Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Mwanasheria mkuu wa serikali Werema amesema kuwa Tanzania inahitaji marekebisho tu katika katiba ya sasa na siyo kuandikiwa mpya.
Chanzo:TBC1 Habari saa 2:00 usiku
KWA KAULI HII YA WEREMA, SAED MWEMA AGIZA MABOMU YA KUTOSHA TUFUNGUE MWAKAMPYA UWANJANI MPAKA KIELEWEKE
Kuna kauli kibao zinazojikanganya kanganya kutoka kwenye Serikali ya Mhe Kikwete kuhusu kiu yetu sisi wananchi kujiandikia upya katiba yetu sasa hivi.
1. Makamba; HAKUNA NAFASI YA KUSIKILIZWA MTU HAPA,
2. Chiligati, CHADEMA WASILETE UTANI TUENDA BUNGENI KUWAFUKUZA wote,
3. Chiligati, aaahhh, haya madai ya CHADEMA ni ya msingi na YANAZUNGUMZIKA,
4. Kombani alianza na SUALA LA KATIBA HAPAN, NI GHARAMA NA WALA SI MUHIMU,
5. Mzee Tyson, kuhusu madai ya KATIBA sisi serikali TUNAZO ZILE NJIA ZETU NA WALA HUA HAZITANGAZWI,
6. Alipofika Jaji Mstaafu Mzee Bomani; Suala hili ni halikwepeki na ninashauri Serikali iteue JOPO LA WATAALAM kuliangalia KATIBA na kubaini MAHITAJI yaliomo;
7. Mzee Ruksa; Kwa nini Wa-Tanzania muhitaji KATIBA MPYA SASA HIVI, KUNA NINI???
8. Mwana-JF 'Dar es Salaam' aka JK; Nani kasema Mheshimiwa Kikwete mwenyewe hapendi Kuandikwa KATIBA MPYA???
8. 'Mtoto wa Mkulima' alipofika kwenye kio (TV); Nitamshauri Raisi ateue JOPO LA WATAALAM kuipitia katiba na kushauri HATIMA YAKE NI NINI.
9. Kombani; Leteni rasimu sifuri zenu za KATIBA MPYA kwangu,
10. Jaji Mkuu Augustino Ramadhani; Kwa KATIBA MPYA Tanzania hii kazi tulihitajika kulikamilisha tangu majuzi.
11. Mzee Warioba, CCM Uadilifu lakini masikini, Serikali isicheleweshe zaidi KATIBA MPYA
12. Mzee wa RICHMOND / DOWANS, CCM Ufisadi Mabilionea; Kwa usalama wa nchi yetu KATIBA MPYA haikwepeki.
13. Vuai Nahodha; Wananchi chonde MSILETE VURUGU NA KUANDAMANA kwani vilio vyenu kutaka KATIBA MPYA vinashughulikiwa.
14. Werema; Sasa serikali tumepata jibu sahihi hata bila ya Jopo la Wataalam au bila hata kupeleka popote hizo RASIMU SIFURI zenu za kutaka KATIBA MPYA.
Jibu lenyewe ambalo ni sahihi kabisa na kila mwananchi LAZIMA kuikubali ni kwamba 'WATANZANIA HAMUHITAJI KUANDIKA UPYA KATIBA BALI VIRAKA TU VICHACHE VINATOSHA.
15. Wanaharakati, Asasi za Kiraia, Vyama Vya Wafanyakazi, Vijana, Wana-JF, Vyama vya Siasa, Taasisi za Kidini na Vyuo Vikuu nchini nao wakasema; Saa ya Kuandikwa kwa KATIBA MPYA kwa njia Shirikishi kwa wananchi wote ni sasa.
16. Kesho au keshokutwa; ....
Kwa hayo maelezo yote yanayojikanganya kushoto na kulia sasa tushike lipi? MAFISADI watuambie ya kwamba sasa JIBU RASMI YA SERIKALI NI HILO ALILOLITOA WEREMA.
Na kama kweli ndilo jibu na msimamo rasmi wa serikali juu ya jambo hili la msingi na wa UMUHIMU WA PEKEE HASA KWETU VIJANA na walalahoi tuliowengi nchi hii basi nasi tunaomba kumshauri murua kwenu.
Kwa kuwa HAKI hua hauombwi wala kuletwa bila ya purukushani mivutano ya kujitakia MAFISADI, Saed Mwema tunakuomba ukaagize upesi MA-BOMU YA MACHOZI YA KUTOSHA kabisa na madai sasa yahamie uwanjani kama hata hoja yetu kule Bungeni ndilo hilo mnaelekea kusema ni kupoteza wakati!!!!