Imalamawazo
JF-Expert Member
- Jul 27, 2021
- 1,342
- 3,234
Hawa miamba wawili waliotikisa siasa za Tanzania na Zanzibar kwa miaka ya hivi karibuni. Ulinganisho wao unatokana na ukweli kuwa wote walikuwa viongozi wa juu wa kisiasa na pia muda wao wa kiaga dunia ulikaribiana sana.
Kila mmoja kati ya viongozi hawa walikuwa na misimamo, falsafa na mitazamo iliyowajengea umaarufu mkubwa. Sasa baada ya miezi kadhaa bila uwepo wao tutaweza kutathimini ni nani aliyweza kujijengea wafuasi kwa wingi na wapambe wachache na yupi alijijengea wapambane kwa wingi na wafuasi kwa uchache? Je, ni mbinu zipi kiongozi wa kisiasa anaweza kuzitumia kupata wafuasi wengi badala ya wapambe wengi?
NB: Kwa ajili ya hii post neno wafuasi litamaanisha watu waliojifunza mitazamo na falsafa za kiongozi na kuziishi, lakini wapambe ni watu wanaosifia na kumpamba kiongozi bila kuwa na imani thabiti ya mitazamo na falsafa zake.