Mwanaume akikataa mimba au kukutelekezea mtoto, usitumie majina yake Kwa mtoto wako

Stupid,stop putting blames on one side. Do you the think the act was done by one human???
Wewe ndo stupid mwenyewe sasa. Unafungua miguu mtu aingie na unajua kabisa upo kwenye "HEAT" halafu unataka usilaumiwe?!

Mabinti mmekuwa Kama mapepo hivi saaa
 
Stupid,stop putting blames on one side. Do you the think the act was done by one human???

kubeba mimba kwa mwanamke ni kutaka, hakuna mimba ya bahati mbaya. tungekua tunazungumzia wsichana wa 21-15 hiyo ingekua ni mada nyengine, lakini sio kwa hawa waliopevuka.
 
Kwema Wakuu!

Lazima tutende haki, lazima tuseme ukweli.
Wanawake wanamakosa Yao Kama tulivyo Sisi wanaume tunamakosa yetu.
Na mwenye makosa lazima aadhibiwe, na akiomba Msamaha sharti asamehewa lakini adhabu inaweza kubaki palepale.

Taikon huwaga ni mtu wa kuongea mambo magumu yasiyo rahisi, bila kujali yanamgusa Nani, iwe ni Mimi au wewe au Yule. Lengo ni kuweka mambo Sawa Kwa Haki. Ingawaje nafahamu Haki haitawezekana Kwa Asilimia 💯.

Najua wapo wanawake walifanya makosa Kwa kujibebesha mimba kimakusudi Kwa wanaume Kwa malengo Fulani, mathalani
1. Kwa lengo la kuolewa
2. Kwa lengo la Mali
3. Kwa lengo kupendwa

Hata hivyo zipo mimba zilizoingia Kwa bahati mbaya(bila kupanga baina ya mwanaume na Mwanamke).

Makosa ni makosa tuu. Lakini haimaanishi watu waendelee kujilaumu Kwa makosa waliyoyafanya. Lazima maisha yaendelee.

Amekataa mimba!
Amekubali mimba lakini kakataa kumlea mtoto.
Amekubali lakini ameshindwa Kumlea mtoto.

Ikiwa Baba mzazi amekataa au kushindwa kumlea mtoto Kwa sababu yoyote Ile isipokuwa sababu ya kifo au Maradhi basi nakushauri Usimpe mtoto Ubin wa huyo Baba Mzazi.

Amua kumpa jina lolote lile utakalolipenda, aidha ni jina la Wajomba zake wanaokusaidia kumlea, au jina la Baba yako(Babu yake upande wa Mama).

Wala sio dhambi.
Wala hakuna shida yoyote.
Kila mmoja awajibike Kwa makosa yake.

Wakati wewe ukiitwa single Mother, ukitukanwa na kuonekana Malaya, au mwanamke usiyefaa, iwe ni kweli au sio kweli, iwe ni Kwa bahati mbaya au makusudi lakini akakataa na ukazalilishwa na kuyapitia machungu.

Ukamenyeka kumlea mtoto Kwa halali na haramu wakati Baba yake anayetakiwa kutoa matumizi yupo anarandaranda huko, hata Kama Hakuwa na chakutoa lakini hata salamu na kukutia moyo alishindwa, ninachoweza kukushauri ni kubadilisha tuu Ubin WA mtoto.

Hakuna atakayekuuliza,
Na hautaonekana mbaya popote pale.

Hoja ya Msingi hapa ni kuwa, atakayemlea mtoto ndiye mwenye mamlaka naye.
Yeye ndiye ataamua aitwe Nani, ataamua jina la pili na latatu liwe la Nani.

Maana Vijana wa siku hizi tumezidi sasa.

Iwe ni Mimi Taikon au Nani, Kama umezaa na Mimi alafu nikaleta uhuni wa kukataa mimba au kushindwa kuhudumia mtoto, usitumie jina langu. Sistahili.
Na mtoto huyo hastahili kutumia jina langu.

Wanawake msiwafundishe watoto wenu kuwachukia Baba zao, nyie waleeni Kwa maadili ya kimila na Kidini, tumieni majina mtakayopenda ninyi, watoto wanavyokua wanajionea na kujua ni zipi sababu za nyie mama zao kufanya mlio ya fanya.

Lakini jitahidini kuwa wema ili watoto wasijeona kuwa ninyi ndio Wabaya.

Wito Kwa Vijana; msikimbie mimba wala msikimbie Kulea watoto.
Hata Kama huna chochote kitu, angalau mjulie hali mtoto au mzazi mwenza. Mtie moyo, kubali kubeba lawama Kwa maana wanawake ni watu wa lawama hata ungemuoa, lakini wakitulia na kutafakari wenyewe wanaelewa.

Mwanamke ukiwa mwema kwake hata Kama huna kitu anajua, anajali ingawaje atakutolea maneno ya shombo. Lakini haiondoi ukweli kuwa nao wanajisikia vibaya unavyoteseka.

Lakini Kulea mtoto hulei,
Kusalimia husalimii wala kumjulia Hali,
Mwanamke akiwa mkali kwako nawe unajifanya kiburi na jeuri Kwa maneno ya kashfa.
Unafikiri hata ungekuwa wewe ungefanyaje?

Hapo ndipo wanaume tunapokosea.
Saikolojia ya Wanawake ni kuendeshwa na mihemko, kulia upesi na kutoa maneno ya shombo kwao ni ishu ya kawaida lakini haimaanishi hawajali wala haimaanishi hawana akili ya kushindwa kutuelewa.

Mwanamke anahitaji Upendo(kujaliwa, kutiwa moyo, kufarijiwa, kupewa maneno matamu na laini, kushauriwa,)
Ukiyaweza hayo mwanamke kama alikuwa na hisia na wewe hawezi kukuchukia hata Kama humlei mtoto wake. Kwani wanaelewa.

Kitu kingine, wanawake ndio viumbe pekee ambao wanaelewa watu wanaojali hisia zao.

Unaweza kumhudumia Mkeo kila kitu(materials) kamwe hawezi kumnyang'anya mtoto wa Baba mwingine aliyezaa naye akakupa wewe ikiwa Bwana huyo bado anamjali na kumpenda.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Kheee we kijana
 
Sawa. Kuna ambao wameishi Kama mke na mume (bila ndoa rasmi), mpaka wakapata mtoto. Mtoto akiwa na mwaka mmoja, binti akaanza Tabia zisizofaa mpaka akalazimisha kutengana/kuachana.

Jamaa akaona asilazimishe Mambo, akaondoka akaenda kupanga sehemu nyingine. Baada ya jamaa kuondoka, binti naye kaondoka Kwa kutoroka akahamia mahali pengine, akamblock jamaa na baada ya muda akabadili kabisa namba.

Kuna kituo ambapo mtoto hushinda (day care), hivyo ili jamaa amuone mtoto analazimika kwenda pale kituoni!

Katika mazingira ya namna hii, unaendelea kumtetea mtoto WA kike?!

Baada ya kuondoka, binti hataki kabisa Baba mtoto ajue wapi wanaishi! Na Kwa kuwa amemblock na baadaye kubadili namba, jamaa Hana namna anaweza kutoa matunzo. Mbaya Zaidi jamaa anaambiwa na watu baki kwamba mama mtoto analalamika kwamba Baba mtoto hakuna anachofanya Kwa mtoto!

Hii ni kesi ya pili (inayofanana), ambazo mabinti wamenfanya nilizothibitisha.

Unaachaje kumtia mtu risasi katika Hali Kama hii!

Utaweza kusema Baba ametelekeza mtoto?

NASISITIZA TENA, KAMA HUJAOA USIJARIBU KU-BET FURAHA YAKO, au AMANI YAKO.
Dah mkuu hii comment yako ni ya 2022 lakini hiki kitu kimenitokea mimi mwaka huu 2024 hakika mwanamke ni kiumbe wa ajabu sana ana block namba zote hataki mawasiliano hapo mtu unatoaje huduma na hataki ata ukue yuko wapi na mtoto aseeee inabidi mtu ukae kimya japo unaumia na mtoto anateseka kwasababu ya tabia za mama yake kujifanya anaweza mambo yote
 
Dah mkuu hii comment yako ni ya 2022 lakini hiki kitu kimenitokea mimi mwaka huu 2024 hakika mwanamke ni kiumbe wa ajabu sana ana block namba zote hataki mawasiliano hapo mtu unatoaje huduma na hataki ata ukue yuko wapi na mtoto aseeee inabidi mtu ukae kimya japo unaumia na mtoto anateseka kwasababu ya tabia za mama yake kujifanya anaweza mambo yote
Duh, 2024? Mbona umepigwa goli la mapema sana mkuu!!
 
Ni changamoto sana
Pole sana.
Madam umezaa naye hapo ameshapata fimbo ya kukuchapia. Atakuwa anakuumiza kupitia mtoto kupitia aina ya malezi. Na hivi wanavyojua kulea kwa kuigana bila ya kuzingatia misingi ya malezi...I real feel sorry kwa mtoto na kwako.
Mwanamke ni mtu anayetamani kuzaa sababu tu kaona mwenzake ame post mtoto au amebeba mtoto, au akatamani kuzaa sababu kaona mwenzake kabeba mbwa
 
Mpe mtoto haki yake.
Huyo unaemuandika ndie baba yake??
Sasa kama baba kakimbia nyumba ndio anapoteza hata watoto aliobaiojoiana na mkewe.

Ni haki ya mtoto kumjua baba yake, awe katili, mvivu, mlevi huyo ndio baba yake na hatopata baba mwingine duniani zaidi ya huyo.

Mwisho wa siku baba akijipata, au akakubali kulea mtoto, mtoto atapagawa mbona majina yangu si ya baba yangu, na hili pia litachangia baba kusepa au kukataa mtoto mazima maana hata jina sio lake anawajibikaje.

Kwenye uzi wako hujataja ni kwa muda gani baba akikimbia au kukataa mtoto basi agawiwe mwanaume mwingine.
Je ni mwaka, mwezi au on the spot pale anapokataa.??

Nadhani bandiko hili umetumia hisia zaidi na sio akili.
Umeumizwa na kina baba wa namna hiyo ukawaanzishia thread.
 
Wanawake msiwafundishe watoto wenu kuwachukia Baba zao, nyie waleeni Kwa maadili ya kimila na Kidini, tumieni majina mtakayopenda ninyi, watoto wanavyokua wanajionea na kujua ni zipi sababu za nyie mama zao kufanya mlio ya fanya.
Taikoni umekuwaje siku hizi mkuu??

Yaani usimfundishe mtoto kumchukia baba yake na wakati huohuo cheti chake kina jina la mjomba??

Kama mama kashaanza kuonesha chuki kwa kubadili jina mtoto lazima afate tu..

Na kumbuka kuna muda Me hukataaimba kwasababu za ukata, mambo yakiwanyookea huja kumgomboa mtoto au huonagi hilo la mtoto kugombolewa na familia ya kiumeni!!
 
Back
Top Bottom