Mwanaume akikimbilia pangoni muache!

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Wanaume ndo wanajua siri ya kukimbilia mapangoni wakipatwa na shida au matatizo ya msongo wa mawazo na wakitoka huko wanakuwa bomba sana. Moja ya tofauti kubwa kati ya wanaume na wanawake ni jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo.

Mwanaume akiwa na msongo wa mawazo hujitenga, huwa mwenyewe na huwa mkimya na hataki kuguswa wala kuongeleshwa na mtu yeyote, wakati mwanamke hujisikia kuogopa na kuathirika kihisia.
Mwanaume hujisikia ahueni atakaposhughulikia tatizo lake yeye mwenyewe bila kuhitaji msaada wakati mwanamke hujisikia ahueni pale atakapokuwa anazungumza au kuongea kuhusu Matatizo yake na mtu mwingine anaweza kuwa mume wake au mtu yeyote anayemwamini.

Mwanaume akipata msongo wa mawazo iwe kukasirishwa kazini, au Matatizo yoyote hujitenga na kwenda kwenye pango (cave) lake katika akili zake ili kuendelea kupambana na kupata solution ya tatizo lake peke yake.
Huwa anakuwa anajihusisha zaidi na kushughulikia tatizo lake na kuwa kama vile amepoteza uwezo wa kutoa ushirikiano kwa mke au mpenzi wake kwa zaidi ya asilimia 95.
Hujitenga, huwa mbali kimawazo, huwa kama amejisahau kwamba ana mke ambaye anahitaji kumsikiliza.
Anakuwa yupo kimwili na si kiakili kwani asilimia 95 zinakuwa kwenye kushughulika na tatizo lake.
Akiwa katika hali ya msongo wa mawazo inakuwa ngumu sana kumpa mwanamke attention kubwa na hisia ambazo mwanamke anastahili.
Na ikiwa atapata solution kwa tatizo lake basi haraka sana atatoka kwenye pango lake ambapo alikuwa amejificha na kurudisha ushirikiano kwa mke au partner wake kama kawaida.
Na kama hatapata majibu ya Matatizo yake basi anaweza kukwama huko kwenye cave lake kwa muda mrefu zaidi.
Wakati mwingine ili wasikae muda mrefu kwenye pango utaona wanaume wanapenda sana kusoma magazeti, kuangalia news kwenye TV, kufanya mazoezi nk.

Kwa mfano!
Mzee Kimbweka na Mkewe Madame flani wote wamerudi nyumbani hoi wakiwa na msongo wa mawazo baada ya mabosi wao kuwakasirisha huko kazini.
Baada ya kufika nyumbani Mzee Kimbweka anaamua kupoteza mawazo yake kwa kujisomea gazeti la Kilimo cha kisasa na hataki kabisa kusumbuliwa na mtu kwani bado anatafakari jinsi ya kupata solution baada ya bosi kumkasirisha kazini.
Wakati huohuo mkewe naye (Madame Flani) baada ya kurudi home huku amechoka na kelele za bosi anataka kuongea na mumewe Kimbweka ili kupata ahueni ya visa vya bosi.
Hii ina maana kwamba Mzee Kimbweka baada ya kutatizwa na bosi ameamua kukimbilia kwenye cave lake hataki kuongeleshwa na mtu na wakati huohuo na mke wake naye (Madame Flani) anataka kusikilizwa na mumewe kwani bosi naye kamjeruhi.
Bila shaka kila mmoja akiamua kufanya kile anataka hata kama wanapendana sana bado kutakuwa na zogo na kukwazana ajabu.
Mzee Kimbweka atadhani mkewe Madame flani anachonga sana na hataki kumpa muda, na Mke naye atamuona mzee hamjali na hataki kumsikiliza.

Hili ni tatizo la mahusiano mengi na ili kutatua tatizo hili haitategemea ni kiasi gani Mr. Kimbweka anampenda kiasi gani mkewe Madame flani bali ni kuhusiana na uelewa wao wa tofauti zilizopo kati ya mwanaume na mwanamke na jinsi ya kumpa mwenzake kile anastahili.

Mwanaume akipatwa na msongo wa mawazo au tatizo, kama wewe ni mwanamke kwanza utajua tu hasa jinsi anavyojiweka kivyake na hata ukimuuliza je, unatatizo lolote?
Bila shaka jibu utakalopata mwanaume atakwambia hakuna shida nipo safi tu na pia atakwambia shida yake haikuhusu wala usijali
(hata kama ni usiku wa manane usingizi hana bado atakwambia hakuna shida yoyote hapo jua jamaa yupo pangoni usimsumbue)
Ujue hapo yupo kwenye pango (cave) anahitaji muda wake mwenyewe ili ashughulikie tatizo lake.
Kuendelea kumsemesha ni sawa na kuendelea kumfuata kwenye cave lake na matokeo unaweza kuliwa au kuumizwa na nyoka anayelinda cave lake (hasira, matusi, kupigwa, kutokujibiwa chochote au kuvurugana kabisa)
Kitu cha msingi kama ni mwanamke ukishaona dalili za kuwa jamaa ameenda pangoni wewe ni kuachana naye, fanya vitu vingine kujipa raha zako mwenyewe ndipo utashangaa jamaa katumia muda kidogo kukaa huko mapangoni.
Kumchungulia mwanaume pangoni au kumfuata pangoni na hata kuendelea kumsemesha akiwa pangoni hakumfanyi awahi kutoka pangoni, bali kunaweza kusababisha akwame huko na kubaki huko kwa muda mrefu zaidi. Dawa ni kumpa muda wa kutosha na kuachana naye kabisa hadi amalize muda wake na atarudi mwenyewe.
207510_416089301777729_418061691_n.jpg



AMEN..............!
 
Thank you for a lesson.
Mi huwa nagombana na mheshimiwa, kwenye kitchen party nilifundishwa kuwa akiwa down nimliwaze, lakini yeye ukimkaribia anakuwa mbogo.
From sasa, nitakuwa namuacha tu
 
Thank you for a lesson.
Mi huwa nagombana na mheshimiwa, kwenye kitchen party nilifundishwa kuwa akiwa down nimliwaze, lakini yeye ukimkaribia anakuwa mbogo.
From sasa, nitakuwa namuacha tu

Hahahahaaa pole , anakuwa yupo pangoni mpe muda......!:becky::becky:
 
yaani sijamaliza maana unaniacha hoi balaa nice kitchen party kwa kina noninoo..
 
Ole wake B/f akimbilie pangoni, tutakutana huko huko. Hakuna kumwachia nafasi hata kidogo. Siwezi kumuacha wakati nami namhitaji aniliwaze
 
Ole wake B/f akimbilie pangoni, tutakutana huko huko. Hakuna kumwachia nafasi hata kidogo. Siwezi kumuacha wakati nami namhitaji aniliwaze
utakuwa humtendei haki!hawa watu wana aina yao ya kufikiri!ni bora umuache akirudi hurudi omba ile mbaya!mwenyewe utafurahi!
 
Hahahahahahh Aseeee mwendo wa kumfata pangoni ka fuko lol
Ole wake B/f akimbilie pangoni, tutakutana huko huko. Hakuna kumwachia nafasi hata kidogo. Siwezi kumuacha wakati nami namhitaji aniliwaze
 
HASWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA............................!!
Hii thread nimeipenda asikwambie mtu, nimeikubali sana!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom