TANZIA Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Njelu Kasaka amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Mbeya alipokuwa akipatiwa matibabu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,580
217,962
Masache Kasaka amethibitisha kifo cha Baba Yake kwa kusema amefariki dunia kutokana na tatizo la moyo lililokuwa linamsumbua. “Wakati anaedelea na matibabu katika hospitali akapata mshituko wa moyo uliosababisha kufariki dunia,” . Msiba uko nyumbani kwake, Chunya mkoani Mbeya, “na mazishi yatakuwa Jumapili (tarehe 5 Julai,2020).”

Kasaka ambaye amepata kuwa mbunge, Waziri na mkuu wa mkoa, alijitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kugombea ubunge jimbo la Lupa.

Mwaka 2019, Kasaka alizindua kitabu chake alichokiita ‘Njelu Kasaka: Maisha, Siasa na Hoja ya Tanganyika-G55.”

Mzee Njelu Kasaka ameacha watoto saba na mjane mmoja.

Baada ya kusoma makala yake nikaisaka CV ya Njelu Kasaka

Njelu Kasaka: Hakuna aliye salama ndani na nje ya CCM

Njelu Kasaka ajiunga na CHADEMA

Wako wapi G55?

Njelu.jpg
 
Umri? Next time ulizia umri wa marehemu kwanza kabla ya kukimbilia kuhabarisha.

Apumzike kwa Amani!
 
Back
Top Bottom