johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,751
- 141,615
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus Kilangi amewaonya CHADEMA kutowabugudhi wabunge wa chama hicho wa viti maalum kutoka chama hicho.
Profesa Kilangi amesema, mchakato wa Wabunge wa viti Maalum kutoka CHADEMA umefuata Sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.
Awali Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai alisema, kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda Wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote.
Kuhusu Wabunge 19 wa viti Maalum kutoka CHADEMA Bw Ndugai alisema wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu.
Amesema majina ya wabunge wa viti maalum alipewa na na Tume ya Uchaguzi, na kazi yake ni kuwaapisha Wabunge hao na ameshafanya hivyo.
Maendeleo hayana vyama!