mtapa wilson
Member
- Jan 2, 2014
- 10
- 13
Mwanasheria mkuu wa serikali (AG) ameweka mapingamuzi manne dhidi ya kesi namba 35 ya mwaka 2019 iliyofunguliwa na Mwanasheria wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Paul Kisabo, ambaye anapinga watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kunyimwa dhamana.
Katika shauri hilo ambalo limefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es salaam, Mwanasheria Kisabo anapinga kifungu namba 148 (5) (d) (v) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho kinazuia watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kupewa dhamana, jambo ambalo analitaja kuwa ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Mnamo Februari 13, 2020 shauri hilo lilitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, ambapo upande wa mleta maombi unaowakilishwa na Wakili Daimu Halfani na Jeremiah Mtobesya walidai kutopokea majibu ya maombi yao kutoka upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali, lakini hata hivyo Mawakili wa serikali, Aboubakar Mrisho na Vivian Method waliieleza mahakama kuwa wamechelewa kujibu maombi hayo baada ya kuchelewa kupata baadhi ya taarifa, ambazo zingewezesha kujibu maombi hayo kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali nchini (DPP), na kudai kuwa taarifa hiyo waliipata baada ya siku 14 za kujibu maombi hayo.
Majaji watatu wanaosimamia kesi hiyo akiwemo Jaji Masoud, Jaji Magoiga na Jaji Juliana Masabo waliutaka upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali kujibu maombi hayo ndani ya siku saba kuanzia siku ya Februari 13, 2020 ambapo shauri hilo lilitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo.
Ikiwa jana (Februari 25, 2020) ni mara ya pili kesi hiyo inatajwa mahakamani hapo, kabla ya kujibu maombi hayo, upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali, ambao jana uliwakilishwa na Wakili wa serikali, Kalokola Stanley uliweka mapingamizi manne ikiwemo; kiapo cha mleta maombi kudaiwa kuwa na makosa yanayokiuka sheria ya mwenendo wa kesi za madai.
Aidha upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali ulidai kuwa aina kesi aliyoifungua mleta maombi (Paul Kisabo) ilishawahi kutolewa uamuzi huko nyuma.
Vilevile, Mwanasheria mkuu wa serikali alidai kuwa kesi ya mleta maombi inakiuka kifungu cha 3 na cha 4 cha Sheria ya BRADEA (Basic Rights and Duties Enforcement Act).
Kadhalika, upande wa Mwanasheria mkuu wa serikali ulidai kuwa maombi ya mleta maombi hayakubaliki kisheria.
Kesi hiyo iliahirishwa jana Februari 25, 2020 mpaka Mei 13, 2020 ambapo itaitwa tena mahakamani hapo saa 7:30 mchana.
CHANZO: WATETEZI TV
Sent using Jamii Forums mobile app