Mwanasheria mkuu kuwa mwanachama wa CCM ni sahihi?

Kusema kweli sijui sheria wala kanuni za kuwa jaji wa mahakama kuu. Maelezo yangu ni ya hisia binafsi, nikizingatia professionalism ambapo mbali na elimu, mtu anatakiwa awe mkweli, mwadilifu na bila ya upendeleo katika maamuzi namatendo yake. Hata kama mtu hana chama (rasmi) lakini ikiwa katika matendo yake anapendelea chama fulani, huyo nafasi hiyo haimstahiki kama ambavyo Werema anatumia nafasi ya umma kwa misingi ya chama kwanza kuliko wajibu wake kwa umma, atakuwa amepotea na hatufai.

Ndugu zangu mtaumiza vichwa bure kwa kutumia nguvu nyingi kufikiria haya mambo yanayofanywa na wateule hawa katika serikali yetu. Nchi hii tuna watu wazuri sana ambao ni wasomi na wana uzalendo wa hali ya juu katika kulitumikia taifa hili; utajiuliza kwa nini hawakuteuliwa hao? Waliteuliwa hawa tulionao ili wafate na watekeleze matakwa ya waliowateua, iwe kwa kuvunja sheria, kwenda kinyume na katiba, kuongea pumba, nk. Ilimradi kile ambacho kinatakiwa na waliowateua kinafuatwa na kutekelezwa, haijalishi kitaigarim nchi au maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom