Mwanasheria Mkuu: Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu waliapishwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba, CHADEMA isiwaguse

Hakuna MTU mkubwa kuliko taasisi...
Ulicho elewa ni kwamba , umekariri taasisi zingine mifumo imefanya watu kuwa wakubwa kuliko chama , mfano mzuri ni MEMBE tizama ukubwa alionao lakini angalia impact uliyo iacha baada ya kuondoka ccm =o , lakini tizama chadema sasa hivi
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

Attorney General amewaonya CHADEMA kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Chanzo: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!


Marahii mwanasheria wa serikali kawa mwanachadema , kawa mwanasheria wa Chadema .We Pimbi mnahangaika bure na sarakasi zenu Dona kantri , watoa tilioni mbili wanaona Kila kitu hawayotoa hela .
 
Screenshot_20201127-132528_Chrome.jpg


My take

Nimegundua ccm katika hili wanadili na tazizo na sio na chanzo cha tatizo.
 
Hivi mbingu ipo kweli? Maana hawa hawa viongozi wa serikali unaowaona nyumba za ibada lakini kauli zao hata mtoto mdogo hawezi kuzungumza
 
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus Kilangi amewaonya CHADEMA kutowabugudhi wabunge wa chama hicho wa viti maalumkutoka chama hicho.

Profesa Kilangi amesema, mchakato wa Wabunge wa viti Maalum kutoka CHADEMA umefuata Sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.

Awali Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai alisema, kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda Wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Kuhusu Wabunge 19 wa viti Maalum kutoka CHADEMA Bw Ndugai alisema wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu.

Amesema majina ya wabunge wa viti maalum alipewa na na Tume ya Uchaguzi, na kazi yake ni kuwaapisha Wabunge hao na ameshafanya hivyo.

Maendeleo hayana vyama!


Inaniwia vigumu sana kuamini kuwa tuna watu kwenye nafasi nyeti za uongozi nchini wenye matatizo ya kufikiri sawa sawa.Matamko yote ni ishara ya "udhaifu".Tujipe pole kwa kuongozwa na imbeciles!
 
Hv hata Kama ni kupenda vya ndani nadhani ni vile vnavyojitambua na sio kujaza propaganda za kijinga kama gazeti tajwa full kichefuchefu nyoo!
Jaji na waziri Mkuu wetu Mstaafu Mzee Joseph S. Warioba na wazi wakati anafungua baraza la Habari Tanzania alisisitiza watanzania tuanze kufuatilia taarifa za vyombo vya habari vya hapa nyumbani. Ingawa alisisitiza waandishi nao waongoze juhudi. Tuvipende vya kwetu nchi yetu istawi.
 
Back
Top Bottom