Mwanasiasa afungwa jela kwa kuwaita majaji 'wajinga'

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
753
3,096

Mahakama ya juu nchini Uganda imemuhukumu kifungo cha jela mgombea wa zamani wa urais kwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya majaji , ikiwa ni pamoja na kuwaita majaji "Wapumbavu wasio na uwezo wa kazi yao ".


Ivan Samuel Ssebadduka alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuidharau mahakama, kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo.

Mwezi Sempemba Bw Ssebadduka alikuwa amepeleka ombi latika mahakama ya juu akitaka kusimamishwa kwa kigezo cha mgombea wa urais kukusanya kura za uteuzi.

Pia alitaka kuahirishwa kwa sheria za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona zilizokuwa zimewekwa na wizara ya afya katika mikutano ya kampeni.

Alitumia maneno hayo ya matusi alipokuwa akitetea ombi lake mbele ya majaji.

Hakimu mkuu wa mahama kuu nchini Uganda Alfonse Owinyi-Dollo alinukuliwa akisema kuwa ukosoaji dhidi ya majaji unapaswa kuwa sahihi na wa haki na haupaswi kukiuka haki za watu wengine:
 
Mpumbavu siyo tusi ni kiwango cha juu kabisa cha ujinga (huwezi tena kuelewesha jambo ukaelewa).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom