Mwanasiasa Bunge la Ulaya ahoji uwezo wa Marekani kumkamata Maduro lakini kushindwa kumuwajibisha Netanyahu wa Israel

Mwanasiasa Bunge la Ulaya ahoji uwezo wa Marekani kumkamata Maduro lakini kushindwa kumuwajibisha Netanyahu wa Israel

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,931
Reaction score
2,961
Mwanasiasa wa Bunge la Ulaya amehoji uwezekano wa Marekani kumkamata Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro na kumfikisha katika Mahakama , lakini imeshindwa kumkamata na kumuwajibisha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anayesimamia vikosi vyake kuishambulia Palestine

Hapo ni sawa na kusema simba dume amwajibishe simba jike kwa kwenda kuvamia makazi ya swala!, kwanza palestine wapigwe tu kwann wawafuge magaidi.
 
Wakamkamate wao maana wako jirani naye
 
Wakamkamate wao maana wako jirani naye
kwamba wapeleke special force jerusalem na tel aviv wamdabe BENJAMIN DE NETANYAHU aaahaaha kwamba waingze ma helcopter kama chinook kule israel ksha wamkamate PM wa israel kwny ardhi ya israel? waende bs maana ni majiran sn watakachoktafuta watakpata.
 
Mwanasiasa wa Bunge la Ulaya amehoji uwezekano wa Marekani kumkamata Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro na kumfikisha katika Mahakama , lakini imeshindwa kumkamata na kumuwajibisha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anayesimamia vikosi vyake kuishambulia Palestine

Huyo "mpolitishian" ana kiseyeye sugu cha ubongo.
 
Hapo ni sawa na kusema simba dume amwajibishe simba jike kwa kwenda kuvamia makazi ya swala!, kwanza palestine wapigwe tu kwann wawafuge magaidi.
Na nyie acha mtandikwe kwa kumtusi Rais wa Nchi. Ikibidi muuliwe ni sawa kabisa.
 
Marekani siyo kwamba imeshindwa kumkamata Netanyahu bali haioni sabanu ya kufanya hivyo. Kwani Netanyahu amefanya kosa gani?

Jamii ya kimataifa ilikosea sana. Mara baada ya lile shambulio lila la kigaidi la Hamas, ilitakiwa jamii nzima, hasa nchi za kiarabu, zilaani na zitoe tamko la kushirikiana na Israel kuwaangamiza Hamasi. Hiyo ingetoa nafasi ya kujadili jinsi ya kuwalinda raia, na namna ya kuwakamata Ha.as wote. Lakini kitendo cha baadhi ya nchi za kiarabu na makundi ya kigaidi kuamua kushirikiana na Hamas, ile ilitoa nafasi kwa Israel kutumia nguvu zake zote bila ya kujali magaidi wamejificha katika ya raia au wamekimbilia hospitali au shuleni. Na bila ya hasara kubwa upande wa Hamas, wangekuwa bado wanaishambulia Israel. Kwa kile walichokifanya Hamas dhidi ya Israel, hakuna nchi itakayomkamata Netanyahu, labda kama Israel ingeanza kuwaua wapalestina bila ya lile shambulio la Hamas.
 
kwamba wapeleke special force jerusalem na tel aviv wamdabe BENJAMIN DE NETANYAHU aaahaaha kwamba waingze ma helcopter kama chinook kule israel ksha wamkamate PM wa israel kwny ardhi ya israel? waende bs maana ni majiran sn watakachoktafuta watakpata.
Mbona waliposema akikanyaga Mfano Norway atakamatwa sijawahi ona akienda Norway kweli? Sio kila mtu muoga kama wewe, Netanyahu anayo arrest warrant kabisa so mtu akifanikiwa kumkamata anao msingi wa kisheria.

Israel hana uwezo wa kumpiga mfadhili wake otherwise atapotezwa siku hiyo hiyo kwenye ramani
 
Hapo ni sawa na kusema simba dume amwajibishe simba jike kwa kwenda kuvamia makazi ya swala!, kwanza palestine wapigwe tu kwann wawafuge magaidi.
Ndio huu unafiki sasa unaongelewa, Putin akivamia Ukraine ni haramu ila Netanyahu kuvamia gaza ni halali!!

Kama issue ni ugaidi israel pia inafadhili magaidi mfano Rais wa sasa wa Syria ni Al Qaeda kabisa ila aliingia kwa msaada wa US na Israel kushambulia targets zote zenye silaha za Assad!!

Hata SDF ni branch ya magaidi wa PKK ila wanakua supported na israel but sijawahi ona mkisema israel inafadhili ugaidi.

Unafiki tu
 
Kwa kile walichokifanya Hamas dhidi ya Israel, hakuna nchi itakayomkamata Netanyahu, labda kama Israel ingeanza kuwaua wapalestina bila ya lile shambulio la Hamas.
Haupo serious kwamba Palestina ndio imeanza kuua wayahudi? Yaani miaka yote Israel ilikua haiuwi mpaka oktoba 7? Hivi unajua wapalestina wangapi walikua wanauwawa kila siku tokea 1948?
Jamii ya kimataifa ilikosea sana. Mara baada ya lile shambulio lila la kigaidi la Hamas, ilitakiwa jamii nzima, hasa nchi za kiarabu, zilaani na zitoe tamko la kushirikiana na Israel kuwaangamiza Hamasi
Ndio nini hiki unaandika? Mbona Jordan, Saudia, sio tu zinasaidia ku intercept makombora ya Iran kutopiga Israel bali zilikaa pembeni bila kuwasaidia Gaza alafu ndio justification ya kuua maelfu?

Mbona Israel ilingia Syria tu bila idhini na kuua watu uliona waarabu wamemzuia? Ila Iran ingeingia hivyo Gaza mngesema ina support magaidi !! Acheni unafiki wa double standards.

Al shabaab ikiua Nairobi sio leseni ya jeshi la Kenya kuingia Mogadishu na kuua wamama na watoto!!! Ila humu unahalalisha kuwa makosa ya hamas ni halali kuuwawa kwa raia wasio na hatia
 
Huyo naye ni next target mpumbavu, Yani kuwapiga magaidi amba ni sawa na Maduro, mwache huyo anajilaani yeye mwenyewe... Ukiichezea Israel kiuonevu jua kuna litakalokukuta hata kama sio wewe basi rafikio mpendwa.
 
Kwan hao Ulaya wameshindwa nn kumkamata Netanyahu?
 
Back
Top Bottom