Mwanaume amjeruhi mjamzito akitaka kuona mtoto tumboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume amjeruhi mjamzito akitaka kuona mtoto tumboni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 25, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  WAPO wanawake wengi waliofanyiwa ukatili wa aina mbalimbali, lakini huu ambao amefanyiwa mwanamke, Nyamhanga Matiko (45) mkazi wa Kitongoji cha Senta Kijiji cha Masangura wilayani Serengeti, unatisha.


  Huu unatokana na mwanaume katili ambaye kwa dhamira ya kutaka kuona jinsi mtoto mchanga anavyokaa tumboni, akamteka mjamzito na kwenda kumfanyia unyama huo.


  Haya yanafanyika wakati ambapo sheria kali za kukomesha unyanyasaji wa kijinsia hapa nchini zipo na pengine mwanaume huyo anaamini mkono wa dola hauwezi kumtia kwenye msemeno huo.


  Maisha ya sasa na yajayo kwa mwanamke huyu ni kitendawili ambacho yeye binafsi, anasema ni vigumu kukitegua, lakini liwe liwalo kwa sasa anafikiria apone majeraha anayouguza.
  Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Serengeti, mama huyo kama anavyoonekana pichani, hana vidole katika mikono yake yote miwili.


  Akiwa hapa hospitalini anakaa kwa kusaidiwa anasema:
  “Aliponyanyua panga kwa ajili ya kunikata kichwani nikaweka mkono wa kushoto, akakata, kiganja chote kikaanguka chini. Akanyanyua tena panga, nikaweka mkono wa kulia, akakata vidole vinne vikaanguka chini.


  Lilivyotokea
  Anasema ilikuwa Mei 21, majira ya jioni akiwa na wanawake wenzake wakirejea
  nyumbani baada ya mkutano wa Kijiji kushindikana kufanyika kutokana
  na mvua nyingi kunyesha, walimwona mtuhumiwa akiwa amemsimamisha njiani mama mwenye ulemavu.


  Hawakujua kinachoendelea, lakini kumbe alikuwa amemteka na katika vitisho, alikuwa akimsihi asimuue.
  “Ghafla alimwacha mama huyo mlemavu ambaye na kuanza kutufukuza huku mkononi akiwa na panga, upinde na mishale,” alisema Nyamhanga.
  Anasema walikimbilia katika nyumba ya Mwita Ng’ombe na kujificha humo na hakuwafuata tena akaonekana akirejea alikotoka.
  “Sisi tulifikiri keshaenda zake tukawa tunatoka kurejea kwetu kumbe alikuwa amejificha, ghala akaanza kutukimbiza tena,” alilalamika Nyamhanga.


  Anaongeza: “Kutokana na ujauzito wangu niliishiwa nguvu na kuanguka chini na hapo akanishika kirahisi na kuanza kunitenda unyama huu.”


  Anasema akiwa chini, mtuhumiwa alimpiga kwa ubapa wa panga na kumtishia kuwa atamuua.


  Ingawa alipiga sana kelele, anasema hakuna mtu aliyefika kumuokoa kwa kuhofia kuuawa.


  Mmoja wa watu ambao anasema hakumfahamu alimrushia mtuhumiwa mawe na moja likampata.


  Kuona vile, anasema mtuhumiwa alianza kumvuta hadi nyumbani kwake na kumfungia ndani huku akilalamika kuwa lazima amwage damu ya mtu siku hiyo.


  Alidai kuwa akiwa ndani hajatekeleza unyama wake huo, alijitokeza kijana mmoja aliyemtaja kwa jina la Chacha Nyairangu akiwa na lengo la kumuokoa, lakini alimgeukia akitaka kumjeruhi na akimbia.
  Wakiwa katika majibizano mwanamke huyo alipata nafasi ya kutoroka, lakini kwa kuwa alikuwa ameishiwa nguvu alimkamata tena.


  Safari hiyo, anasema hakumrejesha ndani na badala yake alimvuta na kumpeleka vichakani ambako na kuanza kumshambulia kwa kumkata kata.


  “Aliponyanyua panga kwa ajili ya kunikata kichwani nikaweka mkono wa kushoto,
  akakata, kiganja chote kikaanguka chini. Akanyanyua tena nikaweka mkono wa kulia, akakata vidole vinne vikaanguka chini.


  “Akanikata kichwani na mabega,” anaelezea huku akikunja uso kwa dalili za kutaka kulia, lakini hata hivyo akawa anajizuia.


  Nilianguka chini na kuishiwa nguvu akawa anasema anataka anikate tumbo ili amuone mtoto, lakini kwa kuwa giza lilianza kuingia aliondoka.
  Anasema alitamani asimame aondoke, lakini akawa anashindwa na punde akapita mtu mmoja kwa kutumia simu yake ya tochi akammulika.


  Alimsihi amsaidie ili kumfikisha eneo ambalo anaweza kupata msaada, lakini mtu huyo alimuacha na kuondoka zake.


  Licha ya damu kumtiririka kwenye viganja vya mikono, kichwani na begani, pia tumbo lilikuwa na maumivu makali, hivyo akahisi mimba yake nayo imetoka.


  Anasema alipoteza fahamu na alizinduka siku iliyofuata na kujikuta yuko hospitalini akipatiwa matibabu.
  Anaelezea tukio hilo akisema, “sasa nimeachwa na ulemavu sijui hatma ya maisha yangu.”


  Anasema ana watoto watano ambao wanamtegemea, baadhi wakisoma shule za
  msingi.


  Hata akipona anasema hawezi tena kupika, kulima anaona mwelekeo wa maisha yake sasa utakuwa ni wa ombaomba.


  Mtuhumiwa


  Taarifa za polisi zinamtaja mtuhumiwa (jina tunalo) ambaye baada ya kufanya unyama huo alitoroka.


  Taarifa zinadai pia kuwa kabla ya tukio, wanakijiji walimsikia akisema kuwa lazima amchinje mwanamke ili aone mtoto anavyokaa tumboni.


  Watoto
  Nyamhanga anasema yeye ni mjane na kwa sasa ana watoto watano; miongoni ni Mariamu Kitentani(24), Sabato Mussa(19).


  Mwanaye Mariamu anasema kuwa siku ya tukio walilala kwa wasiwasi kwa sababu haikuwa kawaida ya mama yao kutorudi nyumbani au kukawia nje usiku.


  Ilipofika asubuhi bila kumuona, anasema waliwaarifu majirani ambao walianza kumsaka huko na kule hadi walipompata vichakani akiwa amepoteza fahamu kutokana na kuvuja damu nyingi.


  “Walijitokeza watu wengi kumtafuta na ilipofika saa mbili, tulifanikiwa kumpata kichakani akiwa hajitambui kutokana na majeraha na kuvuja damu kwa
  wingi,” anasema Mariamu.
  Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Mwita Marwa Wambura analielezea tukio hilo la kikatili limeibia maswali mengi yasiyo na majibu.
  Anasema pamoja na masikitiko kwa namna alivyofanyiwa unyama, mtuhumiwa anadaiwa kuondoka na kiganja pamoja na vidole vya mwanamke huyo.
  Hisia hizo zinatokana na watu kutafuta viganja na vidole eneo la tukio bila mafanikio.
  “Wananchi wamejitahidi kusaka viungo hivyo bila mafanikio na inadaiwa kakimbilia
  wilayani Tarime,” anasema.


  Anasema kabla ya kutenda unyama siku hiyo palizuka ugomvi kwenye kilabu cha pombe za kienyeji na mtuhumiwa huyo inadaiwa alipigwa na akatoka kwa kasi kwenda nyumbani kwake.


  Akiwa njiani inadaiwa alimpora kijana mmoja baiskeli akakimbia hadi kwake na kuchukua silaha hizo, huku akifungia baiskeli ndani ya nyumba yake,” anasema Wambura.


  Mtendaji huyo alisema tabia ambazo mtuhumiwa amekuwa akizionyesha kijijini hapo zinaashiria kwamba anatumia dawa za kulevya.


  Hasira za wanakijiji


  Wambura alisema baada ya kusikia tukio hilo, wanakijiji walianza kumsaka huko na kule lakini hawakumpata.


  Hali hiyo iliwapa hasira wakaenda nyumbani kwa mtuhumiwa wasimpate mtu ila kukawa na taarifa ana ng’ombe watatu ambao amewaweka kwa mmoja wa wakazi wa kijiji hicho.


  Wakiwa wamepania kuwakamata ng’ombe hao ili wauzwe na fedha zitumike kumuuguza mama huyo.


  Lakini kwa bahati mbaya baada ya uchunguzi wakabaini kuwa taarifa hyizo siyo za kweli.


  Ofisa Mtendaji anasema hali hiyo iliwafanya wanakijiji waitishe mkutano wa kijiji wa kuchangishana ili fedha hizo zitumike kumsaidia mama huyo ambaye ni mjane.


  Hata hivyo, anasema ulivunjika kutokana na mahudhurio ya watu wachache.
  Mmtendaji huyo wa Serikali anasema watoto wawili wa mama huyo wanasoma
  shule za msingi na wanasaidiwa ndugu kwa kuwa hawana baba.


  Daktari


  Daktari wa zamu, Mnanka Funga anasema hali ya mama huyo inaendelea vizuri pamoja na ujauzito wake.


  Mwenyekiti wa Shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu Wilaya ya Serengeti, Samweli Mewama
  Anasema jamii inatakiwa kubadilisha mitizamo ili kuachana na vitendo vya kikatili.
  Mratibu wa Mpango wa Kuzuia Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia Kupitia Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wilaya ya Serengeti, Sophia Mchonvu anasema vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaonekana kushamiri kwenye wilaya hii.


  Matukio mengine
  Taarifa za polisi zinasema kuwa mbali na tukio hilo, mengine kadhaa yameripotiwa katika siku za karibuni.


  Mojawapo, anasema ni la Neema Charles Ngoko (17) ambaye ana ujauzito wa miezi minane kupigwa na mumewe.


  Kama hiyo haitoshi, polisi wanasema kuwa mwanaume huyo alimfungia ndani siku 14, kwa kosa la kumpikia uji kwa viazi.


  Jingine, polisi wanasema ni la
  Bhoke Nyaheke mkazi wa Gesarya kuuawa na mme wake kwa kipigo kisha kumpaka sumu ya tumbaku ili kupoteza ushahidi.


  Polisi wanasema mwanamke huyo alitendewa unyama huo kwa kosa la
  kutoamka mapema kwenda kufungua zizi la ng’ombe.

  Mwanaume amjeruhi mjamzito akitaka kuona mtoto tumboni
   
 2. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha kweli, lakini sijaona mantiki ya ku withheld jina la mtuhumiwa asiwe protected inabidi ingekuwepo hata alert ili kuwezesha kupatikana kwa urahisi kwa huyo jamaa.
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Bad newz....
   
Loading...