Mwanasiasa wa Nigeria Akamatwa na kilo 2 za Cocaine Tumboni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,041
4495134.jpg

Eme Zuru Ayortor Tuesday, May 18, 2010 10:13 PM
Mwanasiasa wa Nigeria ametiwa mbaroni nchini humo baada ya kunaswa uwanja wa ndege akiwa amemeza kilo mbili za madawa ya kulevya aina ya cocaine. Polisi nchini Nigeria walisema kuwa mwanasiasa huyo aliyegombea ubunge wakati wa uchaguzi uliopita na ambaye pia anagombea ubunge katika uchaguzi ujao, alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Lagos akiwa amemeza kilo mbili za madawa ya kulevya aina ya cocaine akijaribu kuzisafirisha kuzipeleka Ujerumani.

Mwanasiasa huyo aliyetajwa jina lake kuwa ni Eme Zuru Ayortor aliwaambia maafisa wa polisi kuwa alimeza madawa hayo ya kulevya ili aweze kupata pesa za kupigia kampeni wakati wa uchaguzi.

Polisi walisema kuwa scanners za uwanja wa ndege zilionyesha kete za madawa ya kulevya zikiwa tumboni mwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 52.

Polisi walisema kuwa walifanikiwa kuzipata kete 100 za cocaine toka kwenye tumbo lake.

Taarifa zilisema kuwa Ayortor aliwaambia polisi kuwa alihitaji pesa kwakuwa alipoteza pesa nyingi sana wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita wa mwaka 2007.

"Kiasi cha madawa ya kulevya alichokibeba tumboni ni kikubwa sana", alisema afisa wa polisi na kuongeza "Tunaamini hii sio mara yake ya kwanza kusafirisha madawa ya kulevya".

Kitaaluma Ayortor, ana shahada ya pharmacy aliyoipata kwenye chuo kikuu cha Wisconsin nchini Marekani.
NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Huenda na Tanzania tunao wanasiasa wa aina hii, anyongwe tu huyu.
 
Wanigeria ni kama wamepata laana!Ukienda jela zote za EU,lazima utapata Mnigeria convicted of drug offences.
Hata mwaka mmoja niliangalia documuntary ya Gereza mashuhuri huko Thailand,wanigeria walikuwapo.Hata India!!!!
 
Huku kwetu si wanapewa diplomacy passports - yaani hata katibu wa deep green airpot anapita VIP side ndipo wanapopitisha vitu vyao
 
Kuna mwaka mmoja nasikia Balozi(WAZIRI) wetu huko nje sasa marehemu,walimshutukia kuwa alikuwa anabeba unga.It was shameful act!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom