Mwanaume aliyeniacha miaka miwili iliyopita baada ya kunifungulia duka anataka kunirudia

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,017
2,154
Nilipompata nilisema nimepata, huyu mwanaume tuliishi vizuri ghafla akaanza kuwa busy.

Katika kubembeleza nijue kulikoni nilinunua khanga na vitenge viende kwa mama yake kama zawadi ya sikukuu. Hiyo ndiyo siku alipofunguka kuwa haina haja kwani hatutakaa tuoane. Nililia, Sikuu ilikuwa chungu sana.

Haya yalitokea akiwa ameshanifungulia duka. Nililiongeza lile duka upande mmoja umekuwa mgahawa na upande wa pili ni grocery.

Sasa huyu mwanaume anataka tuongee, huyu aliyesema hatanioa. Sijui yemkuta makubwa gani huko alikokwenda.
 
Unaonekana unampenda sana huyo mwanaume mkuu maana amesema anataka muongee nawewe umeconclude kuwa anataka akurudie....je kama anataka achukue duka lake hahahaha just joke mkuu..... Subiria afunguke dhamira yake
Kumbeee
 
Kama unamuelewa yajengeni shida zote za nini Fanya vile moyo unapenda

Au humpendi ?
 
Safari hii kajifunza ndo maana karudi
Huwa tukishika adabu sometimes tuna surrender tunarejesha majeshi
Kuachana kurudiana kuachana kurudiana tena ndo mapenz yenyewe hapo mnapendana sema ni tamaa za baharia tu zinamsumbua

Halafu acha kuwaza negative kukuacha ni matokea tu embu suka mkeka huo tuone itakuaje kwenye hio betting yako
Ninampenda sana lakini ninaogopa asije akaniacha tena
 
Sikiliza moyo wako

Lakini yaweza kua
1. Yawezakana kaona unampenda sana hivyo anaona kama amekuwekeza muda wowote akitaka kurudi anarudi na anajua utampokea tu na huna pa kwenda

2. Labda dunia imemfunza amegundua wewe unamfaa zaidi ya huko alikokua
 
Nilipompata nilisema nimepata, huyu mwanaume tuliishi vizuri ghafla akaanza kuwa busy.

Katika kubembeleza nijue kulikoni nilinunua khanga na vitenge viende kwa mama yake kama zawadi ya sikukuu. Hiyo ndiyo siku alipofunguka kuwa haina haja kwani hatutakaa tuoane. Nililia, Sikuu ilikuwa chungu sana.

Haya yalitokea akiwa ameshanifungulia duka. Nililiongeza lile duka upande mmoja umekuwa mgahawa na upande wa pili ni grocery.

Sasa huyu mwanaume anataka tuongee, huyu aliyesema hatanioa. Sijui yemkuta makubwa gani huko alikokwenda.
Duka linaendeleaje lakini?

Ulipolitoa na lilipo leo kuna tofauti gani?
 
Back
Top Bottom