov 25, 2009
3,039
1,195
uliyosema ni kweli tupu lkn pia Mwanammke anahitaji mwanamme malaika wakiwa sebuleni na mwanamme mtundu wakiwa chumban
 
Digna37

JF-Expert Member
May 17, 2010
725
250
Mnataka mfanyiwe hayo yoooote na tunajitahidi sana kuyafanya. Ninyi mnafanya nini zaidi ya kuleta mauzi tupu? Nadhani ni 50/50 sio zoezi la upande mmoja. Haijakamilika hii..... :A S kiss::music::peace:
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,601
2,000
Mnataka mfanyiwe hayo yoooote na tunajitahidi sana kuyafanya. Ninyi mnafanya nini zaidi ya kuleta mauzi tupu? Nadhani ni 50/50 sio zoezi la upande mmoja. Haijakamilika hii..... :A S kiss::music::peace:

Sema utakacho ufanyiwe sio kubwabwaja tuuuu
Siye tumeanika wazi hapoo:A S-alert1: au nikusaidie bibie :kev:
 
Digna37

JF-Expert Member
May 17, 2010
725
250
Tizama hata jinsi unavyoongea jamani! Loh! Kama nabwabwaja weye umebwatuka pale juu. Haijakaa vizuri, ikikaa vizuri mazungumzo yoootee yanateleza tu. brb...
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,601
2,000
Tizama hata jinsi unavyoongea jamani! Loh! Kama nabwabwaja weye umebwatuka pale juu. Haijakaa vizuri, ikikaa vizuri mazungumzo yoootee yanateleza tu. brb...

sema umeshindwa usaidiwe ndo maana yangu

Wanawake pia wanahitaji tendo la ndoa linalowaridhisha na kuwafikisha pale wanahitaji. Anahitaji mwanaume anaye mtimizia ndoto zake za mahaba, anafurahia na kujisikia raha jinsi Mume anavyompa mgusu wa kimwili wenye msisimko wa raha,
Anajisikia vizuri kupata busu tamu,
Anajisikia vizuri kukumbatiwa
Anapenda kusikia maneno matamu ya kimapenzi kwenye masikio yake
pia wanapenda kusikia na kuona mambo mapya uwanjani siyo mazoezi ya kila mwaka mambo yaleyale, anajisikia vizuri kuwa na mwanaume mbunifu na dereva mzuri.
Hahitaji mwanaume anayempeleka uwanjani na baada ya dakika mbili amemaliza.
Hapo unaweza kumpotezea hamu ya tendo la ndoa ambayo ni zawadi kuu Mungu ametupa viumbe wake.
Mwanamke anahitaji mwanaume anayejua kumuandaa kabla ya tendo lenyewe na pia anahitaji mume anayejua kumaliza kwa mtindo ambao anaridhika.
Mwanaume unahitaji kuhakikisha tendo la ndoa linakidhi kiu yake, anaridhika na linakuwa na maana kwako na kwake na kila siku hamu inazidi kukua zaidi.

UTAIPENDAAAAA.................................
 
Atoti

Senior Member
Nov 30, 2010
118
170

Wera wera weraaaaa
 
St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,401
2,000
Kimbweka tukishafanya hayo yote tunapata nini?

Hapo ndio shida inapoanzia,na kila siku mmejiwekea akilini kuwa ni mwanamke tu ndiye anayeandaliwa,na ukiendelea kuuliza hivi usijemlaumu baba watoto wako kwa kuchelewa kurudi nyumbani.
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
24,912
2,000
Hapo ndio shida inapoanzia,na kila siku mmejiwekea akilini kuwa ni mwanamke tu ndiye anayeandaliwa,na ukiendelea kuuliza hivi usijemlaumu baba watoto wako kwa kuchelewa kurudi nyumbani.
We PM ndo wale wale!Kama nimetimiza wajibu wangu huo kwanini kuwe na tatizo kama nae atatimiza wake?Ubaya ni kwamba unajaribu kusema wanawake tu ndo wakuzingatia yaliyosemwa!Wakati kila kitu kinahitaji ushirikiano!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom