Mwanasheria mkuu, Mabadiliko ya mafao ni kwa PPF pekee, iweje isiwe kwa NSSF? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanasheria mkuu, Mabadiliko ya mafao ni kwa PPF pekee, iweje isiwe kwa NSSF?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Oct 26, 2012.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Mwanasheria mkuu wa serikali(AG) Jaji Werema amewasilisha muswada wa marekebisho ya mafao ya kujitoa katika ofisi ndogo ya bunge jijini Dar es Salaam ukiwa na maana utajadiliwa kwenye mkutano wa bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo tarehe 30 November,

  Kwa mujibu wa muswada huo wa AG sehemu ya sita inapendekeza marekebisho ya sheria ya Pensheni ya mashirika ya umma PPF na kuwaacha NSSF kubaki ilivyo wakati inajulikana kuwa 85% ya wanachama wa NSSF ni sekta binasfi.

  Sura ya 372 ya muswada huo kifungu kipya cha 44 kutoa fursa kwa mfuko huo wa PPF kutoa fao la kujitoa kwa manachama wake.
  Kwa maana nyingine ni kuwa wanachama wa mifuko mingine kama NSSF itaendelea kutumia sheria ambayo imelalamikiwa na wafanyakazi nchi nzima.

  Chanzo: Gazeti la nipashe.


  Swali: Iweje serikali ilete muswada wa kurekebisha mfuko wa mashirika ya umma PPF ambao wanachama wake wana uhakika na ajira zao huku ikiuacha mfuko wa NSSF ambao ni asilimia kubwa ya wanachama wake ni sekta binafsi ambao hawana uhakika wa ajira zao??????
   
 2. Jangakuu

  Jangakuu JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jamani hii nchi inakuelekea kubaya. watakuwa hawajasolve chochote bcoz asilimia kubwa ya watu wapo NSSF. watu ambao wapo PPF asilimia kubwa ni wafanyakazi wa serikali ambao wana ajira za uhakika.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wabadilishe NSSF halafu watoe wapi hela za kufanikisha miradi ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi 2015? NSSFkwa sasa haina tofauti na WAMA. Uwekezaji wake ni wa kisiasa zaidi - wakubwa wakitaka kufanya kitu simu inapigwa NSSF, sasa mfuko unayumba, at the same time kuna 2015!

  Haya ni madharau kwa watanzania - kwamba hawatagundua huu usanii wa kitoto!
   
 4. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mimi mfanyakazi wa sekta binafsi nina hasira sana na hii serikali kandamizi.

  Hii serikali ya mafisadi sasa wanatudharau sana wafanyakazi wa sekta binafsi. Hii ni dharau saaanaaaa.

  Tumekuwa wapole saaana, Why like this. jamaniii

  Pia sekta binafsi imeitia serikali mfukoni maana haya makampuni binafsi yanachangia kampeni za chama cha mafisadi.

  Jamani wafanyakazi, sasa tuanze mkakati, vinginevyo tunanyongewa mbaaali na hawa mafisadi sasa.

  Sasa tuseme basi na tuandamane.
   
 5. M

  Mndokanyi JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama serikali inaweza kulazimisha mambo kama haya,kweli imekosa utashi wa kusikiliza wananchi wake.Tanzania tuna watawala na sio viongozi,kwa sababu kiongozi anakuwa na busara,na huwapa matumaini anaowaongoza.Wafanyakazi tusibiri 2015 tuiingize chama mbadala,ndo kitatusikiliza.
   
 6. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,275
  Likes Received: 2,951
  Trophy Points: 280
  Wanaacha NSSF kwenye tatizo wanakwenda PPF ambako hakuna tatizo,unadhani 2015 ccm ndiyo imeshaji-lock.Yaani watu wanaichukia kwakushindwa hata mambo madogo kama haya yanayogusa maslahi ya walalahoi.
   
 7. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Sijaona mantiki ya kubadili sheria kwa PPF huku ikiwaacha wafanyakazi kama wa migodini wakikandamizwa,,,wafanyakazi wa migodini wote wako NSSF,,,kila kukicha wafanyakazi wa migodini wanafukuzwa na ndoo wanachama wa NSSF,,iweje NSSF iachwe itumie sheria ya miaka 60??,,,kuna nini hapo???
   
 8. U

  UNO Senior Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huko ndiko kwenye makato manono. Wanakochota pesa na hakuna wa kuuliza. We unafikiri 2015 watoe wapi hela? Na EPA ni kama haipo. NSSF inadai serikali zaidi ya bilioni 200; zimekwenda wapi na wanategemea kulipa lini???????
   
 9. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Simpendi werema! Anakuwa kada! Sijawahi kuona mkulya wa hivo.
   
 10. V

  Visionmark Senior Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania hatuna serikali bali tuna 'Genge la wahuni' na ambalo pasipo haya wala soni linaongoza nchi kihuni! Niimani yangu kubwa kwamba endapo Tanzania tungelikuwa na serikali na sio hilo 'Genge la wahuni', kitu cha kwanza kabisa ambacho serikali hiyo ingelifanya ni kukaa na wadau wote wa mifuko ya jamii ili kupata maoni yao kwanza kabla ya hayo marekebisho yanayotaka kufanywa na hili 'Genge la wahuni'. Sekta binafsi hapa nchini HAIAMINIKI HATA KIDOGO halfu leo MIJITU INAKURUPUKA TU na MAWAZO MFU!
   
 11. V

  Visionmark Senior Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania hatuna serikali bali tuna 'Genge la wahuni' na ambalo pasipo haya wala soni linaongoza nchi kihuni! Niimani yangu kubwa kwamba endapo Tanzania tungelikuwa na serikali na sio hilo 'Genge la wahuni', kitu cha kwanza kabisa ambacho serikali hiyo ingelifanya ni kukaa na wadau wote wa mifuko ya jamii ili kupata maoni yao kwanza kabla ya hayo marekebisho yanayotaka kufanywa na hili 'Genge la wahuni'. Sekta binafsi hapa nchini HAIAMINIKI HATA KIDOGO halfu leo MIJITU INAKURUPUKA TU na MAWAZO MFU!
   
 12. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  haina mantiki kufanya ubaguzi wa wanachama wa mifuko hiyo. ni bora basi waseme kuchangia mifuko ya jamii ni hiari ya mfanyakazi, na pia iwe hiari kwa mfanyakazi kuchagua mfuko wa kujiunga nao. Vinginevyo ni usanii tu tunafanyiwa hapa, ni wizi mtupu, uwekezaji usio na tija kwa wanachama, uhakika wa kuishi miaka 60 nani anao??
   
 13. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,371
  Likes Received: 8,462
  Trophy Points: 280
  *Utawanufaisha wanachama wa mfuko mmoja

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema
  Muswada wa marekebisho ya sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa Kumi wa Bunge, umewaacha solemba wanachama wa mifuko mingine baada ya marekebisho hayo kurejesha fao hilo kwa mfuko mmoja pekee.

  Sheria ya mafao ilipitishwa katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu na kuwazuia wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuruhusiwa kuchukua mafao yao hadi wafikishe umri kati ya miaka 55 na 60.

  Baada ya wanachama wa mifuko hiyo na wadau wengine wakiwamo wabunge kuipinga sheria hiyo, serikali iliahidi kuwa itaifanyia marekebisho na kuwasilisha muswada kwa hati ya dharura.

  Tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, amekwishawasilisha muswada huo katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam, ikiwa na maana kuwa utajadiliwa kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

  Muswada huo unakusudia kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali.

  Kwa mujibu wa muswada huo, ambao NIPASHE imeuona, sehemu ya sita inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), sura ya 372 kwa kuongeza kifungu kipya cha 44 ili kutoa fursa kwa mfuko huo kutoa fao la kujitoa kwa mwanachama wake.

  Kwa maana nyingine ni kwamba wanachama wa mifuko mingine kama NSSF itaendelea kutumia sheria ambayo imelalamikiwa na wafanyakazi.

  HOJA YA JAFO YAZIKWA

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kisarawe (CCM), Seleman Jafo, ambaye wakati wa mkutano wa Bunge wa Bajeti, alitaka kuwasilisha muswada binafsi, alisema amepata barua kutoka kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, ikimtaarifu kwamba, serikali itawasilisha muswada wa marekebisho hayo, hivyo hana sababu ya kuandika muswada mpya.

  Jafo alisema kwa kuwa alikwishawasilisha hoja ya kutaka marekebisho kwenye sheria ya hifadhi ya jamii, Bunge lilimweleza kwamba ni fursa kwa serikali au Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii; hivyo serikali imeazimia kuiwasilisha kwenye mkutano ujao.

  “Lakini kwa hali hii ni kwamba serikali haitatatua matatizo ya msingi ya hoja yangu, muswada unatakiwa uguse mifuko yote kwa sababu malalamiko ni ya wafanyakazi wote,” alisema.

  SUGU AIONYA SERIKALI

  Kwa upande wake, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, aliionya serikali kutochezea wafanyakazi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhamasisha fujo.

  Alisema ni vyema marekebisho yatakayowasilishwa bungeni yakarejesha fao la kujitoa kwa mifuko yote kwa kuwa wafanyakazi wengi hawana usalama kazini.

  “Tunajua faida ya pensheni uzeeni kwa sababu ni msaada mtu anapostaafu, lakini kwa mfumo wa nchi yetu ambayo wafanyakazi hawana usalama wa kazi haiwezi kufanyakazi ipasavyo,” alisema.

  Sugu alisema wafanyakazi kama wa migodini au hostelini wanafanyakazi katika mazingira magumu na wanaweza kuachishwa kazi wakati wowote hivyo fao la kujitoa litawasaidia.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, alisema fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii halimo katika sheria za kimataifa.

  Dk. Dau, alisema hayo alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) katika kikao kati ya kamati hiyo na bodi na menejimenti ya shirika hilo, katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema pia ni Tanzania Bara pekee ndiko ambako kuna fao la kujitoa katika mifuko hiyo, lakini katika nchi za Kenya, Uganda, duniani kote, hata Zanzibar, suala hilo halipo.

  Hata hivyo, alisema mwanachama wa NSSF anapoamua kujitoa, anaupunguzia Mfuko mzigo wa kumtunzia pensheni yake ya uzeeni, badala yake na kujiumiza mwenyewe.

  Shinikizo la kutaka serikali kuirekebisha sheria hiyo ili wanachama wa mifuko walipwa mafao wakati wanapoacha kazi, liliilazimisha serikali kukubali yaishe na kuahidi kuwasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2012.

  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, aliliambia Bunge la bajati kwamba kabla ya kuwasilishwa, muswada huo utapelekwa kwa wadau ili watoe maoni na pia Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) itatoa elimu kuhusu fao la kujitoa.

  Hata hivyo, alisema wapo baadhi ya watu waliotafsiri kuwa kusitishwa kwa fao la kujitoa kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imefilisika kwa kuwa imewekeza kwenye miradi mibaya, jambo alilosema sio la kweli.

  Kabaka alisema kuwa mifuko hiyo haina hali mbaya kifedha wala haijafilisika na kwamba kuzuia fao la kujitoa ni utekelezaji wa sheria.

  Waziri Kabaka alisema mchakato wa kuwasilisha muswada huo utaanza mara moja kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

  Kabla ya kauli ya Kabaka, Bunge lilipitisha Azimio lililowasilishwa na Jafo, la kuletwa bungeni muswada wa dharura wa marekebisho ya Sheria Na. 5 ya mwaka 2012 inayozungumzia marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ndani yake inaelezea kuzuiwa kwa fao la kujitoa kwa wafanyakazi.

  Kutokana na mapendekezo ya muswada huo kutowatuhusu wanachama wa mifumo kingine kuchukua mafao kabla ya miaka 55 au 60, wanachama hao huenda wakashinikiza kwa njia za maadamano na migomo.

  Aidha, upo uwezekano wa kuzuka mjadala mkali bungeni kwa kuwa na wabunge nao ni wanachama wa mifuko hiyo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 14. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,320
  Likes Received: 1,495
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kuwa na hasira tu hakutoshi, unaonaje kama tukishirikia na wale jamaa wa migodini kuihenyesha serikali, kama niko sahihi nadhani hata hili sakata lilianzia kwao na serikali iaktia adabu, wengine pia tuwaunge mkono, vinginevyo itakula kwetu, chezea Kikwete weyee, yeye anajua kutumia tu na sio kutafuta!
   
 15. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mazindu Msambule, ni kweli hasira tu hazitoshi. Inatakiwa mkakati.

  Inatakiwa tupate jinsi ya kujiunga na wale wa Migodini. Natumaini wale wa migodini watatupa mwongozo na Hamasa jinsi ya kuandaa maandamano.

  Tutumiane message sms kwa wafanyakazi wote, halafu kila mfanyakazi akiwa na taarifa sahihi on what is going on, then ni rahisi kujipanga. Wafanyakazi wengi hawajui, sio wote wanapita hapa JF.

  Sasa who to start sms?
   
 16. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Uuuwiiiiiiii, Uwiiiiii weziiiiiii

  MIGOMO NA MAANDAMANOO. TANZANIA LAZIMA SASA TUSEME BAASI. UVUMILIVU NA WOGA BASI.

  HAKUNA WA KUZUIA MAANDAMANO WAFANYAKAZI NI WENGI SANA, POLISI NA JWTZ NI WATOTO WETU, WAJOMBA ZETU, DADA ZETU, KAKA ZETU. ILA HAO VIBARAKA WACHACHE TUTAWADHIBITI TUKIUNGANA TUNAWEZA.

  TUTASHUSHA HAYO MAGHOROFA ya kifisadi, udom, machingwa complex, daraja la kigamboni. HAYO NI MIRADI YA KISIASA NA KIFISADI KUINUFAISHA SERIKALI YA CCM.

  Sasa tuanze kuhamasishana na kutaarifiana, tujiandae sasa. Mtumie huu ujumbe mfanyakazi mwenzako.

  "ndugu yangu mfanyakazi, akiba yako ya NSSF inachezewa na mafisadi, je wewe una uhakika gani na ajira yako? Mshahara wako unakutosha ama unanyonywa!!! Je ukiacha kazi ama ukiachishwa utaishiji ili ufike miaka 55? Una akiba ya kutosha kujikimu kusomesha ana kulisha familia? Una uhakika wa kuishi hadi miaka 55? Majibu unayo, jiandae na acha woga. tetea haki yako. uwe tayari kwa maandamano yatakatoitishwa na wanaharakati ama mpango mzima"
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwenye website ya PPF, kuhusu benefits wanasema hivi

  Benefits to Members
  PPF offers seven different types of benefits to its members under the traditional scheme.
  Each type of benefit is granted to member upon such member ceasing employment and other qualifying condition related to each benefit. General Qualifying conditions are Age of Retirement, Period of Contribution and Reason of Ceasing employmenT


  Kwa maelezo hayo nadhani ukimaliza mkataba wa ajira unapewa chako, nipeni ufafanuzi zaidi
   
 18. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuhusu withdrawal benefits PPF wanasema hivi

  WITHDRAWAL BENEFIT
  Qualifying condition
  Where a member ceases employment through summary dismissal or termination.
  Mode of granting withdrawal benefit
  i) Granted as Lump sum immediately on ceasing employment.
  Documents required
  � Benefit Claim duly filled by the employer; (See Page 25)
  � Confirmation from the employer that the member has been dismissed or terminated from employment;
  � Two passport-size photographs of the member.

  Hayo marekebisho ya sheria yanahusu nini sasa? Au kilichopo kwenye website ni utapeli?
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,599
  Trophy Points: 280
  Hawa wana cheza na akili na muda wetu.wanataka wapeleke nusu nusu ili ikataliwe waseme wataipeleka tena mwakani April kikao kiajcho hapo wana poteza muda ili kukusanya kusanya ili angalau iwe stable kabla uchaguzi,then waachie!maana wanajua watakosa kura zoote za wafanyakazi na ndugu zao tegemezi!maana wakipewa 2yrs kubana mifuko yote itarudi kuwa stable.
   
 20. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  The Fund is the first contributory pension fund in the country operating under defined benefit system. PPF provides social security coverage to all employees in private companies, Parastatal organizations and public institutions. Its coverage has been extended to self employed as well as labour force in the informal sector. Initially it covers employees of parastatal organizations and those in private companies were registered but with the consent of Minister of Finance. However the legal provision requiring the Minister’s consent was removed giving the Fund’s mandate to widen up coverage to all employees including those on contracts following amendment of its Act (Parastatal Pensions Amendment Act No.25 of 2001) passed by the National Assembly in 2001.
   
Loading...