Mwanasheria mkuu wa Serikali:Hakuna haja ya kuwa na katiba mpya,tuboreshe iliyopo

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Mwanasheria mkuu wa serikali Werema amesema kuwa katiba ya sasa inabidi ifanyiwe marekebishi na siyo kuandikiwa kwa katiba mpya

chanzo TBC1 Habari saa 2:00 usiku
 
Mwanasheria mkuu wa serikali Werema amesema kuwa Tanzania inahitaji marekebisho tu katika katiba ya sasa na siyo kuandikiwa mpya.

Chanzo:TBC1 Habari saa 2:00 usiku
 
Mwanasheria Mkuu, Mhe Werema anayo haki ya kufurahisha nafsi yake lakini si kuamua juu ya hatima ya KATIBA ya nchi.

Huyu bwana anayo wajibu tu wa kuishauri serikali juu ya KATIBA ikishapatikana. Lakini pale KATIBA inapotafutwa, yeye kutoa juu ya HATIMA ya andiko hili ni to act ULTRAVIROUSLY bila ya ulazima. Hatujamsikia akizungumzia Mbunge anapopigwa na polisi, kwa nini adandie kazi si yake hapa??

Katiba si mali ya Werema, Katiba si Mali ya Kikwete na Mwinyi wala Katiba si mali ya Serikali.

Kama walivyowahi kusema Waheshimiwa Prof Lipumba, Dr Slaa, Duni Haji Duni, Wasomi kibao na Wanasheria waliotukuka, KATIBA ni mali ya Mtanzania wa kawaida. Lini akalirekebishe na kwa mtindo gani yote ni juu yake mwenyewe kuamua.

Mwanasheria Mkuu ni mwajiriwa wa KATIBA na hana msingi wa kumamulia mwajiri wake kitu gani akafanye juu ya KATIBA. Wapinga MABADILIKO YA KWELI nchini, hebu tukutane bungeni Dodoma.
 
Werema haikubali katiba mpya na alilizibitisha mnano mwezi wa tisa mwaka katika conference ya chuo Cha Ruaha baada ya our good Prf. Mbunda kupresent paper iliyochambua matatizo yaliyomo ndani ya katiba na kusisitiza kuwa tunahitaji katiba mpya, Werema alikua mwenyeki wa session hiyo na alicrash mawazo ya our good Prof. Mbunda kwa kusema watanzania tunakurupuka.
Werama ni mpinga maendeleo namba moja.
 
Werema anajidanganya maana katiba mpya itakuja hata kwa damu ya watanzania. Hivyo akae pembeni asubiri matokeo. Lakini katiba mpya ni lazima wala hatumuombi.
 
Mwanasheria mkuu wa serikali Werema akihojiwa baada ya sherehe ya kuapishwa CJ leo asema, tena kwa kujiamini: "Katiba Mpya Hapana ila Marekebish ya Katiba Ruksa".

Source: Taarifa ya habri ITV saa 2 usiku 27/12/2010

Hivi kuna mtu mmoja au watu fulani ndo wenye maamlaka ya kuruhusu mchakato wa katiba ya watanzania?? Nini maana ya hapana na Ruksa? Huyu Werema ndo mwenye hatima ya au tuwe na katiba mpya au siyo? Ni vipi hadi aseme neno Ruksa? Kwani katiba ni mali ya serikali au ya Watanzania?

Nionavyo mimi Werema hana cha kuzuia kuhusu katiba mpya endapo Watanzania (Nguvu ya umma) wakiamua wawe na katiba mpya. Ila nimekerwa mno na kauri ya Werema...

Great Thinkers mnasemaje juu ya hilo?

Bensonlifua92
 
Huyu naye ni fisadi tu,na inaonyesha ni jinsi gani akili yake isivyofanya kazi sawasawa.N.y.a.m*b*f...
 
Huyu naye ni fisadi tu,na inaonyesha ni jinsi gani akili yake isivyofanya kazi sawasawa.N.y.a.m*b*f...

Mh kichwa kinauma kwa kweli pumba zingine, ngoja nkaangalie kwanza mechi ya Arsenal na Chelsea kesho nitakuwa na kuchangia kuhusu huyu Wema sijui Werema
 
Mwanasheria mkuu wa serikali Werema akihojiwa baada ya sherehe ya kuapishwa CJ leo asema, tena kwa kujiamini: "Katiba Mpya Hapana ila Marekebish ya Katiba Ruksa".

Source: Taarifa ya habri ITV saa 2 usiku 27/12/2010

Hivi kuna mtu mmoja au watu fulani ndo wenye maamlaka ya kuruhusu mchakato wa katiba ya watanzania?? Nini maana ya hapana na Ruksa? Huyu Werema ndo mwenye hatima ya au tuwe na katiba mpya au siyo? Ni vipi hadi aseme neno Ruksa? Kwani katiba ni mali ya serikali au ya Watanzania?

Nionavyo mimi Werema hana cha kuzuia kuhusu katiba mpya endapo Watanzania (Nguvu ya umma) wakiamua wawe na katiba mpya. Ila nimekerwa mno na kauri ya Werema...

Great Thinkers mnasemaje juu ya hilo?

Bensonlifua92

Yeye kama nani hadi atuamulie Watanzania kwamba hakuna haja ya kuwa na katiba mpya bali tuendelee kuongeza viraka tu katika hii tuliyonayo? Hawa vingunge wengine wanasahau mipaka ya nyadhifa zao walizokabidhiwa na kudhani wana mamlaka makubwa ya kuamua kila kitu kwa niaba ya Watanzania bila hata kutushirikisha. Katiba mpya ni lazima ipatikane kabla ya 2015, majirani zetu Kenya wametuonyesha njia na sisi hatuna budi kufuata nyayo zao na kutosubiri mpaka tukatane mapanga ndiyo tuone umuhimu wa kuwa na katiba mpya.
 
Mwanasheria mkuu wa serikali Werema amesema kuwa Tanzania inahitaji marekebisho tu katika katiba ya sasa na siyo kuandikiwa mpya.

Chanzo:TBC1 Habari saa 2:00 usiku

Hilo ndilo jibu ambalo Watanzania tungelipata endapo tungekubali Mhe Kikwete angeweza kuteua Jopo la Wataala kuhusu Katiba kama ambavyo alivyowahi kuzungumzia hapo awali na 'Mtoto wa Mkulima'.

Wapenda mabadiliko wote sasa macho yetu yageukie Dodoma Bungeni. Waheshimiwa wabunge wapenda mabadili, bila kujali tofauti za itikadi tukawape jibu lao ving'ang'anizi wa katiba ya zamani kwa kauli moja na tupate KUIMARISHA ZAIDI UMOJA WETU KITAIFA huko.

Mheshimiwa Mnyika, fikisha hiyo hoja yetu bungeni na msaidiane na wabunge wote tuliowachagua kweli kwa kura zetu bila kuchakachua kufanikisha ndoto za wananchi kupata katiba mpya.
 
This is not only distasteful, but attempts to renege on the nation's obligation to have a an accountable and just government. It's saddening that the entire debate on the new constitution is now being hijjacked by self-serving individuals. Werema and his likes, should know that there is no need for him to try to generate panick and confusion as to whether a process of writing a new katiba is adopted, but let him just watch only that process and the motion is adopted, the reality is that his assertion is just a futility if the intention is to scuttle any ongoing attempts to have a new constitution.
 
Wanaume wa Tarime huwa hawataki kuwa challenged. Wana hulka ya kupadisha hasira bila kufuata mfumo unaoeleweka. Sasa na huyu naye anajiingiza kule kule kwa "wasomi" wa Tanzania na fikra zao zisizo lisaidia chochote Taifa hili.
 
Werema haikubali katiba mpya na alilizibitisha mnano mwezi wa tisa mwaka katika conference ya chuo Cha Ruaha baada ya our good Prf. Mbunda kupresent paper iliyochambua matatizo yaliyomo ndani ya katiba na kusisitiza kuwa tunahitaji katiba mpya, Werema alikua mwenyeki wa session hiyo na alicrash mawazo ya our good Prof. Mbunda kwa kusema watanzania tunakurupuka.
Werama ni mpinga maendeleo namba moja.

WEREMA AS 'CIVIL SERVANT' OF THE CONSTITUTION JUST LIKE PRESIDENT KIKWETE, MUST STOP OVER-STEPPING HIS CONSTITUTIONAL MANDATE

Kumbe huyu ndio aina ya MWANASHERIA MKUU tulionaye - CLOSED MINDED TYPE OF PERSON???

Nchi hii ni lini tutaanza KUWAHESHIMU WASOMI WETU NA MAONI YAO YA KITAALAM pindi wanapoto ushauri kwa jamii yetu kwa msingi na kadri taaluma yake inavyomeelekeza aseme??

Kwingineko maoni ya Maprofesa na wasomi wengineo huheshimika mno sawa sawa na maoni ya Viongozi wetu wa Imani mbali mbali katika jamii wanapozungumza. Lakini kwetu sisi ni sauti ya watawala tu ndio ya maana.

Werema, KATIBA ni mkataba kati yetu sisi wananchi na nyinyi watawala. Kwa bahati mbaya sana, mpaka sasa haturidhiki na utendaji wenu hata kidogo.

Sasa wewe kama mwajiriwa wetu KIKATIBA unapotuambia nini tufanye na mkataba tuliokuingiza nayo kazini, hivi kweli unachukua muda kusikiliza japo robo tu ya maneno yako mwenyewe???

Werema, STOP OVERSTEPPING your Constitutional mandate to question Wananchi's Resolve to Re-Write the Governance Blueprint.
 
Anaonekana ni mmoja wa watu wanaotaka kuendeshwa na matukio badala ya yeyekufanya matukio!
 
mamajusi waliiona Nyota ile mashariki, wakaifuata. Huyu hajui kusoma alama za nyakati na kuzifuata
 
Mwanasheria mkuu wa serikali Werema amesema kuwa Tanzania inahitaji marekebisho tu katika katiba ya sasa na siyo kuandikiwa mpya.

Chanzo:TBC1 Habari saa 2:00 usiku

Kama huu sasa ndio MSIMAMO RASMI WA SERIKALI YA MHE KIKWETE kuhusu swala la kupatikana kwa KATIBA MPYA nchini basi ushauri wetu moja kwa moja umuendee Saed Mwema akaagize upesi MA-BOMU ZAIDI YA KUTOA MACHOZI.

Tudhibitishieni hili kwa HUU NDIO MSIMAMO RASMI wa serikali hii iliojiweka yenyewe madarakani kupitia nguvu za Bank Accounts.
 
Hivi tunataka katiba mpya ambayo inamaelekezo gani mapya tofauti kabisa na yaliopo kenywe katiba ya sasa ukitoa matatizo ya nguvu za raisi na uchanganyaji wa mambo ya muungano?
 
Back
Top Bottom