Mwanasheria Mkuu wa Serikali aweka mapingamizi manne kesi kuhusu watuhumiwa uhujumu uchumi kunyimwa dhamana

mtapa wilson

Member
Jan 2, 2014
10
13
Mwanasheria mkuu wa serikali (AG) ameweka mapingamuzi manne dhidi ya kesi namba 35 ya mwaka 2019 iliyofunguliwa na Mwanasheria wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Paul Kisabo, ambaye anapinga watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kunyimwa dhamana.

Katika shauri hilo ambalo limefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es salaam, Mwanasheria Kisabo anapinga kifungu namba 148 (5) (d) (v) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho kinazuia watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kupewa dhamana, jambo ambalo analitaja kuwa ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Mnamo Februari 13, 2020 shauri hilo lilitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, ambapo upande wa mleta maombi unaowakilishwa na Wakili Daimu Halfani na Jeremiah Mtobesya walidai kutopokea majibu ya maombi yao kutoka upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali, lakini hata hivyo Mawakili wa serikali, Aboubakar Mrisho na Vivian Method waliieleza mahakama kuwa wamechelewa kujibu maombi hayo baada ya kuchelewa kupata baadhi ya taarifa, ambazo zingewezesha kujibu maombi hayo kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali nchini (DPP), na kudai kuwa taarifa hiyo waliipata baada ya siku 14 za kujibu maombi hayo.

Majaji watatu wanaosimamia kesi hiyo akiwemo Jaji Masoud, Jaji Magoiga na Jaji Juliana Masabo waliutaka upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali kujibu maombi hayo ndani ya siku saba kuanzia siku ya Februari 13, 2020 ambapo shauri hilo lilitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo.

Ikiwa jana (Februari 25, 2020) ni mara ya pili kesi hiyo inatajwa mahakamani hapo, kabla ya kujibu maombi hayo, upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali, ambao jana uliwakilishwa na Wakili wa serikali, Kalokola Stanley uliweka mapingamizi manne ikiwemo; kiapo cha mleta maombi kudaiwa kuwa na makosa yanayokiuka sheria ya mwenendo wa kesi za madai.

Aidha upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali ulidai kuwa aina kesi aliyoifungua mleta maombi (Paul Kisabo) ilishawahi kutolewa uamuzi huko nyuma.

Vilevile, Mwanasheria mkuu wa serikali alidai kuwa kesi ya mleta maombi inakiuka kifungu cha 3 na cha 4 cha Sheria ya BRADEA (Basic Rights and Duties Enforcement Act).

Kadhalika, upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali ulidai kuwa maombi ya mleta maombi hayakubaliki kisheria.

Kesi hiyo iliahirishwa jana Februari 25, 2020 mpaka Mei 13, 2020 ambapo itaitwa tena mahakamani hapo saa 7:30 mchana.

CHANZO: WATETEZI TV

IMG_20200226_123643_814.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi nyingi duniani zinafanya mabadiliko kesi zote ziwe na dhamana ila kesi za murder ina utata kidogo.Mtu kama anayo dhamana zaidi ya aliyotuhumiwa nayo plus ulimwengu wa sasa huwezi toroka popote duniani na usikamatwe,hatuoni shaka kwann wasipewe dhamana.

Hii ishu ya uhujumu uchumi imetumiwa vibaya hasa na wanasiasa pale wale wote wasio na chapa wanasukumizwa ndani kwanza kisha ushahidi wa kusuasua ndio unaanza kutafutwa ambapo mtuhumiwa lengo akae tu ndani hata miaka 5 eti ananyooshwa utadhani amekuwa ni nguo then anakuja kutolewa na DPP either kwa kununua Uhuru wake au shinikizo la kunyimwa mikopo au misaada na mabeberu, ndipo utasikia DPP akisema hana haja ya kuendelea na shauri hilo.Hali walio na chapa wao sheria hii haiwahusu hata wakitenda the same.

Lengo kuu ili mtuhumiwa avurugikiwe na maisha yaani aanze upya kama ni mali ifilisike kwa kukosa usimamizi,familia isambaratike kabisa.Tuna wanasheria tena wanajiita wasomi lakini hawana uwezo wa kuandaa thesis za kupunguza idadi ya mahabusu magerezani.Tufike wakati tuwe kama watu walioelimika tujitofautishe na wasioelimika ukimnyoosha mwenzie wewe umefaidika na nini.
 
Tetea sheria kandamizi ukiwa huru ili siku usipokuwa huru ikufae.Kuna kiongozi aliwahitunga sheria ya kuwakandamiza wengine akiwa kwenye system akidhani atakuwa salama na alipotoka kwenye system akawa ndo wa kwanza kuhukumiwa na sheria aliyoisaini.Makamba aliwahi sema atawabatiza kwa moto akidhani ubatizo hautomhusu,Mungu fundi bwana akabatizwa yeye na mwanae leo wamelowa kama wamemwagiwa maji ya mchele.Na hizi sheria za uhujumu uchumi mbeleni huko zitakuja kuwabatiza hao wanaowabatiza uhujumu uchumi wenzao sababu kwa sasa wameshikilia Uhuru wa watu hali nao wanaishi nyumba za vioo,ni heri waziboreshe jela sasa wangali wana nafasi wakiwa kama wafungwa watarajiwa ili pawafae watakapoingia.
Pinga sheria kandamizi sasa ukiwa huru ili ikufae kesho ukiwa mfungwa jela ni yako na mie haina mwenyewe sawa na hospital.
 
Kwanini mahakama huisikiliza zaidi serikali badala ya kuwa katikati kwenye sheria, kila Mara serikali hupewa muda lakini upande wa wananchi hunyimwa muda.
 
Tetea sheria kandamizi ukiwa huru ili siku usipokuwa huru ikufae.Kuna kiongozi aliwahitunga sheria ya kuwakandamiza wengine akiwa kwenye system akidhani atakuwa salama na alipotoka kwenye system akawa ndo wa kwanza kuhukumiwa na sheria aliyoisaini.Makamba aliwahi sema atawabatiza kwa moto akidhani ubatizo hautomhusu,Mungu fundi bwana akabatizwa yeye na mwanae leo wamelowa kama wamemwagiwa maji ya mchele.Na hizi sheria za uhujumu uchumi mbeleni huko zitakuja kuwabatiza hao wanaowabatiza uhujumu uchumi wenzao sababu kwa sasa wameshikilia Uhuru wa watu hali nao wanaishi nyumba za vioo,ni heri waziboreshe jela sasa wangali wana nafasi wakiwa kama wafungwa watarajiwa ili pawafae watakapoingia.
Pinga sheria kandamizi sasa ukiwa huru ili ikufae kesho ukiwa mfungwa jela ni yako na mie haina mwenyewe sawa na hospital.

Wao kwa wakati huo wanadhani hawawezi kushtakiwa kwa makosa hayo wanasahau ya Mungu ni mengi.
 
Tetea sheria kandamizi ukiwa huru ili siku usipokuwa huru ikufae.Kuna kiongozi aliwahitunga sheria ya kuwakandamiza wengine akiwa kwenye system akidhani atakuwa salama na alipotoka kwenye system akawa ndo wa kwanza kuhukumiwa na sheria aliyoisaini.Makamba aliwahi sema atawabatiza kwa moto akidhani ubatizo hautomhusu,Mungu fundi bwana akabatizwa yeye na mwanae leo wamelowa kama wamemwagiwa maji ya mchele.Na hizi sheria za uhujumu uchumi mbeleni huko zitakuja kuwabatiza hao wanaowabatiza uhujumu uchumi wenzao sababu kwa sasa wameshikilia Uhuru wa watu hali nao wanaishi nyumba za vioo,ni heri waziboreshe jela sasa wangali wana nafasi wakiwa kama wafungwa watarajiwa ili pawafae watakapoingia.
Pinga sheria kandamizi sasa ukiwa huru ili ikufae kesho ukiwa mfungwa jela ni yako na mie haina mwenyewe sawa na hospital.

Umesema vyema sana mkuu
 
Mbona Lugola anatuhumiwa kwa uhujumu uchumi lakini yuko nje

Mkuu ,Sheria ni ile ile /DPP ni yule yule /Jeshi la Polis ni lilelie na Nchi ni ile ile ,lakini Matokeo yanakuwa/yanaonekana/yanakuwa tofauti kwa Kosa lile lile.

Ajabu ya Waafrika ndio hii ,Roho mbaya kabisa sisi.
 
Nchi nyingi duniani zinafanya mabadiliko kesi zote ziwe na dhamana ila kesi za murder ina utata kidogo.Mtu kama anayo dhamana zaidi ya aliyotuhumiwa nayo plus ulimwengu wa sasa huwezi toroka popote duniani na usikamatwe,hatuoni shaka kwann wasipewe dhamana.

Hii ishu ya uhujumu uchumi imetumiwa vibaya hasa na wanasiasa pale wale wote wasio na chapa wanasukumizwa ndani kwanza kisha ushahidi wa kusuasua ndio unaanza kutafutwa ambapo mtuhumiwa lengo akae tu ndani hata miaka 5 eti ananyooshwa utadhani amekuwa ni nguo then anakuja kutolewa na DPP either kwa kununua Uhuru wake au shinikizo la kunyimwa mikopo au misaada na mabeberu, ndipo utasikia DPP akisema hana haja ya kuendelea na shauri hilo.Hali walio na chapa wao sheria hii haiwahusu hata wakitenda the same.

Lengo kuu ili mtuhumiwa avurugikiwe na maisha yaani aanze upya kama ni mali ifilisike kwa kukosa usimamizi,familia isambaratike kabisa.Tuna wanasheria tena wanajiita wasomi lakini hawana uwezo wa kuandaa thesis za kupunguza idadi ya mahabusu magerezani.Tufike wakati tuwe kama watu walioelimika tujitofautishe na wasioelimika ukimnyoosha mwenzie wewe umefaidika na nini.
Yaani kuielewa hii serikali ya Ccm ina hitaji elimu ya ziada. Juzi tulimsikia jaji mkuu akilalamika sheria kali na kandamizi zinazo wanyima nguvu mahakimu na majaji kutoa dhamana kwenye kesi ambazo wao wanaona zina dhaminika.
Ametokea raua mwema ana omba hizo sheria zifutwe ana tokea mtu huko huko serikakini kwa jaji mkuu ana pinga. Tuna shindwa kuwaelewa wasomi wa awamu hii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tunatakiwa kujua,uwezi kumwongoza mwafrica kama unatavyomwongoza mzungu au binadamu mwingine..mwafrica anahitaji force kubwa kujiendeleza..ndo maana tulichapwa mijeredi kujenga reli kwa faida yetu..Period
Lkn haki za binadamu lzm zilindwe
 
Back
Top Bottom