Mwanasiasa Msafi anafanya nini ndani ya CHAMA KICHAFU- Dr. Azaveli Feza Lwaitama

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Ndugu wanJF, Juzi juzi nimemsikia mchambuzi maarufu Dr. Lwaitama akihojiwa kupitia Sibuka TV, pamoja na nondo nyingi alizotoa, nimefurahishwa na hoja ya kama mtu ni msafi anafanya nini ndani ya chama kichafu, chama ambacho kimetuletea umaskini wa kutupwa, mwanasiasa msafi iweje agombee kupitia chama ambacho kinanuka, na wananchi hawakitaki?

Mtaaluma huyo alienda mbali na kuiasa jamii iwapige chini wale ambao wanajipapambua kuwa ni wasafi huku wanashikiria mikoba ya chama kichafu. Hapa ndio hatari sana, maana mtu msafi atakaa vipi chama kichafu, alihoji mtadi huyo.

Ktk mambo mengi hili suala lilinigusa sana, hivi kweli iweje mtu msafi akae chama kichafu, hapa ndo nikawakumbuka kina magufuli, mwakyembe, sitta, kilango, filikunjombe, maige, shelukindo beatrice, january makamba na wengine wa aina hiyo.

Kama kweli hawa watu ni wasafi na bado wako chama kichafu, basi kunashida kubwa (wako mentally dehydrated) na ni ukweli kuwa wao ndo hatari sana kwa jamii ya kitanzania. Kwa uelewa wa sitta au makufuli au mwakyembe bado wanafanya nini huko kama kweli wao niwasafi??? why not to form a winning team na wasafi wenzao? Shida ipo hapo, Watanzania tuwakatae kama wasaliti ktk jamii.Usaliti zamani au kwa wenzetu walioendelea ni kosa kubwa sana, mtu mwenye akili timamu asingependa alifanye.

Kauli ya Lwaitama ilinikumbusha usemi wa mwanafalsafa mmoja unahusu unafiki katika jamii, it is not the bad people to blame, it is the good ones who opt willingly to remain silence while the bad people act against humankind.

TUWAPIGE VITA WATU HAWA MCHANA, USIKU, POPOTE NA DAIMA.
 
Tena hawa ndo tuwafanye wa kwanza kuwadosha kwa kosa la unafki na maigizo wanayoyaleta kwa kudanganya kuwa ni wasafi while they are in the same bottle.
Dr Lwaitama ni moja kati ya vichwa vichache vilivyojaa knowledge hapa tanzania.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Pamoja na misemo isemayo: (1) Samaki mmoja akioza, wote wameoza (2) adhaniaye amesimama na angalie asianguke (3) mwenzako akinyolewa nawe zako tia maji (4) Hakuna marefu yasina ncha n.k. Nadhani sio busara kuamini kuwa mapambano lazima yaendeshwe kutokea nja ya ccm, na wala sio kweli kuwa waliowachafu tu ndio wanaopaswa kubakia ndani ya CCM.

Ifahamike tu kuwa walioiasisi CCM hakuwa na mipango kuwa siku moja mambo yatakuwa hivi, ila ulevi huleta mambo yanayofanana na haya. Kuijenga Tanzania imara ni vyema bado wanaodhani kuwa ni wasafi kuendelea kupambana ndani ya CCM ili kuitakasa. Hii mwisho wa cku itatoa fursa sawa katika kuchangia maendeleo ya Tanzania. Hebu fikiri, leo CHADEMA wanachukua nchi mtataka wapinzani wao wawe watu wenye sifa zipi?

Ningependa kuiona ccm inayobadilika, inayokubaliana na haki za msingi za raia wa nchi hii, inayoondoa matabaka, inayojali fursa sawa (afya, elimu, demokrasia n.k) kwa watanzania wote.

Kubwa zaidi inayoamini na kutambua kuwa nchi hii inaweza kutawaliwa na Mtanzania yeyote mwenye sifa japo sio miongoni mwa CCM, na wakubali kujenga ngome imara ya kambi ya upinzani pindi watakapokuwa upande wa pili.
 
Demokrasia ni maendeleo, kwa maana kwamba demokrasia yoyote yenye faida kwa jamii ni lazima iwekewe mipaka fulani ambayo itailazimisha kuleta maendeleo. Kama chama tawala kinafanya vizuri sana, haki na ukweli, timiza wa wajibu baada ya mlipa kodi kufanya hivyo, hakika demokrasia ingelazimisha kuwe na chama kimoja, kwa maana ya kulinda na kuleta maendeleo.

Kwa hoja hiyo, ninachelea kuona mtu anaandika akifikiria nani atakuwa mpizani wakati CHADEMA iko madarakani, naona kama anafikiria upinzani zaidi kuliko maendeleo, anadhani demokrasia ni kuwepo na upinzani, sio sahihi mimi ningesema demokrasia ni kuwepo kwa haki, maendeleo na uwajibikaji hata kama chama ni kimoja, kuna wakati kwa dhana hii CCM ilikuwa chama pekee lakini kulikuwa na demokrasia nzuri sana.

Sioni namna unavyoweza kuhalalisha USALITI kwa dhana eti nani atakuwa mpinzani hapo baadae. NI AIBU kwa mtu msafi mwenye akili timamu kuwa sehemu ya CHAMA KICHAFU ambacho wananchi hawakitaki. Ni vigumu kuelewa mtu mwenye akili nzuri ila maneno yake tu ndo machafu, inawezekana?

Mtu mwenye tabia nzuri ila matendo yake tu ndo mabaya??? inawezekana hiyo? WAPIGANAJI WA KWELI LAZIMA WAJE MBELE, maana haiwezekani kubeba kiti ulichokalia, watoke chama kichafu harafu wafagie uchafu.
 
...Katika mambo mengi hili suala lilinigusa sana, hivi kweli iweje mtu msafi akae chama kichafu, hapa ndo nikawakumbuka kina magufuli, mwakyembe, sitta, kilango, filikunjombe, maige, shelukindo beatrice, january makamba na wengine wa aina hiyo...

Kwenye RED, Inamaana hao ni wasafi au? Tutakukatalia mpaka mwisho...
 
Wote niliowataja usafi wao ni wamashaka makubwa, sio Maige na January pekee. Ndo maana hoja ni mtu msafi anafanya nini chama kichafu?
 
Kama ndege wenye rangi moja huruka pamoja, je unaweza kuwa ktk chama la wezi angali wewe si mwizi wala huna hulka ya wizi??? mtajadili nini kila mnapokutana?? unachangia hoja gani kwenye vikao??
 
Inaeleweka kisayansi ya kwamba ukiwa ndani ya gari huwezi kulisukuma maana utakuwa unasukuma uzito wako mwenyewe!
Ndugu mwana CCM msafi ondoka mapema jiunge na wakombozi kama walivyofanya askari wa IDD AMIN majeshi ya ukombozi yalivyoanza kuinyatia Kampala mwaka 1979.
 
quote_icon.png
By fikirikwanza
...Katika mambo mengi hili suala lilinigusa sana, hivi kweli iweje mtu msafi akae chama kichafu, hapa ndo nikawakumbuka kina magufuli, mwakyembe, sitta, kilango, filikunjombe, maige, shelukindo beatrice, january makamba na wengine wa aina hiyo...

Kwenye RED, Inamaana hao ni wasafi au? Tutakukatalia mpaka mwisho...

Mkuu nakuunga mkono kwa hilo.. Wana usafi gani hao..? Tena hao ndo hatari kabisa kwa kuwa ni wanafiki wa hali ya juu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom