Mwanasheria Mkuu: Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu waliapishwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba, CHADEMA isiwaguse

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus Kilangi amewaonya CHADEMA kutowabugudhi wabunge wa chama hicho wa viti maalum kutoka chama hicho.

Profesa Kilangi amesema, mchakato wa Wabunge wa viti Maalum kutoka CHADEMA umefuata Sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.

Awali Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai alisema, kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda Wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Kuhusu Wabunge 19 wa viti Maalum kutoka CHADEMA Bw Ndugai alisema wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu.

Amesema majina ya wabunge wa viti maalum alipewa na na Tume ya Uchaguzi, na kazi yake ni kuwaapisha Wabunge hao na ameshafanya hivyo.

Maendeleo hayana vyama!


IMG-20201126-WA0016.jpg
 
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa CHADEMA Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama.

Baada ya sauti hizo kuvuja mara moja chama kilitangaza kikao cha dharura cha kamati kuu kuwahoji ili waweze kuchukuliwa hatua kali sana ikiwa pamoja na kufukuzwa CHADEMA.

Matokeo yake baada ya kikao cha kamati kuu hao wabunge wauaji walisamehewa na kutakiwa kuomba radhi tu!

Kama hali ni hiyo, wabunge wa viti maalum CHADEMA si wauaji na wala hawajatishia kumuuwa mtu yoyote ila wanajaribu tu kutumia haki yao ya kikatiba iweje wafukuzwe CHADEMA?
Kweli kuwa mwanamke CHADEMA ni dhambi kubwa kuliko wapanga mauaji waliosamehewa??

Tusubiri na kuona kesho kikao cha kamati kuu CHADEMA kitaamua nini ,bila shaka Mbowe is going to be tested again na maamuzi tofauti na kufukuza yatamwimalisha ,na maamuzi ya kufukuza hao wanawake itakuwa ni kiss of death kwa Mbowe na CHADEMA kwa ujumla.
 
Unaleta vitu viwili tofauti, uasi na usaliti.
Sasa endelea
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa Chadema Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama...
 
Mwanasheria mkuu wa serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa Chadema ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya Chadema kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Source: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!
Anayebidi aongelee hili suala kwa sasa ilibidi awe NEC lakini nao simu hawapokei wakipgiwa. Wanaona aibu hata kutoa matamko. Sasa huyu mwanasheria mkuu huo mchakato wa ndani ya CHADEMA alikuwepo mpaka apingane na Katibu wa chama!

Kweli Tanzania ina ajabu sana.
 
Mwanasheria mkuu wa serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa Chadema ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya Chadema kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Source: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!
Huyo hana tofauti na mkewe mdogo,kazi kuropoka kma mahera
 
Napata shida sana kuona CCM wenzangu tuna angaika na maswala ya CHADEMA, waacheni waumane...

AG, CHADEMA wakifanya kikao chao na kuazimia kuwa futa uanachama ni hatua gani utachukua? Ni itakuwa dhidi ya taasisi au utachukua kwa mmoja mmoja na kuiacha taasisi salama?

Kwa CCM wenzangu kushabikia hili ina tuingiza moja kwa moja ktk swala lenyewe, hivyo ni bora waumane wao kwa wao...

Maswala yao ya Ndani tuwaachie wenyewe, ili mradi wafate sheria za nchi.

Nawasihi tuwaache wapambane na mambo yao... Mfumo dume hauta kuja kuisha kuanzia ktk familia, ktk taasisi za kiimani mpka ktk serikali

Sasa wanao pinga mfumo Dume ktk siasa wana ajenda zao

Mh. Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi alieleza vizuri sana ktk hotuba yake na ktk maswali na majibu

Kidumu chama cha mapinduzi...
 
Mwanasheria mkuu wa serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa Chadema ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya Chadema kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Source: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!

AG anahusika Vipi na maamuzi ya CDM?.
 
Hivi Lipumba alipowavua wabunge 8 viti maalum hawakuwa wameapa kufuata vigezo vyote vya sheria?

Wakitimuliwa sio sababu ya kanuni kufuatwa kwenye kupitishwa kwao bali insubordination ya maazimio ya kamati kuu whether walifanya collusion na mtu au lah wataenda naye na maji.
 
Mwanasheria mkuu wa serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa Chadema ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya Chadema kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Source: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!
Mkono wa sheria utawafuata vipi? Wakati mwingine ni busara kujinyamazia.

Amandla...
 
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa Chadema Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama....

Kwa kweli chama mboga mboga wana huruma. Kama aliyo nayo mbwa mwitu kwa mwana kondoo!
 
Hivi kuna mtu anayejitambua anasoma huo uchafu uitwao gazeti la Uhuru?
Jaji na waziri Mkuu wetu Mstaafu Mzee Joseph S. Warioba na wazi wakati anafungua baraza la Habari Tanzania alisisitiza watanzania tuanze kufuatilia taarifa za vyombo vya habari vya hapa nyumbani. Ingawa alisisitiza waandishi nao waongoze juhudi. Tuvipende vya kwetu nchi yetu istawi.
 
Back
Top Bottom