Mwanasiasa bora 2015-2020 PM Kassim Majaliwa ndiye Rais ajaye 2025

rutegeramisi gwategera

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
405
500
Kwa mtazamo mpana Kassim Majaliwa ndiye mwana CCM makini na bora kama CCM itaendelea kuwa madarakani basi huyu PM Kassim Majaliwa ndiye mtu pekee anafaa kuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wana CCM wengi hawana mvuto ni mamluki na wabinafsi vizabizabina wa kujipendekeza ila Kassim Majaliwa ndiye pekee mwenye sifa ya kuwa kiongozi bora kutoka CCM na kuleta mshikamano wa kitaifa.

Tanzania bila upinzani na Demokrasia makini ni hatari kwa ustawi wa maendeleo ya taifa letu.

Mungu mbariki Kassim Majaliwa
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
 

Tayukwa

JF-Expert Member
Dec 11, 2014
1,262
2,000
Laana ya milele ikuangazie wewe na kizazi chako chote , huyu Majaliwa aliyeteka na kuumiza wagombea wa ubunge wa upinzani kwenye jimbo la kwao kama ndio mwanasiasa bora basi nchi hii itakuwa nchi ya kibwege sana !
Sipendi scandal za hawa watawala wetu, lakini mkuu maneno yako tisa ya kwanza ni mazito sana kupewa mtu hasa kwa kutumia maandishi maana wengi hulisoma hilo andiko.

Namuombea msamaha kwa niaba yake.
Nisamehe na mimi pia kwa namna yoyote itayokukwaza
 

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,445
2,000
Rejea Uzi ulioandikwa wenye kichwa cha habari LAANA YA WATU WA KUSINI.

Jua kwamba majaliwa hachomoki Kwenye laana ya watu wa kusini.

Ni suala la muda na uzuri ni kwamba the glimpse of truth has been released ; it is your time now to think and rethink
In politics, nothing happens by accident
 

rutegeramisi gwategera

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
405
500
Laana ya milele ikuangazie wewe na kizazi chako chote , huyu Majaliwa aliyeteka na kuumiza wagombea wa ubunge wa upinzani kwenye jimbo la kwao kama ndio mwanasiasa bora basi nchi hii itakuwa nchi ya kibwege sana !
Mkuu umetumia maneno makali ila nafahamu umeumizwa na uchafuzi ubakaji wa demokrasia ambao umeumiza kila mpenda haki.

Lakini ukweli ni dhahiri huyu bwana hana nguvu anaamlishwa na bosi wake lakini ni mojawapo ya wana Ccm wenye weledi ambao kama Ccm itaendelea bora ya Kassim ana afadhali.

Upinzani na wapenda haki tupo kipindi kigumu katika taifa hili

Anayeweza kufurahia haya yanayoendelea ya kubaka demokrasia ni juha pekee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom