Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar: Muungano unaweza kuvunjwa endapo...

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Mwanasheria MKuu wa Serekali ya Zanzibar: asema Muungano unaweza kuvunjwa Pindipo Wananchi wa Z'bar wakiamua hivyo.

IMG_0783.JPG


Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh othman Masoud Othman​


Na Mwinyi Sadallah | 20th July 2012

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaweza kuvunjika kama wananchi hawataridhishwa na misingi ya muungano wenyewe.

Alisema hayo wakati akifafanua hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) mjini Zanzibar, baada ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria katika kikao kinachoendelea huko Chukwani.

Alisema si kweli kwamba muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauwezi kuvunjika kama wanavyoamini baadhi ya watu.

"Sio kweli kwamba muungano hauwezi kuvunjia…unaweza kuvunjika kama wananchi watakuwa hawakuridhishwa na misingi ya muungano wenyewe" alisema.

Alisema kwamba, kasoro za kikatiba katika mungano wa Tanzania zilianza kuonekana tangu kuasisiwa kwa kwake mwaka 1964 na kusababisha malalamiko kutoka pande zote mbili za muungano huo.

Othman alitoa mfano kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuchaguliwa kuwa Rais bila kupata kura hata moja Zanzibar au jimbo la uchaguzi kwa chama chake.

Aidha, alisema katika Katiba ya Tanzania kuna vifungu vingi vya sheria vimekaa kimya kuhusu nafasi ya Zanzibar katika muundo wa muungano kutokana na kusema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano bila ya kuweka wazi kama nchi mkoa au wilaya.

Mwansheria huyo alisema tatizo kubwa la muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kwamba haujajengwa na misingi mathubuti wakati wa kuanzishwa kwake.

"Muungano huu hauna tofauti na watu waliojificha katika boksi na kushindwa kufahamu kinachoendelea nje na kujikuta wakipoteza hewa" alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kutumia nafasi ya kutoa maoni katika Katiba mpya yatakayosadia kuimarisha muungano huo.
 
Akili zao zinafikiria kama Malawi wanachowaza!!mafuta na Gas si vingine!
 
..he is just repeating what Mwalimu Nyerere said long time ago.

..shime wa-ZNZ, the ball is in ur court. Vunjeni muungano.

..wa-ZNZ msilete usanii wa "muungano wa mkataba."
 
Hivi hakuna jingine la kuzungumzia kutoka Zanzibar zaidi ya vitisho vya kutaka kuvunja Muungano kila kukicha?
 
Bravo mwanasheria zanzibar. Mwanasheria zanzibar ana upeo wa juu na ujasiri kuliko huyu wa bara, jaji werema.
 
Tazama hii video kuanzia dakika ya 27

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom