Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alikuwa Makamo Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Tanzania

mwetanano

Member
Nov 2, 2010
6
0
Ndugu wana-JF, kumekuwa na tuhuma juu ya Tume ya Uchaguzi Tanzania kutokuwa huru na hivyo kupendelea chama tawala wakati wa chaguzi za viongozi. Inasemekana hali hiyo husababishwa na ukweli kuwa viongozi au wajumbe wa Tume hiyo huwa wamewekwa hapo na serikali iliyoko madarakani hivyo kuipendelea kama njia ya kulinda ajira zao au kupata manufaa zaidi siku za mbeleni.

Mwanasheria mkuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Jaji Othman Omar Makungu, aliyeteuliwa na kuapishwa jana alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania na alihusika sana katika 'kuhakiki' kura za rais kabla ya kuzitangaza akiwa na Mwenyekiti wake Jaji Lewis Makame.

Je, hii ni njia ya kupeana asante kwa namna ya 'nikune nami nikukune' au wadau mnaona imekaaje hapo?

Nawasilisha..
 
kwa wnzetu hii ni Kasfa kubwa sana, ila hapa Bongo huyo ni shujaa
 
Tazama hii video kuanzia dakika ya 27

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom