Mwanaume alivyotumia sura mbaya kupata umaarufu, marafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume alivyotumia sura mbaya kupata umaarufu, marafiki

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Sep 18, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  “NILIPOSIKIA juu ya mashindano ya wanaume wenye sura mbaya sikusita kushiriki kwani nilijua ni lazima niibuke na ushindi,” anasema Sultani Masoud maarufu kwa jina la Sura Mbaya.

  Masoud Sura Mbaya kama anavyojulikana sasa ni msanii ambaye alivuma miaka ya 90 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya mwanamume mwenye sura mbaya.

  Kwa mara ya kwanza alishiriki katika mashindano ya wanaume wenye sura mbaya yaliyofanyika Buguruni Dar es Salaam na kuibuka mshindi wa kwanza ambapo alipata zawadi ya redio.

  Mashindano hayo ya kusisimua yalifanyika kwa mara ya pili katika Wilaya ya Kinondoni ambapo, Masoud aliwashinda wasanii wengine maarufu wakiwamo mwanamuziki wa siku nyingi Remmy Ongala na msanii maarufu wa vichekesho Khalid John, maarufu kama Mzee Jangala.

  Masoud anasema anaamini kuwa hakuna mwanamume mwenye uwezo wa kumnyang’anya nafasi hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ana uwezo wa kubadilisha sura yake kwa kutumia hisia mbalimbali. “Mimi ni sura mbaya nambari wani Tanzania…wa kunishinda hajapatikana.

  Wapo waliojaribu kukata rufaa kupinga ushindi wangu lakini niliwashinda hata kwenye rufaa…najivunia ushindi wangu na kila ninapojiangalia kwenye kioo naona wazi kuwa nina haki ya kushinda,” anasema Masoud.

  Ingawa hivi sasa anajivunia sura yake, maisha yake ya utotoni hayakuwa ya furaha kwa kuwa alichukizwa na tabia ya vijana wenzake waliopenda kumtania kwa kumuita sura mbaya. Kitendo hicho kilimsababishia hasira za mara kwa mara na kujiona mpweke.

  Mama yake alikuwa akimliwaza na kumsihi apuuzie utani wa vijana hao kwa kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kujichagulia sura wala umbile na hivyo kukasirika ni kumkufuru Mungu.

  “Mama alisema sura niliyonayo inatokana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu hivyo ninapaswa kumshukuru na kujinyenyekeza mbele zake kwa kuwa hakuna anayemzidi Allah.

  “Niliamua kuzingatia ushauri wa mama yangu na baada ya muda niliona utani huo kama jambo la kawaida…waliniita sura mbaya nami niliitika bila kukwazika jambo ambalo limenipatia umaarufu na marafiki wengi,” anasema Masoud.

  Masoud ambaye anaishi Ilala jijini Dar es Salaam anasema anatamani mashindano hayo yafanyike tena ili apate fursa ya kuwaburudisha Watanzania kwa kutumia anachokiita kipaji chake katika sanaa.

  Masoud anafurahia mashindano hayo kwa sababu yanampatia fursa ya kupata marafiki wapya pia kukutana na watu wengine wanaodhani kuwa wanasura mbaya.

  “Kwa kuwa mimi ni msanii…ninafurahi kuona kuwa wapo watu wanaoburudika kutokana na uwezo wangu wa kubadili sura kulingana na hisia,” anaeleza.

  Masoud alishiriki pia katika mashindano ya pili ya kumtafuta mwanamume mwenye sura mbaya ambayo yalifanyika Kinondoni na kupata zawadi ya TV baada ya kuibuka mshindi wa kwanza.

  Baada ya ushindi huo, Ongala alikata rufaa na kudai kuwa Masoud alipendelewa. Hata hivyo Masoud alishinda katika rufaa hiyo jambo lililomuongezea umaarufu.

  Kuanzia kipindi hicho amekuwa akishiriki katika matamasha ya wasanii mbalimbali na sherehe ambapo watu humkodisha ili atoe burudani.

  Anasema ubunifu na kipaji cha kubadili sura ni mambo yaliyomwezesha kuibuka na ushindi katika mashindano hayo yaliyosisimua washabiki wanaopenda michezo inayoambatana na vituko.

  Katika mashindano hayo washiriki wanapaswa kuonesha sura mbaya wakati wa kucheka, huzuni pia sura mbaya ya mtu anayeshangaa jambo.

  “Nakumbuka siku ya mashindano watu walianza kucheka mara nilipojitokeza. Sikujali, nilipanda jukwaani na kuonesha sura ya kukasirika…watu wakacheka sana…nikaamua kuhuzunika kama mtu aliyefiwa na mama mzazi, watu wakaendelea kucheka.

  “Baada ya kuona wanacheka sana nikabadilika na kuonesha sura ya kushangaa watazamaji wakaendelea kucheka. Nilipoamua kucheka watazamaji walianza kulalamika mbavu zinawauma kwa kucheka mno.

  Haukupita muda nikatangazwa kuwa mshindi wa kwanza jambo lililoungwa mkono na watazamaji ambao walipiga miluzi na vifijo,” anasema.

  Mashindano hayo ya aina yake alimfanya Masoud kuwa maarufu na kupata marafiki wengi. Pia baadhi ya watu walikuwa wakigombania kupiga naye picha ili waweze kupata ukumbusho.

  Ingawa mashindano hayo yalipokewa kwa mtazamo tofauti huku baadhi ya watu wakiyapinga kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa na kwamba hakuna mtu mbaya, Masoud anataka yaendelee kwa kuwa kinachoshindaniwa ni ubunifu wa sanaa ya majukwaani.

  “Sura mbaya ilikuwa ni kigezo cha kuingia kwenye shindano lakini ushindi unapatikana kutokana na ubunifu wa kuvuta hisia za watu kama vile kuchekesha, kuhuzunisha, kushangaza au kukasirisha,” anasema.

  Masoud amezaliwa jijini Dar es Salaam mwaka 1966 akiwa mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa familia ya Masoud yenye watoto watano wa kiume na wawili wa kike. Inadaiwa Masoud anafanana na dada yake ambaye ni wa kwanza kuzaliwa.

  Amepata elimu ya msingi katika Shule ya Msimbazi Mseto kuanzia mwaka 1977 na kuhitimu mwaka 1983.

  Kwa kuwa mama yake hakuwa na uwezo wa kumwendeleza kimasomo, Masoud aliishi kwa kufanya vibarua hadi alipopata kazi ya kutunza viti katika baa inayofahamika kwa jina la Bonga iliyopo Ilala, Dar es Salaam.

  “Sikuwahi kuwa na ajira bora…nilipata kibarua katika baa ya Bonga na kazi yangu ilikuwa kuingiza viti ndani wakati wa kufunga baa…nilifanya kazi hiyo takriban miaka nane na kupata ujira mdogo kwani hata kazi yenyewe haikuwa kubwa,” anaeleza.

  Baada ya baa hiyo kufungwa, Masoud aliamua kujiajiri mwenyewe na kununua toroli kwa ajili ya kusomba maji.

  Kutokana na ukosefu wa maji katika Jiji la Dar es Salam, vijana wasiokuwa na ajira hufanyakazi ya kuchota maji kisha kuyauza kati ya Sh 50 hadi Sh150 kwa ndoo moja.

  Pia baadhi ya familia hukodisha vijana wenye mikokoteni na kuwapa kazi ya kusomba maji kwa ujira mdogo. Hata hivyo Masoud anasema kuwa sasa yeye hafanyi kazi ya kusomba maji.

  Toroli lake linatumiwa na kijana anayesomba maji kisha kugawana fedha kidogo zinazotokana na kazi hiyo isiyo rasmi.

  Kwa mujibu wa Masoud, fedha iliyotokana na kazi ya kusomba maji ilikuwa ndogo na haikuweza kutosheleza mahitaji ya siku na hivyo alilazimika kutumia kipaji chake katika sanaa kama njia ya kujipatia kipato.

  “Kwanza kabla hujaendelea nataka unijulishe unanilipa shilingi ngapi baada ya mahojiano haya…mimi hapa nikokazini.

  Mambo yote yanayohusiana na sanaa siwezi kuyaelezea pasipo malipo kwa kuwa ndio kazi yangu….hii sehemu ya ajira binafsi hivyo najua lazima hapa nitapata riziki,” Masoud alimdai Mwandishi wa makala haya.

  Baada ya kuelezwa kuwa waandishi wa habari hawana utaratibu wa kutoa malipo ili kupata habari, Masoud alijitetea kwa kusema, “wewe usinilipe ila msaidie shangazi yangu mzee asiyejiweza ili aweze kupata angalau mlo mmoja kwa siku ya leo.”

  Anaendelea, “ona sasa ni saa tisa alasiri na bado sijapata fedha ya kumnunulia shangazi yangu chakula ili aweze kupata futari…shangazi anazingatia misingi ya dini ya Kiislam hivyo nina changamoto ya kuhakikisha anapata futari na daku kwa kutumia kipato halali….siwezi kuiba wala kupokea hongo.”

  Anasema changamoto inayowakabili wasanii wadogo ni ukosefu wa mitaji ya kujiendeleza, hulka ya Watanzania kupuuzia vipaji vya wasanii, kudharau kazi za sanaa na elimu duni miongoni mwa jamii.

  Anawashauri vijana wasiokuwa na ajira kuacha kujiingiza katika vitendo vya uhalifu badala yake watumie vipaji na nguvu zao kubuni miradi itakayowapatia ajira binafsi.

  Anafahamisha kuwa vijana wanaojiingiza katika vitendo viovu wanaongeza umasikini, simanzi na majonzi katika familia hasa kwa akinamama.

  “Mama ni mtu muhimu sana, anastahili heshima ya kipekee kwa sababu bila yeye tusingeiona dunia…hivyo nawasihi vijana waepuke vitendo viovu kwa sababu vinasababisha majonzi kwa mama zetu,” anaeleza.

  Anafahamisha kuwa mama yake mzazi alifariki mwaka 2000 na kwamba anaendelea kumuenzi kwa kujiepusha na vitendo viovu, kuheshimu kila mtu, kudumisha upendo na mshikamano baina ya ndugu, majirani, jamaa na marafiki.

  Ingawa Masoud anaweza kubadili sura yake na kuonekana kama mtu anayetisha, watu wa eneo waliopo karibu naye wanaeleza kuwa ana upendo, mcheshi, mpole, mtiifu, mnyenyekevu na anayependa kuheshimu watu wa rika zote.

  Jina la Sura Mbaya limempatia umaarufu na marafiki wengi wakiwepo watoto ambao wanapenda kumtania. Masoud anasema katika maisha yake amewahi kuwa na mpenzi mmoja ambaye amezaa naye mtoto wa kiume anayeitwa kwa jina la Rashid Maghembe Sultani.

  “Mimi nimejitahidi kuepuka kuwa na wapenzi wengi…sio kwa sababu watu wanasema sura yangu mbaya bali ni kwa sababu naogopa kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi…nimeamua kuwa na mpenzi mmoja maishani ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Ukimwi,” anaeleza.

  Masoud anaunga mkono kampeni ya kitaifa ya kupambana dhidi ya Ukimwi kwa kusema kwamba,Tanzania bila Ukimwi inawezekana endapo wanaume wataamua kuacha tabia ya kuwa na wapenzi wengi na kuzingatia maadili ya ndoa.

  “Nasema wanaume kwa kuwa ndio wanaofanya uamuzi kuhusiana na masuala ya mapenzi…wasipotoka nje ya ndoa na kujenga tabia ya uaminifu inakuwa rahisi kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi,” anasisitiza.

  Masoud anapendelea mchezo wa mpira wa miguu na wakati alipokuwa shule alikuwa anacheza winga ya kulia. Hivi sasa ni mshabiki wa timu ya Simba na anasema,” Simba ni Taifa Kubwa lisilotingishika.”

  Masoud anapenda kutembea na redio yake ndogo ili aweze kusikiliza vipindi mbalimbali.Anapenda Muziki hususani wa bendi ya Ottu Jazz wana Msondo Ngoma.

  http://www.habarileo.co.tz/wikinyota/?n=3609
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

 3. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=H8sl4tDOZ2o[/ame]

  ....naona Muziki Munene wampatia Steve umaarufu wa Dakika kadhaa....
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Don't compare yourself with any one in this world.
  If you compare, you are insulting yourself.
   
Loading...