Mwanataaluma Bi. Mwanahamisi Singano kuongoza Timu ya Ilani ya Uchaguzi ya ACT Wazalendo 2020

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Ndugu Wananchi

‪Katika kuhakikisha kuwa Chama chetu cha ACT Wazalendo kinakuwa na Ilani ya Uchaguzi yenye majawabu ya changamoto za nchi yetu, nimeunda timu yenye wanachama wa ACT Wazalendo na Wataalamu (Professionals) ili kuchambua maoni ya Wananchi yaliyokusanywa nchi nzima wakati wa “Listening Tour” na kuandaa Rasimu ya Ilani ya mwaka 2020 .

‪Timu hii ya Ilani ya ACT Wazalendo kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 itaongozwa na mwanataaluma ndugu Mwanahamisi Singano na Sekretariat yake itakuwa chini ya ndugu Idrisa Kweweta ambaye ni Katibu wetu wa Sera, Utafiti na Mafunzo. Wajumbe ni timu hii ni wafuatao

1. Emmanuel Lazarius Mvula - Wakili na Mtaalam wa Haki za Kijamii
3. Dkt. Elizabeth Benedict - Mtaalam Sekta ya Afya
4. Godluck Mushi - Mtaalam Sekta ya Fedha
5. Ismail Jussa Ladhu - Mjumbe wa Kamati Kuu
6. Abdul Omary Nondo - Mwenyekiti, Ngome ya Vijana ACT Wazalendo
7. Dkt Janeth Fussi - Katibu, Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo‬
8. Mwanaisha Mndeme - Katibu, Ngome ya Vijana ACT Wazalendo
9. Edgar Mkosamali - Katibu, Idara ya Bunge na Baraza la Wawakilishi ACT Wazalendo

Rasimu hii ya Ilani itakayoandaliwa (pamoja na ile ya Zanzibar) zitafikishwa kwenye Sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama ili kuidhinishwa. Naitakia timu hii kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yao haya.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Mei 23, 2020

DA735179-8AD8-4545-B036-5921CA63A480.jpeg
 
Ilani iwe na preamble yenye kauli mbiu ifuatayo

"Watanzania leo tunatawaliwa kidikteta, Sababu za kuondoa udikteta tunazo, nia ya kuuondoa tunayo, na uwezo wa kuuondoa tunayo na hiyo kazi tutaifanya"

Mkiweka hayo maneno kwenye Ilani, kura yangu mmeshaipata
 
Nimeona sehemu umeandika" nimeunda timu...." Kwa maana hiyo tume itafanya kazi zako na si za chama. Huu mtego watanzania tuuepuke utawala wa kiimla unanukia
 
Ilani iwe na preamble yenye kauli mbiu ifuatayo

"Watanzania leo tunatawaliwa kidikteta, Sababu za kuondoa udikteta tunazo, nia ya kuuondoa tunayo, na uwezo wa kuuondoa tunayo na hiyo kazi tutaifanya"

Mkiweka hayo maneno kwenye Ilani, kura yangu mmeshaipata
Nionyeshe kiparata cha kura 😂😂😂! Ukinionyesha tunaweka
 
Nilitegemea Mwenyekiti wa ACT au Katibu Mkuu wa ACT ndio wangehusika na uundwaji wa hiyo Kamati ya Ilani ya Uchaguzi 2020.

Sasa Ndugu yangu Zitto napata ukakasi kidogo na namna ACT wanavyotenda kazi zao.

Mwisho pamoja na yote lakini nitoe pongezi zangu za dhati kwani huu ni mwanzo mzuri.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mkuu Zitto tatizo la ACT kama vilivyo vyama vingine vingi sio "documents" bali tabia. Nadhani ACT ina documents nzuri tu ukizisoma, tatizo ni "ceremonial". Hakuna anayezifuata wala kuonesha hadharani kuziamini.

Iko wapi misingi 10? Iliyoasisi ACT?

Uko wapi uwazi? Kama jina la chama na chama chenyewe kilivyoanza kwa kujidhihirisha mwaka 2014?


Kuwa na document, ni jambo moja lakini kama matendo hamna ni sawa na msomi asiyejua kasoma nini au namna ya kuunganisha alichosoma na maisha ya kawaida.

Halafu pia mbona mmechelewa sana kuanza hilo zoezi? Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri, CCM walianza kuandaa ilani 2018 mwishoni au 2019 mwanzoni na walikuwa wanakusanya maoni. Anyway, nibora kuchelewa lakini kufanya. Kwa hiyo tunawatakia kila la heri.
 
Nilitegemea Mwenyekiti wa ACT au Katibu Mkuu wa ACT ndio wangehusika na uundwaji wa hiyo Kamati ya Ilani ya Uchaguzi 2020.

Sasa Ndugu yangu Zitto napata ukakasi kidogo na namna ACT wanavyotenda kazi zao.

Mwisho pamoja na yote lakini nitoe pongezi zangu za dhati kwani huu ni mwanzo mzuri.
Nilishamshauri juu ya jambo hili hili hapa hapa, akasema wao hawana itifaki, yoyote anafanya chochote.
 
Back
Top Bottom