Mwanaume akikataa mimba au kukutelekezea mtoto, usitumie majina yake Kwa mtoto wako

Mimi sioni shida mtoto akipewa majina kulingana na atakayemtunza na kumlea Kwa ruhusa ya mama au Baba
Wanafanya Hivyo bila Process Yoyote? namaanisha ni Automatic tu? Sijui utaratibu wake ulivyo hivyo ndio maana nikasema kwamba wanaofahamu watatujuza.

Ila all in all, hiyo haiondoi blood father bado atabaki; Mi nadhani ukiamua kufanya hivyo ni bora ukatae na genes zake kabisa; Kukataa Majina tu huku ili hali umebeba genes za baba naona haina maana yoyote.
 
Jina ni utambulisho
Jina ni umiliki MKUU.

Jina linaweza kubadilika kama vile umiliki unavyoweza kubadilika.

Baba yako anaweza kuwa anaitwa ISSA wewe unaitwa Meshack. Ukaitwa Meshack ISSA
Lakini Baba akabadili jina kutokana na sababu mbalimbali labda kubadili dini akawa Mkristo, akaitwa Peter.
Hivyo wewe utaitwa Meshack Peter sivyo?
Hiyo ni mfano wa utambulisho kwamba jina lomebadilika kumtambulisha Baba yako kwa kuitwa majina ya kikristo baada ya kubadili Dini.

Mfano wa pili.
Jina ni UMILIKI.

Salome Daudi Nziku ndilo jina la Mchumba wako.
Wewe jina lako ni Meshack Warioba

Baada ya kufunga ndoa na Salome.
Salome ataitwa Salome Meshack Warioba hii ni Kwa sababu wewe ndiye mmiliki wa Salome Kwa muda huo. Wewe ndiye utakayemtunza na kumhudumia Kwa lolote lile katika muda wote mtakaokuwa ndani ya ndoa.

Hivyo Mkeo ataitwa Mama Warioba wakati angetakiwa aitwe Mama nziku Kwa kufuata majina ya alipotoka(ukoo wake)

Kubadilisha jina haimaanishi damu au vinasaba vinabadilika.
 
Inategemea na aina ya mwanaume; kwa mwenye mafanikio, hata asipomjali mtoto, mwanamke atalazimisha mtoto wake atumie jina la baba.
 
Sijasoma hadi mwisho, lakini naunga mkono hoja kwa asilimia 100%.
 
Nakuelewa King, Ila nataka kwanza turudi nyuma Tufahamu kazi ya Jina ni nini??? hii ndo itajibu masawali mengi; Na kazi ya Jina kulingana na waanzilishi walivyoianzisha sio kama tunavyoitumia sisi..

Tatizo Vijana wa siku hizi tunayumba. Lazima watu wacheze kulingana na Mdundo
 
Unaweza kufanya hivyo kwa kumuandikisha surname nyingine. Then mbeleni baba yake akawa tajiri mkubwa then akafariki. Kwenye mirathi mtoto akakosa haki zake na kukulaumu mama yake kwa ulichofanya

Hizo case nimeshakutana nazo sana.

Watoto wengi wanawajua baba zao wakiwa wameshafariki hao ma baba. Ila misibani wanaenda na mirathi wanajumlishwa. Hasa wakiwa wanafanana na baba zao
Kwa hiyo kwako ubaba ni mirathi

thamani ya baba ni mali !!..
Kwa hiyo watu walio maskini ndio wanastahili hiyo adhabu kwa sababu hawana urithi wa kuwaachia watoto ??..

Kwa hiyo mtoto akang'ang'anie ubini sababu ya mirathi kana kwamba yeye hawezi kutengeneza ridhki yake mwenyewe..

Mimi baba yangu pamoja na madhaifu yake YOTE lakini kuna zile moments ambazo alijitolea sehemu ya maisha yake kwa ajili yangu. Kunilinda, kunilisha, kunivisha, kunisomesha, kunifurahisha, kuniimarisha, kunifunza, kunionesha dira na kunitengenezea msingi wa mimi kuwa mimi.
KWANGU INATOSHA

Hata leo akisema aninyime mirathi nitaumia si kwa sababu ya kukosa mali ila kujua kuwa sikuwa priority katika maisha yake. Ila kama atagawa mirathi yake katika charities sitomchukia na nitamuombea kheri
 
Kwema Wakuu!

Lazima tutende haki, lazima tuseme ukweli.
Wanawake wanamakosa Yao Kama tulivyo Sisi wanaume tunamakosa yetu.
Na mwenye makosa lazima aadhibiwe, na akiomba Msamaha sharti asamehewa lakini adhabu inaweza kubaki palepale.

Taikon huwaga ni mtu wa kuongea mambo magumu yasiyo rahisi, bila kujali yanamgusa Nani, iwe ni Mimi au wewe au Yule. Lengo ni kuweka mambo Sawa Kwa Haki. Ingawaje nafahamu Haki haitawezekana Kwa Asilimia 💯.

Najua wapo wanawake walifanya makosa Kwa kujibebesha mimba kimakusudi Kwa wanaume Kwa malengo Fulani, mathalani
1. Kwa lengo la kuolewa
2. Kwa lengo la Mali
3. Kwa lengo kupendwa

Hata hivyo zipo mimba zilizoingia Kwa bahati mbaya(bila kupanga baina ya mwanaume na Mwanamke).

Makosa ni makosa tuu. Lakini haimaanishi watu waendelee kujilaumu Kwa makosa waliyoyafanya. Lazima maisha yaendelee.

Amekataa mimba!
Amekubali mimba lakini kakataa kumlea mtoto.
Amekubali lakini ameshindwa Kumlea mtoto.

Ikiwa Baba mzazi amekataa au kushindwa kumlea mtoto Kwa sababu yoyote Ile isipokuwa sababu ya kifo au Maradhi basi nakushauri Usimpe mtoto Ubin wa huyo Baba Mzazi.

Amua kumpa jina lolote lile utakalolipenda, aidha ni jina la Wajomba zake wanaokusaidia kumlea, au jina la Baba yako(Babu yake upande wa Mama).

Wala sio dhambi.
Wala hakuna shida yoyote.
Kila mmoja awajibike Kwa makosa yake.

Wakati wewe ukiitwa single Mother, ukitukanwa na kuonekana Malaya, au mwanamke usiyefaa, iwe ni kweli au sio kweli, iwe ni Kwa bahati mbaya au makusudi lakini akakataa na ukazalilishwa na kuyapitia machungu.

Ukamenyeka kumlea mtoto Kwa halali na haramu wakati Baba yake anayetakiwa kutoa matumizi yupo anarandaranda huko, hata Kama Hakuwa na chakutoa lakini hata salamu na kukutia moyo alishindwa, ninachoweza kukushauri ni kubadilisha tuu Ubin WA mtoto.

Hakuna atakayekuuliza,
Na hautaonekana mbaya popote pale.

Hoja ya Msingi hapa ni kuwa, atakayemlea mtoto ndiye mwenye mamlaka naye.
Yeye ndiye ataamua aitwe Nani, ataamua jina la pili na latatu liwe la Nani.

Maana Vijana wa siku hizi tumezidi sasa.

Iwe ni Mimi Taikon au Nani, Kama umezaa na Mimi alafu nikaleta uhuni wa kukataa mimba au kushindwa kuhudumia mtoto, usitumie jina langu. Sistahili.
Na mtoto huyo hastahili kutumia jina langu.

Wanawake msiwafundishe watoto wenu kuwachukia Baba zao, nyie waleeni Kwa maadili ya kimila na Kidini, tumieni majina mtakayopenda ninyi, watoto wanavyokua wanajionea na kujua ni zipi sababu za nyie mama zao kufanya mlio ya fanya.

Lakini jitahidini kuwa wema ili watoto wasijeona kuwa ninyi ndio Wabaya.

Wito Kwa Vijana; msikimbie mimba wala msikimbie Kulea watoto.
Hata Kama huna chochote kitu, angalau mjulie hali mtoto au mzazi mwenza. Mtie moyo, kubali kubeba lawama Kwa maana wanawake ni watu wa lawama hata ungemuoa, lakini wakitulia na kutafakari wenyewe wanaelewa.

Mwanamke ukiwa mwema kwake hata Kama huna kitu anajua, anajali ingawaje atakutolea maneno ya shombo. Lakini haiondoi ukweli kuwa nao wanajisikia vibaya unavyoteseka.

Lakini Kulea mtoto hulei,
Kusalimia husalimii wala kumjulia Hali,
Mwanamke akiwa mkali kwako nawe unajifanya kiburi na jeuri Kwa maneno ya kashfa.
Unafikiri hata ungekuwa wewe ungefanyaje?

Hapo ndipo wanaume tunapokosea.
Saikolojia ya Wanawake ni kuendeshwa na mihemko, kulia upesi na kutoa maneno ya shombo kwao ni ishu ya kawaida lakini haimaanishi hawajali wala haimaanishi hawana akili ya kushindwa kutuelewa.

Mwanamke anahitaji Upendo(kujaliwa, kutiwa moyo, kufarijiwa, kupewa maneno matamu na laini, kushauriwa,)
Ukiyaweza hayo mwanamke kama alikuwa na hisia na wewe hawezi kukuchukia hata Kama humlei mtoto wake. Kwani wanaelewa.

Kitu kingine, wanawake ndio viumbe pekee ambao wanaelewa watu wanaojali hisia zao.

Unaweza kumhudumia Mkeo kila kitu(materials) kamwe hawezi kumnyang'anya mtoto wa Baba mwingine aliyezaa naye akakupa wewe ikiwa Bwana huyo bado anamjali na kumpenda.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Waambie hao kina mama wawapoteze damu nyingine nyepesi.
Baadhi ya damu hazipotezwi mkuu!
Kumbuka mtoto hana kosa, je kwa nini atengamishwe na baba yake wa damu? Je unafahamu haki za watoto?
Wazee wakiwaita wajukuu wao, huyo mama atamleta mwenyewe hata kwa kuulizia njia.
Vijana wapewe malezi sahihi, kukamiana na kujenga chuki hakuna faida endelevu.
 
Taikon... Acha ukike kike mtoto wa kiume. Mwanaume unaongea kama mwanamke. Je! Ungekua wewe ndio umepewa mimba?
 
Kipato kupiga chenga siyo tatizo. Tatizo ni unapoamua kugeuka na kutupa jongoo na mti wako na maneno ya shombo juu. Unamwambia mwanamke hiyo mimba siitambui au siihitaji au nimekuzawadia. Huu ni uungwana? Kwanini usimjali hata katika hali ya kukosa matunzo. Ukawa naye jirani na kumfariji. Kidogo unachoweza kupata ukamgawia. Ukamthamini kama mwanamke badala ya kumwita malaya nk.

Ukifanyiwa hivi kwa binti yako utaelewa maumivu ya kulea mjukuu wakati babake anakula bata na wanawake wengine. Inauma!

Kama hujawa tayari kulea basi mlinde asibebe mimba. Ikibidi kataa ku ..... bila kinga.
Sawa. Kuna ambao wameishi Kama mke na mume (bila ndoa rasmi), mpaka wakapata mtoto. Mtoto akiwa na mwaka mmoja, binti akaanza Tabia zisizofaa mpaka akalazimisha kutengana/kuachana.

Jamaa akaona asilazimishe Mambo, akaondoka akaenda kupanga sehemu nyingine. Baada ya jamaa kuondoka, binti naye kaondoka Kwa kutoroka akahamia mahali pengine, akamblock jamaa na baada ya muda akabadili kabisa namba.

Kuna kituo ambapo mtoto hushinda (day care), hivyo ili jamaa amuone mtoto analazimika kwenda pale kituoni!

Katika mazingira ya namna hii, unaendelea kumtetea mtoto WA kike?!

Baada ya kuondoka, binti hataki kabisa Baba mtoto ajue wapi wanaishi! Na Kwa kuwa amemblock na baadaye kubadili namba, jamaa Hana namna anaweza kutoa matunzo. Mbaya Zaidi jamaa anaambiwa na watu baki kwamba mama mtoto analalamika kwamba Baba mtoto hakuna anachofanya Kwa mtoto!

Hii ni kesi ya pili (inayofanana), ambazo mabinti wamenfanya nilizothibitisha.

Unaachaje kumtia mtu risasi katika Hali Kama hii!

Utaweza kusema Baba ametelekeza mtoto?

NASISITIZA TENA, KAMA HUJAOA USIJARIBU KU-BET FURAHA YAKO, au AMANI YAKO.
 
Kwema Wakuu!

Lazima tutende haki, lazima tuseme ukweli.
Wanawake wanamakosa Yao Kama tulivyo Sisi wanaume tunamakosa yetu.
Na mwenye makosa lazima aadhibiwe, na akiomba Msamaha sharti asamehewa lakini adhabu inaweza kubaki palepale.

Taikon huwaga ni mtu wa kuongea mambo magumu yasiyo rahisi, bila kujali yanamgusa Nani, iwe ni Mimi au wewe au Yule. Lengo ni kuweka mambo Sawa Kwa Haki. Ingawaje nafahamu Haki haitawezekana Kwa Asilimia .

Najua wapo wanawake walifanya makosa Kwa kujibebesha mimba kimakusudi Kwa wanaume Kwa malengo Fulani, mathalani
1. Kwa lengo la kuolewa
2. Kwa lengo la Mali
3. Kwa lengo kupendwa

Hata hivyo zipo mimba zilizoingia Kwa bahati mbaya(bila kupanga baina ya mwanaume na Mwanamke).

Makosa ni makosa tuu. Lakini haimaanishi watu waendelee kujilaumu Kwa makosa waliyoyafanya. Lazima maisha yaendelee.

Amekataa mimba!
Amekubali mimba lakini kakataa kumlea mtoto.
Amekubali lakini ameshindwa Kumlea mtoto.

Ikiwa Baba mzazi amekataa au kushindwa kumlea mtoto Kwa sababu yoyote Ile isipokuwa sababu ya kifo au Maradhi basi nakushauri Usimpe mtoto Ubin wa huyo Baba Mzazi.

Amua kumpa jina lolote lile utakalolipenda, aidha ni jina la Wajomba zake wanaokusaidia kumlea, au jina la Baba yako(Babu yake upande wa Mama).

Wala sio dhambi.
Wala hakuna shida yoyote.
Kila mmoja awajibike Kwa makosa yake.

Wakati wewe ukiitwa single Mother, ukitukanwa na kuonekana Malaya, au mwanamke usiyefaa, iwe ni kweli au sio kweli, iwe ni Kwa bahati mbaya au makusudi lakini akakataa na ukazalilishwa na kuyapitia machungu.

Ukamenyeka kumlea mtoto Kwa halali na haramu wakati Baba yake anayetakiwa kutoa matumizi yupo anarandaranda huko, hata Kama Hakuwa na chakutoa lakini hata salamu na kukutia moyo alishindwa, ninachoweza kukushauri ni kubadilisha tuu Ubin WA mtoto.

Hakuna atakayekuuliza,
Na hautaonekana mbaya popote pale.

Hoja ya Msingi hapa ni kuwa, atakayemlea mtoto ndiye mwenye mamlaka naye.
Yeye ndiye ataamua aitwe Nani, ataamua jina la pili na latatu liwe la Nani.

Maana Vijana wa siku hizi tumezidi sasa.

Iwe ni Mimi Taikon au Nani, Kama umezaa na Mimi alafu nikaleta uhuni wa kukataa mimba au kushindwa kuhudumia mtoto, usitumie jina langu. Sistahili.
Na mtoto huyo hastahili kutumia jina langu.

Wanawake msiwafundishe watoto wenu kuwachukia Baba zao, nyie waleeni Kwa maadili ya kimila na Kidini, tumieni majina mtakayopenda ninyi, watoto wanavyokua wanajionea na kujua ni zipi sababu za nyie mama zao kufanya mlio ya fanya.

Lakini jitahidini kuwa wema ili watoto wasijeona kuwa ninyi ndio Wabaya.

Wito Kwa Vijana; msikimbie mimba wala msikimbie Kulea watoto.
Hata Kama huna chochote kitu, angalau mjulie hali mtoto au mzazi mwenza. Mtie moyo, kubali kubeba lawama Kwa maana wanawake ni watu wa lawama hata ungemuoa, lakini wakitulia na kutafakari wenyewe wanaelewa.

Mwanamke ukiwa mwema kwake hata Kama huna kitu anajua, anajali ingawaje atakutolea maneno ya shombo. Lakini haiondoi ukweli kuwa nao wanajisikia vibaya unavyoteseka.

Lakini Kulea mtoto hulei,
Kusalimia husalimii wala kumjulia Hali,
Mwanamke akiwa mkali kwako nawe unajifanya kiburi na jeuri Kwa maneno ya kashfa.
Unafikiri hata ungekuwa wewe ungefanyaje?

Hapo ndipo wanaume tunapokosea.
Saikolojia ya Wanawake ni kuendeshwa na mihemko, kulia upesi na kutoa maneno ya shombo kwao ni ishu ya kawaida lakini haimaanishi hawajali wala haimaanishi hawana akili ya kushindwa kutuelewa.

Mwanamke anahitaji Upendo(kujaliwa, kutiwa moyo, kufarijiwa, kupewa maneno matamu na laini, kushauriwa,)
Ukiyaweza hayo mwanamke kama alikuwa na hisia na wewe hawezi kukuchukia hata Kama humlei mtoto wake. Kwani wanaelewa.

Kitu kingine, wanawake ndio viumbe pekee ambao wanaelewa watu wanaojali hisia zao.

Unaweza kumhudumia Mkeo kila kitu(materials) kamwe hawezi kumnyang'anya mtoto wa Baba mwingine aliyezaa naye akakupa wewe ikiwa Bwana huyo bado anamjali na kumpenda.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Kuna ambao wameishi Kama mke na mume (bila ndoa rasmi), mpaka wakapata mtoto. Mtoto akiwa na mwaka mmoja, binti akaanza Tabia zisizofaa mpaka akalazimisha kutengana/kuachana.

Jamaa akaona asilazimishe Mambo, akaondoka akaenda kupanga sehemu nyingine. Baada ya jamaa kuondoka, binti naye kaondoka Kwa kutoroka akahamia mahali pengine, akamblock jamaa na baada ya muda akabadili kabisa namba.

Kuna kituo ambapo mtoto hushinda (day care), hivyo ili jamaa amuone mtoto analazimika kwenda pale kituoni!

Katika mazingira ya namna hii, unaendelea kumtetea mtoto WA kike?!

Baada ya kuondoka, binti hataki kabisa Baba mtoto ajue wapi wanaishi! Na Kwa kuwa amemblock na baadaye kubadili namba, jamaa Hana namna anaweza kutoa matunzo. Mbaya Zaidi jamaa anaambiwa na watu baki kwamba mama mtoto analalamika kwamba Baba mtoto hakuna anachofanya Kwa mtoto!

Hii ni kesi ya pili (inayofanana), ambazo mabinti wamenfanya nilizothibitisha.

Unaachaje kumtia mtu risasi katika Hali Kama hii!

Utaweza kusema Baba ametelekeza mtoto?

NASISITIZA TENA, KAMA HUJAOA USIJARIBU KU-BET FURAHA YAKO, au AMANI YAKO, usijaribu kujipa presha na hawa wanawake ambao nusu ni binadamu, nusu shetani. Mwanamke ambaye ameolewa au anaishi na mtu wake lakini anatongozwa, anakubali na anakwenda kupanua miguu huku akifahamu kwamba ameolewa!
 
Kubadilisha Jina la Ukoo la mtoto hakubadilishi ukweli kuwa mtoto ni wa mwanaume aliemwaga baoo...!! Kuja mtoto wa mjomba wangu baada ya mjomba kufariki aliletwa kafanan sana na watoto wengine lakini anatumia jina la Ukoo mwingine hiyo sio sababu hata kidogo ya kumkataaa yule mtoto so ukoo ulimkubali vizuri tuu.

Case nyingine me mzee anaa mtoto wa nje ila hatumii jina la mzee ila namini ipo siku atakuja kudai chake pale na ataletwa tu hata na wazeee.
 
Kuna ambao wameishi Kama mke na mume (bila ndoa rasmi), mpaka wakapata mtoto. Mtoto akiwa na mwaka mmoja, binti akaanza Tabia zisizofaa mpaka akalazimisha kutengana/kuachana.

Jamaa akaona asilazimishe Mambo, akaondoka akaenda kupanga sehemu nyingine. Baada ya jamaa kuondoka, binti naye kaondoka Kwa kutoroka akahamia mahali pengine, akamblock jamaa na baada ya muda akabadili kabisa namba.

Kuna kituo ambapo mtoto hushinda (day care), hivyo ili jamaa amuone mtoto analazimika kwenda pale kituoni!

Katika mazingira ya namna hii, unaendelea kumtetea mtoto WA kike?!

Baada ya kuondoka, binti hataki kabisa Baba mtoto ajue wapi wanaishi! Na Kwa kuwa amemblock na baadaye kubadili namba, jamaa Hana namna anaweza kutoa matunzo. Mbaya Zaidi jamaa anaambiwa na watu baki kwamba mama mtoto analalamika kwamba Baba mtoto hakuna anachofanya Kwa mtoto!

Hii ni kesi ya pili (inayofanana), ambazo mabinti wamenfanya nilizothibitisha.

Unaachaje kumtia mtu risasi katika Hali Kama hii!

Utaweza kusema Baba ametelekeza mtoto?

NASISITIZA TENA, KAMA HUJAOA USIJARIBU KU-BET FURAHA YAKO, au AMANI YAKO

Mpaka anakuambia hivyo ni kwamba umeshindwa kuwa Mwanaume.

Unacheka CHEKA tuu!

Kuna namna tatu za kuwa Mwanaume.
1. Kutumia Akili
2. Kutumia nguvu
3. Kutumia Akili na nguvu.

Kama Kwa mwanamke hajawahi kuona moja Kati ya hivyo kutoka kwako anakuchukulia Kama jike lenzake.

Hakuna mwanamke mwenye uwezo wa kumtingisha mwanaume aliyekamilika.

Ati unapigwa marufuku😀😀😀 huyo wakukupiga marufuku kakudharau,

Jifunze kutenda Kama Mwanaume. Mwanamke Hana ubavu wa kuongea upuuzi wa hivyo Kama hajakudharau, na anajua hutamfanya lolote.
 
Kubadilisha Jina la Ukoo la mtoto hakubadilishi ukweli kuwa mtoto ni wa mwanaume aliemwaga baoo...!! Kuja mtoto wa mjomba wangu baada ya mjomba kufariki aliletwa kafanan sana na watoto wengine lakini anatumia jina la Ukoo mwingine hiyo sio sababu hata kidogo ya kumkataaa yule mtoto so ukoo ulimkubali vizuri tuu.

Case nyingine me mzee anaa mtoto wa nje ila hatumii jina la mzee ila namini ipo siku atakuja kudai chake pale na ataletwa tu hata na wazeee.

Umesema ukweli jina halibadili asili Ila linabadili umiliki
 
Back
Top Bottom