Mwanataaluma Bi. Mwanahamisi Singano kuongoza Timu ya Ilani ya Uchaguzi ya ACT Wazalendo 2020

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,649
2,000
Mgombea huteuliwa na vyama, kinachofanyika sasa ni kutangaza tuu nia. Mimi pia natangaza nia, wapi subiria kipenga kipulizwe.
P
İs it perfect time to you for Tanzanians
Or
Perfect time to you for u

Kwangu nakuomba subiri ukifika hata mm nitakuunga mkono

Hata ukililazimisha utakwenda kuwa amongst fools

Tusibir tujenge nyumba tukiwa nje kwanza kwani hatuna presha
Usiwaze umri
 

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,649
2,000
Zito maisha ya watz hayaitaji ilani yanataka uongozi tu kwani hayo ya ilani ni kujiliwaza ninyi na wasomi wachache

Watz tunataka uongozi wenye kuderiver rule of law na good governance>>>>> sheria zetu nyingi ni mbovu pia mfumo wa kutoa haki, kuunda sheria bado ni mbovu hata mfumo wa nchi bado hautupi rule of law and good governance.
Hatutaki hospitali wala shule nyingi au ubora leo nawakati mkiondoka tunarudi square zero.
Hatutaki maendeleo kama hisan ya vyama bali matokeo ya sheria na utawala bora.

Kutaka uongozi imara wa nchi unatosha kudrive the wheel of your kampeni.
Lakini shida mnataka madaraka kwa kutupumbaza na maneno yasiyotekelezeka.
İlani inayoweza kutekelezwa hata mkiwa nje ya madaraka kwa kuisimamia kweli.

Pole zitto bado hata kamati yako haijui fikra za wachache zinazoishi leo na kesho na kesho kutwa.
Najua utaparamia ya wengi yenye mvuto wa leo na hasira ya kesho
Pole.
Karibu kwenye fikra za wachache zisizosikilizwa na wengi.
 

aloycious

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
5,594
2,000
Watu wanajifungia wanapika "manifesto".Komaeni mpate asilimia za kupata ruzuku kiishe. Acheni kuhadaa watu.
 

naliwe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
475
1,000
Ndugu Wananchi

‪Katika kuhakikisha kuwa Chama chetu cha ACT Wazalendo kinakuwa na Ilani ya Uchaguzi yenye majawabu ya changamoto za nchi yetu, nimeunda timu yenye wanachama wa ACT Wazalendo na Wataalamu (Professionals) ili kuchambua maoni ya Wananchi yaliyokusanywa nchi nzima wakati wa “Listening Tour” na kuandaa Rasimu ya Ilani ya mwaka 2020 .

‪Timu hii ya Ilani ya ACT Wazalendo kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 itaongozwa na mwanataaluma ndugu Mwanahamisi Singano na Sekretariat yake itakuwa chini ya ndugu Idrisa Kweweta ambaye ni Katibu wetu wa Sera, Utafiti na Mafunzo. Wajumbe ni timu hii ni wafuatao

1. Emmanuel Lazarius Mvula - Wakili na Mtaalam wa Haki za Kijamii
3. Dkt. Elizabeth Benedict - Mtaalam Sekta ya Afya
4. Godluck Mushi - Mtaalam Sekta ya Fedha
5. Ismail Jussa Ladhu - Mjumbe wa Kamati Kuu
6. Abdul Omary Nondo - Mwenyekiti, Ngome ya Vijana ACT Wazalendo
7. Dkt Janeth Fussi - Katibu, Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo‬
8. Mwanaisha Mndeme - Katibu, Ngome ya Vijana ACT Wazalendo
9. Edgar Mkosamali - Katibu, Idara ya Bunge na Baraza la Wawakilishi ACT Wazalendo

Rasimu hii ya Ilani itakayoandaliwa (pamoja na ile ya Zanzibar) zitafikishwa kwenye Sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama ili kuidhinishwa. Naitakia timu hii kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yao haya.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Mei 23, 2020

View attachment 1457298
Uyo nondo ungemtoa hapo mkuu,alafu nikushauri tuu uyo kijana mwangalie Kwa makini siku moja atakuvua nguo,si kijana wa kuaminika sana,siku zote ogopa vijana ambao wanatafuta umaarufu Kwa njia youote Ile kama uyo nondo,nakupa tuu taadhari

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
10,933
2,000
Cha kushauri hapo muwe conscious na time...umeintroduce jopo lako umepata feedback nzuri,now mfanye mipango yenu ijulikane msiweke pending..ni wakati wa kushauriana mfanye nini with this short time..una team nzuri i'm sure mtashauriana vizuri.
 

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
5,908
2,000
Ndugu Zitto, tunawashukuru sana, na inafurahisha sana kuona maendeleo yenu yanakwenda very well. Hata sie ambao tuko upande mwengine tumeanza kuwasikilisa na kuwafuatilia, mnazungumza lugha inayoeleweka.

Juzi ama Jana katika mazungumzo na marafikibwa karibu ambao tuko vyama tofauti, lakini wengi wetu are quite happy na mwenendo wa ACT, kidogo tuliona lugha iliyotushinda akili, kwenye tweeter ya Ndugu JUSSA, hii kuna tulio itafsiri kama wanatofautisha aim ya ACT ya kutafuta election victory utakuwa mbili tofauti kati visiwani na Bara.

" "Uchaguzi wa 2020 #Zanzibar ni fainali. Tumejipanga kushinda Zanzibar na kupigania ushindi wetu. Kama alivyosema Mwenyekiti wetu, Maalim @SeifSharifHamad, CCM wasitarajie kuwa tutawazuia Wazanzibari wasipambanie ushindi wao." @AdoShaibu #ACTWazalendo #GumzoLaNipashe Ismail Jussa on Twitter"

Nadhani mnajua kuwa kuna tuhuma baadhi ya vyama, CCM na vinginevyo, wanajaribu ku spine kilakitu mkifanyacho kuhakikisha wanawatia wananchi taharuki ya kuwa ACT ni chama cha kidini, thus you have no choice but to refrain and be cautious to what can be translated differently.

Ukweli ni kuwa ACT watapigania na kulunda ushindi wao Tanzania nzima, kwanini kutofautisha majimbo?

Mtanisamehe kama tumeelwa vibaya, nia yangu ni kuona kuna upinzani imara na mzuri, pia ninafurahishwa na mwenendo wa ACT, in certain leadership positions, I choose the person and not the party.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
98,608
2,000
Ni wazo zuri sana hawa wawili kutokana na experience yao kubwa katika uwanja wa siasa Nchini wa miaka mingi wanastahili kabisa kuwemo kwenye hii kamati.

Nilitegemea Mwenyekiti wa ACT au Katibu Mkuu wa ACT ndio wangehusika na uundwaji wa hiyo Kamati ya Ilani ya Uchaguzi 2020.

Sasa Ndugu yangu Zitto napata ukakasi kidogo na namna ACT wanavyotenda kazi zao.

Mwisho pamoja na yote lakini nitoe pongezi zangu za dhati kwani huu ni mwanzo mzuri.
 
Top Bottom