Mwanaume Aliyetuhumiwa Uchawi Auliwa Kwa Mabomu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume Aliyetuhumiwa Uchawi Auliwa Kwa Mabomu

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Feb 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Thursday, February 11, 2010 2:31 AM
  Mwanaume mmoja wa nchini Burundi aliyekuwa akituhumiwa kuwaroga ndugu zake, amefariki dunia pamoja na familia yake baada ya bomu kurushwa ndani ya nyumba yake. Mwanaume huyo alifariki dunia pamoja na watoto wake watatu wakati bomu liliporushwa na kulipuka ndani ya nyumba yake.

  Tukio hilo lilitokea jioni ya siku ya jumanne katika kijiji cha Itaba kilichopo ukanda wa kati wa Burundi.

  Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Nyandwi aliuliwa baada ya kutuhumiwa kumroga mmoja wa ndugu zake na kupelekea kifo chake.

  Bomu hilo lilirushwa jikoni kwake wakati Nywandwi alipokuwa amekusanyika na mkewe na watoto wake watatu wenye umri kati ya miaka 7 na 15.

  Mabomu yanapatikana kirahisi nchini Burundi na hununuliwa kwa Tsh. elfu moja tu na hutumika zaidi kwenye kutatua migogoro ya ardhi.

  Mwaka 2008 pekee watu 130 walifariki dunia baada ya kulipukiwa na mabomu.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4058442&&Cat=2
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...