Mwanasheria na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms amuandikia barua DPP kukiri makosa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Washtakiwa watano wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi akiwemo wakili, Dk Ringo Tenga wamemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuomba kukiri makosa yao.

Wakili wa washtakiwa hao, Byrson Shayo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Ijumaa Septemba 27, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Dk Ringo ambaye ni Mkurugenzi na mwanasheria wa kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita, likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababishia Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) hasara ya Dola za Marekani 3,748,751.22.

Mbali na Dk Tenga, washtakiwa wengine ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, Novemba 20, 2017 wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Mawakili wanaowatetea washtakiwa hao ni Alex Mgongolwa, Semi Malima, Constancia Sospeter, Jeremiah Mtobesya na Bryson Shayo.

Katika kesi ya msingi, Dk Ringo na wenzake wanadaiwa kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14, 2016 Dar es Salaam, walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango cha Dola za Marekani 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia, katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya TCRA kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa kiasi cha Dola za Marekani 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

Washtakiwa hao wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti za Dola za Marekani 466,010.07 kwa TCRA.

Katika shitaka la utakatishaji wa fedha, Hafidhi, Noni, Tenga na Chacha, wanadaiwa walitumia ama walisimamia Dola za Marekani 3,282,741.12 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana na mashtaka yaliyotangulia.

Vile vile ,washitakiwa hao wanadaiwa kuisababishia TCRA hasara ya Dola za Marekani 3,748,751.22.
 
hawana hizo dola milioni kumi, hata moja HAWANA!

Wangekuwa washatoka... bei ya DPP kipindi chote hiki kwa watu wote ilikuwa TSH. MILIONI MIA MBILI unatoka...

plea bargains zimeanza tokea mwanzoni mwa awamu hii, hawa wote walikuwa na hizo options

hawakulipa, means HAWANA KITU!

labda awatoe bure! DPP na Rais wanafanya usanii wa wazi wazi
 
hawana hizo dola milioni kumi, hata moja HAWANA!

Wangekuwa washatoka... bei ya DPP kipindi chote hiki kwa watu wote ilikuwa SHILINGI MILIONI MBILI unatoka...

plea bargains zimeanza tokea toka mwanzoni mwa awamu hii, hawa wote walikuwa na hizo options

hawakulipa, means HAWANA KITU!

labda awatoe bure! DPP na Rais wanafanya usanii wa wazi wazi
Huyo ndiyo mtu pekee anayejiita Rais wa wanyonge ila anaongoza kwa kuwatesa wanyonge kama ifuatavyo:-
1. kuwaonea watu wasio na hatia hata kidogo.
2. kuwanyima ajira watoto wa wanyonge.
3. kuwafukuza na kuwaachisha kazi wanyonge.
4. Hajawahi kukemea wanyonge wanavyotekwa na kuuliwa mfano akwelina.
 
Acha masikhara wewe milioni mbili?
 
Huyo ndiyo mtu pekee anayejiita Rais wa wanyonge ila anaongoza kwa kuwatesa wanyonge kama ifuatavyo:-
1. kuwaonea watu wasio na hatia hata kidogo.
2. kuwanyima ajira watoto wa wanyonge.
3. kuwafukuza na kuwaachisha kazi wanyonge.
4. Hajawahi kukemea wanyonge wanavyotekwa na kuuliwa mfano akwelina.
Akili zenu Hata Shetani anaziogopa
Sijui Mnawazaga nini
Mnalo Lipigia kelele leo kesho hilohilo mtalipinga
Kunasiku mtakataa hata vivuli vyenu
Mmejawa unafiki na uzandiki
Kwa bahati nzuri mpo wachache hata kwenye kisoda hamjai
Rais Tulio wengi tumemuelewa
Tena sana tu na huyu ndio Rais mpaka 2025
Hilo halita badilika
 
Ni bora wawaache tu kuna baadhi ya wafanyakazi wao wapo mtaani wanataabika tu,hii kidogo inaweza saidia kurudisha uchumi ukae vizuri ikiwa kama mabosi wa makampuni wakiwekwa ndani basi tunaotaabika ni sie watu wao wa chini
 
Akili zenu Hata Shetani anaziogopa
Sijui Mnawazaga nini
Mnalo Lipigia kelele leo kesho hilohilo mtalipinga
Kunasiku mtakataa hata vivuli vyenu
Mmejawa unafiki na uzanfiki
Kwa bahati nzuri mpo wachache hata kwenye kisoda hamjai
Rais Tulio wengi tumemuelewa
Tena sana tu na huyu ndio Rais mpaka 2025
Hilo halita badilika
Mko wengi mnaomuelewa?😂😂😂na wasiomuelewa wako wachache hata kisoda hawajai?😂😂😂😂😂...Acheni kutesa nafsi zenu kwa watawala ambao wanapita tu.semeni ukweli muwe huru
 
Akili zenu Hata Shetani anaziogopa
Sijui Mnawazaga nini
Mnalo Lipigia kelele leo kesho hilohilo mtalipinga
Kunasiku mtakataa hata vivuli vyenu
Mmejawa unafiki na uzanfiki
Kwa bahati nzuri mpo wachache hata kwenye kisoda hamjai
Rais Tulio wengi tumemuelewa
Tena sana tu na huyu ndio Rais mpaka 2025
Hilo halita badilika
That is the plain truth that you don't want to hear, brother. What is wrong with you, CCM stooges?
Does someone pay you to defend the garbage of your colleague?
 
Huyo ndiyo mtu pekee anayejiita Rais wa wanyonge ila anaongoza kwa kuwatesa wanyonge kama ifuatavyo:-
1. kuwaonea watu wasio na hatia hata kidogo.
2. kuwanyima ajira watoto wa wanyonge.
3. kuwafukuza na kuwaachisha kazi wanyonge.
4. Hajawahi kukemea wanyonge wanavyotekwa na kuuliwa mfano akwelina.
Bado hatujasahau lile la kubomoa nyumba za wanyonge Morogoro road bila ya fidia
 
Akili zenu Hata Shetani anaziogopa
Sijui Mnawazaga nini
Mnalo Lipigia kelele leo kesho hilohilo mtalipinga
Kunasiku mtakataa hata vivuli vyenu
Mmejawa unafiki na uzanfiki
Kwa bahati nzuri mpo wachache hata kwenye kisoda hamjai
Rais Tulio wengi tumemuelewa
Tena sana tu na huyu ndio Rais mpaka 2025
Hilo halita badilika
Watu wanafiki huwa hawabebeki ni kuwatazama tu. Ila wajue Magufuli ana Mungu
 
Huyo ndiyo mtu pekee anayejiita Rais wa wanyonge ila anaongoza kwa kuwatesa wanyonge kama ifuatavyo:-
1. kuwaonea watu wasio na hatia hata kidogo.
2. kuwanyima ajira watoto wa wanyonge.
3. kuwafukuza na kuwaachisha kazi wanyonge.
4. Hajawahi kukemea wanyonge wanavyotekwa na kuuliwa mfano akwelina.
Nani kamwonea? Nani kamnyima ajira umesikia ukisoma lazima akuajiri? ?
Nani kamfukuza kazi kama si wale wa vyeti feki na magumashi
Ulichoongea ni wazi ww ni victim na hujaonewa
 
Back
Top Bottom