Mwanasheria wa Serikali akiri serikali ni dhaifu na legelege

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Uchunguzi wa Mauaji
Katika hatua nyingine, Werema amekiri bungeni kwamba Serikali imekuwa dhaifu kwa kutochunguza vifo vya raia ambavyo vimekuwa vikitokea katika mazingira yenye utata na kuahidi kwamba taratibu zinafanywa ili uchunguzi ufanyike.

"Nakiri kwamba tulilegalega
kidogo kwa kutofanya uchunguzi wa mauaji yaliyotokea bila kujua sababu zake, lakini tumejiandaa shughuli hiyo itaanza karibuni".

Alisema uchunguzi wa vifo hivyo utafanywa na Mahakama za Korona (Coroner’s Court) ambazo zilikwishaundwa tangu mwaka 2004 kwa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali namba 252 la Julai 16, 2004.

Mwananchi
 
Sasa Lukuvi alikua anapinga nini hotuba ya muheshimiwa Lema kwa kusema hotuba ile imejaa uchochezi? Kweli serikali ya CCM inatakiwa ipimwe akili.
 
hawa sisiemu wanajichanganya sana,serekali legelege wao wenyewe wanakiri hilo alakini wanataka uitamke kwa staili tofauti,werema amekiri kwa mdomo wake mwenyewe na dhahiri anajua hilo kuwa wapo leglege.jana kuna magamba mmoja naona kajitahidi kumponda kamanda lema alakini sasahivi wajinga wale wamepungua jamani,watanzania wanaelewa kila kinachoendelea kwenye nchi yao.lema alikua ananukuu baadhi ya semi katika vitabu vya wanaharakati wa marekani,sasa yeye kwa ujuha wake anasema kua hile mifano hafai kulinganishwa na mambo yanayoendelea kwetu.mifano haina mipika jamani ,hile ni elimu tosha na inafaa kutumiwa na mtu yeyoye pasipo kuangalia mipaka wala utaifa wa mtu.mtakoma mwaka huu.wanafunzi mmewajengea maghala mkasema ni madarasa,haya wamekubali kuingia kwenye hayo maghala,mkawaambi mtaingia bure hatima yake sasa sio bure tena imekua ni mradi wa walimu wakuu na wenyeviti wa vijiji.mabomu hayo mnatengeneza jamani yakijalipuka msianze kumtafuta lema uchokozi.shaurizenu.
 
Back
Top Bottom