Mwanasheria wa Zitto atolea ufafanuzi makosa 11 ya Zitto na wenzake

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
447
1479488_630126770382731_1509352392_n.jpg


1504075_630127233716018_1411008223_n.jpg

Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

11/12/2013

ALBERT MSANDO

Baada ya kupokea barua yake ya mashtaka 11 tarehe 01/12/2013 ambayo anashitakiwa nayo na iliyomtaka ajitetee kwa maandishi.

Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB) jana tarehe 10/12/2013 amefanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji za Chama
Pia Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB) ametoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Chama kumueleza nia yake kukata rufaa Baraza Kuu la Chama kupinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani ya Chama.

Kuna sababu mbili za msingi za kukata rufaa;

1. Utaratibu wa kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa.

2. Sababu za kuchukuliwa hatua hizo sio sahihi.


Utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji ni kama ifuatavyo;


Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6 inasema;
Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka yake kwa maandishi na mamlaka
husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

Pia tunapenda ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2 (a), (b), (c) na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema;
Kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza;

a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.


Naomba nichukue fursa hii kufafanua kuwa uongozi wa chama ulifanya mkutano na waandishi mnamo tarehe 26/11/2013 na kusema kwamba marekebisho haya ya Kanuni ya mwaka 2013 ambayo nimewawekea hapo juu, ndiyo utaratibu waliofuata.

Pia walieleza kuwa sikuwa naifahamu na nilidanganywa kwani Kanuni ilishabadilishwa.

Mabadiliko haya ambayo ni katika kipengele (d) kuhusu hatua ya dharura iliyochukuliwa na Kamati Kuu haikugusa kipengele (a) cha Kanuni. Yaani ni kuwa hata kama Kamati kuu itachukua hatua ya dharura kwa mujibu wa kipengele (d), bado kipengele (a) ni lazima ifuatwe na inatamka wazi sharti la kiongozi kupewa mashtaka kwa maandishi na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi. Hii ni haki ya msingi kwa kila utawala au uongozi.


Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hakupewa mashtaka yake aliyakuta ndani ya kikao baada ya kupewa taarifa kwa ujumbe wa simu (text message au sms)
.

Kwa uzito wa makosa hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na kwa kuangalia athari zake kwake yeye binafsi na chama kwa
ujumla, Kamati Kuu ilitakiwa kujiridhisha kwamba Kanuni za Uendeshaji na Katiba zinafuatwa.

Hili linaendana na utaratibu uliotumika kwa Samson Mwigamba
kuvuliwa nyadhifa yake ya uenyekiti wa mkoa. Yeye hakuitwa kabisa kwenye kikao hicho na ni ukiukwaji wa Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6(d) niliyoisoma hapo juu kwamba lazima kiongozi huyo aitwe kwenye kikao.

Sababu zilizotumika ingawaje hajapokea taarifa rasmi ya maandishi kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji ni kwamba yeye ameshirki kwenye kuandaa na kusambaza waraka ambao unasemekana ni mkakati wa ushindi wenye lengo la kupindua uongozi uliopo.


Waraka huo haukumtaja Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kama muandaaji au msambazaji. Waliouandaa hawajaukana na badala
yake wamesema waziwazi kabisa kwa maneno na maandishi kwamba Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe HAHUSIKI.

Sio sawa kumuadhibu Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kwa hisia au tu kwa sababu ya urafiki wake na watu fulani.
Haya ni mapungufu ambayo kwa bahati nzuri Katiba na Kanuni za Uendeshaji zinatoa nafasi ya kurekebishwa kwa kutoa nafasi ya kukata rufaa. Na utaratibu ni huu hapa;

Kwa ufupi, Ibara 6.3.6(d) ya Katiba ya Chama;

"Kiongozi aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho".


Ibara 6.3.6(e) ya Katiba ya Chama;
"Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu".


Kanuni za Uendeshaji zinatoa UTARATIBU ambao unatakiwa ufuatwe ili kiongozi aliyeadhibiwa aweze kutumia HAKI yake ya kukata rufani kwa maneno haya;

Kanuni ya 6.5.8 ya Kanuni za Uendeshaji;
"Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi wa maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumuwezesha kuamua kukata rufani au la"

Kanuni ya 6.5.9 ya Kanuni za Uendeshaji;
"Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu"

Kanuni ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji;

"Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa
taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha mamuzi"

Mpaka hivi sasa hatujapokea taarifa kamili ya mwenendo wa shauri tokea kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 20-21/11/2013 Huo ndio utaratibu ambao Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ameamua kufuata kwa kuheshimu maamuzi ya Kamati Kuu lakini kukatia rufaa maamuzi hayo. Kuheshimu maamuzi sio kuyakubali uhalali wake.

Kumekuwa na matukio ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa fujo na vurugu ikiwa ni pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama. Vurugu hizo baadhi zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya watu.

Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo yanayoendelea na anayakemea na kuwashauriwanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimuviongozi wa kitaifa. Hatua zimeshachukuliwa kukata rufaa na niimani yake kwamba Baraza Kuu la Chama litatenda haki kwakupitia rufaa yake na kutoa uamuzi.

Nawashukuru wote.

ALBERT MSANDO,
Mwanasheria

11/12/2013

 
Kushangilia au kuzomea imo? Maana nahisi kuwepo kwa pumba nyingi sana. Ngija nije.
Hawa jamaa, ni wasaliti. wemeshaandika barua, halafu wanaita press kuvuruga wanachama. Watu kama hawa, hawafai CHADEMA wanafaa sana CCM.
Kwanza huyo mwanasheria gani anasoma oudated document, eti rufaa siku 30, hii imekuwa siku 14. hovyo kabisa

Jamani Ondoeni hawa watu haraka sana, wakafanyie mambo yao CCM. Hatuwataki, nawamind sana hawa, msije mkatuletea balaa waungawana. Kwani lazima Zitto awe CHADEMA jamani, alale mbele.

Hebu angalia lugha ya kinafiki:
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ameamua kufuata kwa kuheshimu maamuzi ya Kamati Kuu lakini kukatia rufaa maamuzi hayo. Kuheshimu maamuzi sio kuyakubali uhalali wake. Kumekuwa na matukio ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa fujo na vurugu ikiwa ni pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama.Vurugu hizo baadhi zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya watu.Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo yanayoendelea na anayakemea na kuwashauriwanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimuviongozi wa kitaifa.

Nani anawapa viroba na pesa.
Kila anayefurahia kurushiwa mawe wenzake naye atarushiwa tu.
 
Asante sana Taswira. Ebu niambie kwa haraha haraka hao waliovalia nguo za chama na wengine wanaoingia unaweza kunote baadhi ya watu mashuhuri waliopo hapo?
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndipo Zitto anapokosa busara au ndio anapodhihirisha malengo yake ni yapi dhidi ya Chadema. Kwa nini mashtaka aliyopewa yajibiwe kwa waandishi habari?

Tiba


Usijitoe ufahamu..

Lisu na Mnyika walivyoitisha press ni sahihi ila kwa Zitto ni kosa¿¿
 
Mkuu Taswira, pamoja sana.

Hakuna mwenye akili timamu atakaye poteza muda wake kukusililiza Taswira!

Kutuletea picha za Mbagala kuzifanya ziwe za Kasulu kumenifanya nikuone mtu wa hovyo hovyo sana;mganga njaa na mwenye uwezo mdogo kama sungura wa kufikiri!
 
Last edited by a moderator:
Yaani huyu mwanasheria kaomba ashikiwe mkoba mahakamani kwasababu ya udhuru huu?.
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom