Mwanasheria Mkuu Zanzibar Akamatwa baada ya kupiga kura ya Hapana

Status
Not open for further replies.

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Leo muda mfupi uliopita Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud baada ya kupiga kura ya wazi ya Hapana kuhusu katiba amekamatwa na watu wa idara ya usalama na sasa yupo njiani akirejeshwa Zanzibar kama ni kweli anapeleka Zanzibar ama Mambwepande .......

Hali hii ni ya hatari na Dodoma tayari kuna tayahari kubwa sana , ila hali inawez kuchafuka wakati Wowote visiwani Zanzibar kutokana na uonevu huu ambao unafanywa na watawala wa CCM .

Updates:
Hali ilikuwa mbaya Sana mara baada ya kupiga kura kwani wabunge wa CCM znz walitaka kumpiga ndio akalazikima kutolewa ukumbini chini ya ulinzi mkali na kufungiwa kwenye ofisi moja akiwa ameandamana na Pandu Ameir Kificho, Balozi Seif Idd, Nahodha , Pinda na baada ya muda aliondolewa hapo Akiwa ameandamana nafPandu Kificho kwenye gari yake kupitia lango la Waziri Mkuu akiwa ameambatana na msafara wa maafisa usalama, na kupelekwa Airport ......

wale wenye Mashaka na habari hii wasilianeni na Dom mtapataukweli ,

Inasemekana amepelekwa airport yadDodoma , ila not yetdconfirmed ,,,,,

Kumbukumbu :::
1. Aboud Jumbe Mwinyi mwaka 1984 , alinyanganywa Urais akiwa Dodoma na mpaka leo yuko Kigamboni
2. Maalim Seif Shariff and wenzake mwaka 1988 , alinyanganywa uwaziri kiongozi akiwa Dodoma
3. Mansour Himid , mwaka 2013 alinyanganywa Ubunge akiwa Dodoma.
4. Othman Masoud , mwanasheria mkuu znz atapona kweli ?

=========================================


Wadau,

Majira ya Saa saba Alasiri, Mtumiaji wa Jamiiforums ajulikanaye kama Haki Sawa ameanzisha mada yenye kichwa cha Habari "Mwanasheria Mkuu Zanzibar Akamatwa Baada ya Kupiga Kura ya Hapana". Katika mada hiyo pamoja na mambo mengine, Haki Sawa amesema kuwa Mwanasheria huyo Othuman Masoud amekamatwa na Maafisa Usalama na amepelekwa uwanja wa ndege wa Dodoma kurejeshwa Zanzibar au Mabwepande. Kwamba CCM wamechukizwa na kitendo cha Mwanasheria huyo kupiga kura ya Hapana na hivyo wanataka kumshughulikia.

Wadau, hakika hizi ni propaganda zenye nia ya kuvuruga mchakato huu wa Katiba mara baada ya hila zao mbaya kushindikana. Mleta mada anakusudia kuwaaminisha Watanzania kuwa wale wote wanaopiga kura za HAPANA ni maadui wa CCM na Serikali. Pia mleta mada anakusudia kuvihusisha vyombo vya dola na tukio la kutekwa na kuteswa Dr Steven Ulimboka kabla ya kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande. Aidha, mleta mada anakusudia kujenga chuki miongoni mwa Wazanzibari na Watanzania bara hasa alipoweka orodha ya baadhi ya Wazanzibari ambao kwa mtazamo wake hawakutendewa haki na CCM. Pia Mleta mada anakusudia kujenga hofu miongoni mwa wakazi wa Dodoma kuwa hali ni tete na kwamba wasifanye kazi zao kutokana na tukio hilo.

Ukweli upo wapi? Mtakumbuka kuwa leo ni siku ya tatu ya upigaji kura. Kwa siku ya Leo, ni wale tu Wabunge ambao hawakubahatika kupiga kura siku ya Kwanza na ya Pili ndio waliopiga kura. Baadhi ya wabunge hao ni Januari Makamba na Mbunge wa Mafya. Pia alikuwepo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud ambaye alikuja kutimiza haki yake ya kikatiba ya kupiga kura.

Katika kupiga kura, OTHMAN MASOUD, Mwanasheria wa Zanzibar ambaye alijitoa kwenye kamati ya Uandishi na kususa vikao vya Bunge akidhaniwa kuwa ameungana na UKAWA aliingia Bungeni muda mfupi kabla ya bunge kuahirishwa na kuomba kupiga kura. katika kupiga kura, Masoud alichagua kupiga kura ya wazi ambapo kwa ujumla wake amepiga kura ya NDIYO kwa Ibara nyingi. Hata hivyo alipiga kura ya HAPANA kwa baadhi ya Ibara ambazo hakubaliani nazo jambo ambalo si la kushangaza na wala yeye si wa kwanza kufanya hivyo. Ibara alizopiga kura ya hapana ni 2,9,86,70 hadi 75, 128, 129,158,159,160,161,243 hadi 251 pamoja na nyongeza ya kwanza. Ukichukua Jumla ya Ibara za Katiba Inayopendekezwa ambazo ni 289 ukitoa na Ibara alizopinga ambazo jumla yake ni 23 unapata jibu kuwa Ibara alizounga mkono ni 266. Hakika inashangaza sana kuona mtu akipotosha kuwa Ibara 23 za HAPANA ni nyingi ukilinganisha na Ibara 266 za NDIYO.

Baada ya Masoud kupiga kura, Mbunge mmoja wa Zanzibar Yahaya Kassim Khamis aliomba mwongozo kwa Mwenyekiti ambapo alitaka kufahamu ni kigezo gani kimetumika kumruhusu apige kura ilhali yeye kama Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar hakuwepo wakati wa kutunga Katiba inayopendekezwa na badala yake amejitokeza siku ya kupiga kura. Kassim alisikika akisema kuwa Othman Masoud ameonesha usaliti mkubwa kwa Wazanzibari kwani kutokana na taaluma yake ya uanasheria alipaswa kuusimamia mchakato huo hadi mwisho ili kuhakikisha kuwa maslahi ya Wazanzibari yanalindwa. Kassim alisikika akisema kuwa Othman Masoud ana dharau sana kwa vile anajiona ni msomi wa sheria kuliko Wabunge wengine waliotoka Zanzibar. Pia alisikika akisema kuwa Othman Masoud hafai kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kutokana na usaliti aliouonesha.

Akijibu hoja za Kassim, Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta alisema kuwa Othman Masoud amekuja kutimiza wajibu wake wa kupiga kura na ni haki yake ya kikatiba na kikanuni. Alisema kuwa kura hazikupigwa kulingana na cheo cha mtu bali kitendo cha kuwa mbunge. Akijibu hoja kwa nini ajitokeze siku ya kupiga kura tu, Sitta alisema kuwa hayo ni maamuzi yake na yeye hawezi kumsemea. Alisema kuwa kimsingi bunge hilo lina wabunge 629 na kwamba wakati wowote kama kuna mbunge alikuwa nje kwa muda mrefu na anataka kupiga kura angeruhusiwa. Anasema kuwa ndo maana hata wale wabunge wawili wa UKAWA ( hakutaja majina yao) waliruhusiwa kupiga kura ijapokuwa hawakushiriki kwenye mchakato wa kutunga katiba. Anaamini kuwa ingawa walikuwa nje ya ukumbi wa bunge, walikuwa wanafuatilia mjadala na walipouona ukweli wakaamua kuja kupiga kura.

Kilichojitokeza baada ya ufafanuzi wa Sitta ni kwamba Wazanzibari wengi walionekana kupaza sauti wakimshutumu Masoud kutokana na usaliti wake kwa Wazanzibari. Baadhi walisikika wakisema kuwa watampiga kwa unafiki aliouonesha. Kutokana na hali hiyo, Maafisa Usalama wa Bunge walichukua hatua za haraka kulinda usalama wake. Hatua ya kwanza waliyochukua ni kumzuia asitoke mapema ndani ya ukumbi wa bunge ili asidhuriwe na wabunge wenye hasira. Pili walimpitisha kwenye lango tofauti na lile wanalopita wabunge. Tatu waliendelea kumsindikiza hadi nje ya bunge. Hii yote ni kuhakikisha kuwa Othman Masoud anakuwa salama wakati wote akiwa ndani na nje ya viunga vya bunge na nimedokezwa kuwa amepewa ulinzi maalum kutokana na tishio lililojitokeza Bungeni.

Wadau, kwa hali hiyo, sijajua mantiki ya mleta mada kuwagombanisha Wazanzibari na Watanzania bara ilhali mvutano ulikuwa baina ya Wazanzibari wenyewe. Hakika huu ni uchochezi uliopindukia. Alichokifanya Haki Sawa hakivumiliki na mini kwa vile nilikuwepo ndani ya Ukumbi wa Bunge na nilifuatilia kwa karibu tukio hilo hakika nalaani hiki alichoandika mdau mwenzetu.

 
ccm watahangaika sana, ila watanzania tumeshajua ukweli ni upi, wamejipa moyo katiba itapatikana sasa wameumbuka, na wale wabunge wa baraza la wawakilishi nawaonea sana huruma.
 
Si Lichaburuma limekuja hapa na calculation zake za kuumba na kusema kapiga kura ya wazi! Swali Dodoma wanatengeneza katiba au Amri
 
Leo muda mfupi uliopita Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud baada ya kupiga kura ya wazi ya Hapana kuhusu katiba amekamatwa na watu wa idara ya usalama na sasa yupo njiani akirejeshwa Zanzibar kama ni kweli anapeleka Zanzibar ama Mambwepande .......

Hali hii ni ya hatari na Dodoma tayari kuna tayahari kubwa sana , ila hali inawez kuchafuka wakati Wowote visiwani Zanzibar kutokana na uonevu huu ambao unafanywa na watawala wa CCM .

more to come .

wakimfanyia kama ulimboka hapatakalika cnhi nzima
 
mmmh hali inatisha kwa kweli ,,,mboni yanalazimisha vitu haya maccm
 
Sio kirahisi na kwa uwazi hivi! Mmmh sidhani...

Hata kuwe na panic ya namna gan weledi ndio dira!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Leo muda mfupi uliopita Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud baada ya kupiga kura ya wazi ya Hapana kuhusu katiba amekamatwa na watu wa idara ya usalama na sasa yupo njiani akirejeshwa Zanzibar kama ni kweli anapeleka Zanzibar ama Mambwepande .......

Hali hii ni ya hatari na Dodoma tayari kuna tayahari kubwa sana , ila hali inawez kuchafuka wakati Wowote visiwani Zanzibar kutokana na uonevu huu ambao unafanywa na watawala wa CCM .

more to come .

Kama habari hii ni ya kweli ..mwili wangu umepigwa ganzi..naanza kumkumbuka Jumbe, salmini Amour , etc.... TZ tunaelekea wapi??? Eheee MOLA inusuru nchi hii na mambo haya.
 

Attachments

  • unnamed (28).jpg
    unnamed (28).jpg
    26.1 KB · Views: 1,506
  • IMG 0702.jpg
    IMG 0702.jpg
    245.9 KB · Views: 1,502
  • DSC05552.jpg
    DSC05552.jpg
    191.4 KB · Views: 1,454
Mkuu ujichunge na wewe pia kama hii ni kweli. Keep us up to date with any new info but please be extra careful.

Leo muda mfupi uliopita Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud baada ya kupiga kura ya wazi ya Hapana kuhusu katiba amekamatwa na watu wa idara ya usalama na sasa yupo njiani akirejeshwa Zanzibar kama ni kweli anapeleka Zanzibar ama Mambwepande .......

Hali hii ni ya hatari na Dodoma tayari kuna tayahari kubwa sana , ila hali inawez kuchafuka wakati Wowote visiwani Zanzibar kutokana na uonevu huu ambao unafanywa na watawala wa CCM .

Inasemekana amepelekwa airport yadDodoma , ila not yetdconfirmed ,,,,,

more to come .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom