Mwanaume aliyelelewa na mama peke yake, ni mtu wa aina gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume aliyelelewa na mama peke yake, ni mtu wa aina gani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Delegate, Jun 20, 2012.

 1. Delegate

  Delegate JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 35
  Nimeona single mothers wakistruggle kulea watoto wao wa kiume peke yao bila baba za hao watoto kuwepo.

  Je unaweza kumjua mwanaume aliyelelewa na mama peke yake? Je tabia zake zinakuwaje? Anaweza kuwa mwanaume halisi yaani roho ngumu?

  Ninachojua watoto wa kiume wanatakiwa kuwa karibu na baba zao ili wakopy mambo kadhaa kwa baba zao. Je kwa aliyelelewa na pande zote mbili yaani baba na mama na aliyelelewa na mama peke yake wana tofauti???

   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
 3. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sijui tunaelekea wapi ndugu zangu,maana naona zimeanza thread za kujadili watoto wanaolelewa na mzazi mmoja naona mwishoe watakuja kunyanyapaliwa. Mwingine aseme sitaoa mtoto alielelewa na mama peke yake kwa kuwa wanafundishwa vibaya. Hao watoto hawajapenda ni sisi wazazi ndio tuliosababisha yote hayo,sasa kwanini waadhibike kwa makosa yetu???!!!! Mtoto anaweza kulelewa na both parents and still akawa kitu cha ajabu. Hebu tumuweke Mungu mbele kwenye malezi ya watoto na si kuanza kushupalia mambo ya ajabu.
  We have a long way to go my people!
   
 4. Delegate

  Delegate JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 35
  mkuu nimekuelewa nilitaka kujua kama kuna tofauti,sijatupa lawama wala sijamdharau mtu,nilitaka kujua kama hawa wawili wanaweza kutofautiana
   
 5. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  yes thats true Mtambuzi..nimelelewa na mama na nina lelewa na mama na Ben Carson ni role model wangu..yani najaribu kuwa na busara za hali ya juu japokua mapenzi kwa mama yangu hayapungui Ng'oo hata nikioa!!! kanilea kwa shida na raha huyo baba hata kalamu wala penseli yake siijui masaburi yake mekundu..safi sana mama angu najua upo humu JF ..Kisses!:A S-heart-2::A S-heart-2:
   
 6. Delegate

  Delegate JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 35
  mkuu kuna wakati unajihisi kama una mapungufu fulani kwa kitendo cha baba kuwa mbali na wewe utotoni? na vipi baba akija sasa hivi na kutaka kujenga uhusiano na wewe,utamkubalia?
   
 7. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  Antolee ujinga wake hapa.. na akijaribu tu ntamtembezea mapanga ..sioni mapungufu yoyote..though askwambie mtu singe parental si mchezo unaweza ukawa na shida labda ya hela na huna option ya kumuomba mtu mwingine zaidi ya mama na akisema sina ujue imekula kwako..binafsi nimekula good time sana..shule nzuri..maisha mazuri..pocket monie ya kutosha..usafiri safii sasa huyo baba wa nini? sioni hata faida yake maana hakija haribika kitu..!
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Binafsi, nafikiri ni vyema watoto wapewe malezi mema bila kujali kuwa wanalelewa na single mothers au laa. Mitaani kuna mitoto imeshindikana kwa tabia mbaya wakati inalelewa na wazazi wote wawili. Tumeshuhudia hata baadhi ya watoto wa viongozi wa dini (ambao kimsingi ndo tungetegemea wawe mfano kwa sababu ya kupata malezi bora) wakionyesha tabia mbovu mitaani zilizoshindikana.
  Ishu hapa ni kuwapa malezi mema, na sahihi na pia kumuomba Mungu awajalie tabia njema.
   
 9. Soraya

  Soraya JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wanakuwa wanaume wazuri sana.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  ndugu mtoa mada na kwa faida ya wanajamvi wengine, naomba niseme hivi.

  Siku mtoto anazaliwa hachagui kuzaliwa kwenye aina yeyote ile ya maisha bali ni nature ina mchagulia so hana makosa hata kidogo kwa maisha atakayojikuta amezaliwa/amelelewa iwe ni single or awe na wazazi wote. kosa kubwa hapa naliona kwa sisi wazazi wenyewe ingawa muda mwingine mtu unaweza kukosa jinsi basi inabidi ukubaliane na hali halisi ya kuwa mzazi pekee. kwangu mimi kuwa na wazazi wote au mmoja haina mashiko sana iwapo tu mtoto huska atajitambua basi.

  sipendi kuongelea sana jinsia za hawa watoto kwa kuzitengenisha bali nitaziongelea kiujumla wake.
  mzazi wa kike anapolea watoto peke yake anaweza kupata matokeo mawili kwamba ama awalee vizuri na watoto atoke wakiwa watu wazuri kwenye jamii ama walee kimayai watoto watoke wakiwa sio watu wema kwenye jamii.
  Mimi ni mama ila kuna jambo ambalo huwa linaniumiza sana juu ya jinsi tunavyolea watoto mara nyingi.

  Iwapo umejikuta unalea mtoto peke yako kwanza jua kabisa kuwa maisha hayanaga upendeleo hata siku moja so kuwa mzazi pekee isiwe ni sababu ya kumlea mtoto kimayai. Jua kuwa hakuna excuse anazopewa mtoto kwa kuwa alilelewa na mzazi mmoja hata siku moja siku zote maisha yanatoa vitu vyote kwa binadamu wote ila uwezo na uwajibikaji wako ndio unaokufanya upate baadhi na vingine ukose. sijawah kuona eti labda gari limetengenezwa kwamba hili liendeshwe na walio lelewa na mama pekee au baba pekee. vyote hutoka kwa ajili ya wote na juhudi zako binafsi na uwezo ndivyo vitakavyo kupatia.

  Akin mama wengi huwa tunafika mahali tunayasahau haya huku tukijua kuwa maisha hayanaga upendeleo kwa yyte yule. watoto wengi wanaolelewa na baba huwa wanaish kigumu naweza sema na mwishowe wanakuwa very prosperous ingawa siyo wote ila hii ni kwasababu baba siku zote maisha anavyomlea nayo mtoto ni ya kumuwajibisha na kumuonyesha sura halis ya maisha tofauti na sisi akina mama ambao siku zote hupenda kumuonyesha mtoto sura nzuri tu ya maisha na kusahau upande wa pili.

  wamama wachache sana waliweza kumudu maisha ya kulea watoto peke yao wakawa prosperious kama aliyetuonyesha Mtambuzi na huyu ilitokana na ukweli kuwa mama yake alimuonyesha mwanae sura ya pili ya maisha kuwa kuna juhudi binafsi na wewe kulelewa bila baba haikupi excuse ya kutokuwajibika. alimnyima mwanae kuangalia TV na kumpa homework nyingi ili kumjengea dhana ya uwajibikaji na hii ilimtoa huyu mtoto. binafsi nimependezwa sana na aina ya mama kama huyu ambaye kwake yeye maisha yako fair kwa kila mtu, ila uwajibikajai tu ndio unoleta tofauti.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndio. Wanakuwa na matege

  (Swali la kipuuzi zaidi ya bajeti)
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kaka tupo wengi,nani kama mama bwana? namshukuru sana mwalimu mama mtolera maana kazi yake ya malezi bora ndio imenifikisha hapa nilipo,tabia nyingine zinakuwa si kwa sababu ya malezi ya mama bali mtu binafsi na makundi aliyopitia.i love my mum mtolera,ahsante sana,sina cha kukulipa kiukweli.love mama
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu andres batta kwanza pole sana kwa kulelewa na mzazi mmoja ingawa baba yupo. Najua inakuuma sana kwani kuna vitu ulitamani uvipate na pengine Mungu alikusudia uwe navyo ila kwakuwa baba alikosa uwajibikaji juu yako basi amekufanya usivipate. Kweli nakupa pole ila pia siyo vya msingi sana manake avijuaye ni Mungu pekee.

  Naomba sana ndugu yangu na wala sitaki kuinglia personal life yako hata kidogo and please have mercy on me nisikilize kwa hili.
  Don't dare kulumbana au kumtukana au hata kumpiga baba yako kwa kosa la kutokuwajibika juu yako. kamwe nakuomba usifanye hayo. Nauona uchungu ulioko moyoni mwako manake najua jinsi alivyokuumiza sana ila maisha hayako hivyo kaka, kwenye maisha huwa siku zote kinachoangaliwa na Mungu ni hiki " wewe unapaswa ufanye nini juu ya mtu mwingine na wala haangalii huyu mtu alikufanyia nini wewe". Alikulea ama hakukulea hilo ni juu yake na Mungu wake wewe kama mtoto chukulia kawaida wala usijaribu kugombana naye siku akikwambia kuwa yeye ni baba na anataka kitu fulan toka kwako, kama huna amani ya kumpa usimjibu kijeuri wala nini tulia kimya au mwambaie mambo siyo mazuri basi.

  Najua mtoa mada alitaka kutunyesha jinsi ambavyo wazazi wa kiume wanavyopanda chuki kwenye nafsi za watoto pale wanapokataa kuwalea. jambo hili ni ukweli usiopingika ila mimi siungi mkono chuki hii iendelee manake unayomambo mengi sana ambayo unataka Mungu akutendee so ukiweka hasira na chuki utajikwamishia mwenyewe.

  Nakuomba sana nisamehe manake najua nimeharibu hata siku yako mpendwa kaka yangu ila pia nimalizie kwa kumpongeza mwanamke mwenzangu kwa kukulea mpaka hapa ulipofikia abarikiwe sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  nakubaliana na wewe kabisa
  Tusianze kusema mtoto aliyelelewa na mzazi mmoja ana hili wa lile au atakuwa na tabia hizi au zile
  tabia ni mtu mwenyewe na ni makundi aliyokutana nayo au anayokaa nayo au kushirikiana nayo wala haina muunganiko na malezi yake kwa baba na mama au ya kulelewa na single parent. Ni jambo la kumuomba sana Mungu kwenye issue ya malezi ya watoto maana mtoto anaweza kuharibika hata akiwa na malezi ya wazazi wote wawili.
  Na vile vile unaweza ukawa na wazazi wote wawili ila ukajikuta kama vile una mzazi mmoja kutokana na upande mmoja kutojihusisha kabisa na malezi ya mttoto
  Tumuombe Mungu sana atujalie busara na hekima na ukaribu na watoto wetu kuweza kuwalea katika malezi ambayo yana uwepo wa Mungu na watoto wakue wakijua kuwa kuna Mungu
  Haya ya kusema sijui malezi ya kulelewa na mzazi mmoja yana hili na lile tuachene nayo kabisa
  Wapo waliolelewa na mzazi mmoja na wako vizuri sana na wana maendeleo mazuri sana na wapo ambao walilelewa na wazazi wote ila ni balaa
   
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  mtoa mada huu uzi umeniumiza sana. yaani siku yote nitajikuta nawaza haya. but nafurah sana kuona kuwa wanawake wenzangu wamefanya kazi kwa watoto wo hadi kuwafikisha hapa walipo.

  MAMA NI MAMA TU. NA NDIYE MZAZI WA KWELI KWA MTOTO.

  Ee Mungu bariki kazi za akina mama wote, wape hekima ujasiri na nguvu ya kustahimili manyanyaso wanayoyapata kwa wenzao akina baba. Panda hekima na busara ya kimungu katika mioyo yao ili wawalee watoto wao katika hekima na kimo wakikupendeza wewe na wanadamu pia.

  AMEN!
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu samahani kama nitakaloongea litakuudhi
  Ila napenda sana kukuomba na nanua wewe ni muumini na unajua uwepo wa Mungu katika maisha yako
  Najua ni jambo baya sana alilotenda huyo ambaye ni baba yako kutokuwa karibu na wewe au kujua au kushiriki katika malezi yako
  Ila naomba nikuombe sana watu wanasema mkono ukinyewa na mtoto huukati ule mkono ila unaufuta na kuuosha na maji na unaendelea na mambo mengine
  Limekwishatokea maishani mwako na baba yako kutokuwa karibu na yeye ila nikuombe tena samahani sana msamehe na mpe nafasi ile ya kuwa baba yako japo kumuona na kujua kuwa huyu ndie baba yangu yatosha
  Inatosha kumjua ila usimpe nafasi ya kukupangia lolote la maisha yako maana kwa sasa naamini una mipango yako na una mambo yako umekwishajiwekea ya maendeleo yako
  Mpe nafasi, msamehe kwa makosa yake na muombee Mungu hata watoto wake wasiwe kama yeye kuwakataa watoto wao
  Msamehe na mwachie Mungu ampe kile anachostahili ila usichukue nafasi ya kuweka kisasi moyoni mwako kwa ajili ya yale aliyokutendea
  Maandiko yanasema mwachie Mungu kulipa kisasi na usilipize kisasi kwa mtu yoyote
  Samahani sana kama nitaharibu siku yako
   
 17. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ngoja nilale kwanza
   
 18. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #18
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Umeongea mengi lakini mi nimepapenda hapo tu..yani huyo baba aniombe hela kwani hata tukipishana bara barani ananijua?? na akithubutu tu ntamzabua mimbata!
   
 19. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Heshima ni kitu cha bure!! Jiheshimu!
   
 20. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kulelewa na mama na baba kama wote wapo hai ni jambo zuri sana then ukute wazazi wanaishi kama marafiki ndani ya nyumba ni jambo la kufurahisha sana uhu ndio mfano niliochukua kwa wazazi wangu wananipa shauku nami nije kumpenda mke wangu na watoto wangu.wakati nipo mdogo nakumbuka baba alikuwa anamsahidia mama kupika kama mama ni mdhaifu hadi sasa hiv kuna wakati baba anaweza andaa meza wakati wa msosi upand wa vinywani na matunda.mwanzo mwisho nilpofurahia maisha ya kulelewa na wazaz wote ni SIKU YA JUMAPILI tunaenda wote church nyumba nzima hadi dada wa kazi watoto wote nyuma ya pick up hilux .duh wacha kabisa ilikuwa rhaaaaa , kama mtoto atalelewa na baba na mama wenye mapenz ya kweli anayomeng ya kujifunza katika kuja kuijenga familia yake.
   
Loading...