Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe ana 'Digrii ya chupi' - DC Mrisho Gambo

Status
Not open for further replies.
Hata kama alitoa uroda akapata degree ni aibu kumdhalilisha mkutanoni.wanasiasa wanawadharau wasomi sijui nchi inaelekea wapi.

hata hivyo, kwa sheria za serikali za mitaa, DC si msemaji wa halmashauri, na pia si mwajiri wa wafanyakazi wa halmashauri, hivyo kwenda kutoa maneno ya kudhalilisha , ni kinyume cha sheria
 
Kusema ndio kwa EL ni kitu kingine na kuongoza ni kitu kingine. Kama kipimo cha uongozi Tanzania kusema ndio au hapana kwa Lowassa basi yule Laigwanan kaiweka nchi mfukoni.
Mrisho Gambo hana proven records za uongozi ktk nchi hii, ila ana proven records za kujipendekeza na kulitumikia kundi hasimu na Lowasa ndo akapewa fadhila la uDC. Lakini huo upuuzi wenu uishie huko huko CCM, Tanzania ya baada ya ccm kila mtu atapata nafasi za uwezo na sio kwa kupewa na Riz1

tusaidie hizo PROVEN RECORDS za kujipendekeza ili tusikuweke kwenye PROVEN RECORDS za wapika majungu!
 
Hivi huyu ndiyo yule ambaye huwa anaenda kupiga majani kwasemangube? The same DC alianza kumtukana mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe katika kikao cha baraza la madiwani cha tarehe 17/8, alimfukuza mhandisi wa maji katika eneo la Hale kisa kalamba percent kutoka SBI, anaacha bodaboda wanajichukulia sheria mkononi kisa yeye anafuatilia wakulima wa bangi kwenkeyu, amesababisha migogoro kibao kwa kuendesha wilaya kama genge lake la kahawa---- Korogwe poleni sana
 
Sina uhakika kama kasema sababu hata hilo gazet la mwananchi sijaliona,ila kiukweli jamaa hana jipya huyo ni mropokaji na hata U DC kapewa shauri ya kumdhibiti kijana mpambanaji Ole James Millya aliamaua kuacha Uenyekiti wa UVCCM arusha na kukimbilia Chadema,ila uropokaji wake ulimsaidia kijana Ridh1 akamchomekea kwa Baba akapewa U DC kutoka pale Halimashauri ya arusha but ushauri wangu wa bure kijana nenda taratibu muda huu umekuwa kioo cha jamii unaangaliwa kama ni kweli kauli hiyo katoa Basi Kikwete hana Bahati na wakuu wake wa wilaya.Be carefull kijana Mrisho Gambo
 
''There is nothing more than nothing,where there is nothing, hapo ngoma droo! waswahili wa pemba hao...teh teh
 
Mrisho umeangusha vijana wenzako wa magamba, maana vijana mliochaguliwa mlipaswa kuonyesha njia.
 
Huyo mwanasheria ni mwanamke??? maanake ndio wanatukwana kwa hayo. If that the case, huo ni udhalilishaji wa kijinsia (sexual harrassment). Kauli hii ingekuwa nchi za wenzetu angekuwa yuko mahakamani. Una uhakika gani kwamba ni degree ya chupi. Anaweza kuthibitisha??? Wanaharakati mko wapi??? By the way, haya ndio matatizo ya kupeana vyeo, kabla ya watu kujenga au kuwa na misingi ya uongozi. Kuwa rafiki wa Ri z 1 na kupewa ukuu imekuwa nongwa na haki ya kutukana wengine? Ole wako kijana; kwa hivyo hufiki mbali.
 
Ni wa kike nini? Sasa kama ndo keshagundua hivyo atawasaidia je wananchi wake?
 
Wateule wa Ridhiwani hao, yani wanafanya ofisi za umma kama vijiwe vya kahawa na kucheza bao. Huyu jamaa kafanya vijana tuonekane hatuna weledi na uwezo wa kuongoza. Ukweli ni kuwa haya ndio matunda ya kuwapa watu nafasi za uongozi ambao hawajakomaa kiakili na kiroho.

Well said Mkuu. Am trying to put myself into the shoes of that lawyer! Lazima alikuwa embarassed na kutamani ardhi ipasuke apotelee humo!
 
digrii za chupi zipo, wala hazijifichi, na wala si kashfa. Kashfa ni kwa mtu kuvua chupi ili apate shahada.
 
azbitishe degree yake sio ya chupi kwa kumburuza mahakamani

...halafu huyo lawyer apewe mtihani wa law wa average lawyer ili kung'oa mzizi wa fitna. In short academics in Tanzania have been FU**ED UP. And we shall pay a dear price for that.
Ila Mh. DC amewadhalilisha wenye vyeti (baadhi yao ni wasomi ati).
 
Huyo mwanasheria asipochukua hatua bas atakuwa ametudhihilishia degree yake ni ya kias hicho, nao Serikali na Chama husika wasipomchukulia hatua DC, bas nao watakuwa wametudhihilishia kuwa utawala huu ni wa Ch*p* zaidi..!!
 
digrii za chupi zipo, wala hazijifichi, na wala si kashfa. Kashfa ni kwa mtu kuvua chupi ili apate shahada.

mi nashangaa watu wanashindwa kujadili kama kweli degree ya huyo mama ni ya chupi au la..wao wanaleta ufuasi wa siasa..hizo degree zipo nyingi sana na ndo zinazoleta matatizo kwenye jamii.unaona mtu msomi lakini maamuzi yake hayaendani na cheti chake,tukijadili vizuri hiyo mada tutapata mengi kuliko kuhamishia lawama kwa DC.
 
Huu udhalilishaji wa hali ya juu. ni udhalilishaji mbaya kuliko alivyofanya mnali. ni afadhali angemchapa viboko
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom