Mwanasheria mkuu kuwa mwanachama wa CCM ni sahihi?

DOMA

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
944
365
Kwenye Cv ya mwanasheria mkuu iliyopo kwenye kumbukumbu za bunge inaonyesha kwamba mwanasheria mkuu jaji Werema ni mwanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) sasa sijajua hivi hii ni sahihi kwa mwanasheria mkuu kuwa na chama cha siasa?
 
Apo ata mimi nimeshindwa kupaelewa kwenye ile c.v yake,wewe unategemea refa anapokua mshabiki wa timu moja kati ya mbili anazochezesha ataitendea hii nyingine haki kweli?tanzania tunahitaji reforms nyingi sn ktk mfumo wetu wa utawala
 
Huyu mzee mie nilishamtoa kwenye list yangu ya watu wa maana ,pale Tundu Lissu alipombana kuhusiana na yeye kukubaliana kuwa ruhusu wakuu wa mikoa na wilaya kuingia kwenye kamati za nidhamu za mahakama.Hata Pinda alikataa mpaka pale spika alipomuuliza mara mbilimbili.Ni mtu ambaye ataingia kwenye rekodi ya kutufanyia maamuzi ya hovyo ya kisheria.
 
Bila kuwa mwanachama wa CCM nani ampe hiyo nafasi, si mnamshuhudia anavyotoa pumba wakati anavyosema Prof. Shivji ambaye ni mwalimu wake hajui lolote kuhusu katiba? Hicho ni kigezo cha kutumwa ki-chama kusema hayo lakini pia LLM yake ni online vile! AIBU KWAKE
 
Kwenye Cv ya mwanasheria mkuu iliyopo kwenye kumbukumbu za bunge inaonyesha kwamba mwanasheria mkuu jaji Werema ni mwanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) sasa sijajua hivi hii ni sahihi kwa mwanasheria mkuu kuwa na chama cha siasa?

Inawezekana kwa TANZANIA PEKEEE!!!:whistle::confused2:
 
Watz wote wanatakiwa wajue si halali kuwa na mwanasheria wa serikali anayetoka ktk chama fulani! kama alivyo Werema ambaye ni mwanaCCM! Imefika wakati wa kutoa maoni ktk tume kwenye mchakato wa kupata katiba mpya, kuhusiana na hili.
 
Mimi sidhani kama kuwa mwanachama wa chama gani kunamfanya mtu akose sifa za kutumikia chombo cha umma. Baadaye tutaangalia anatoka dini gani, mkoa au kanda gani au anapendelea timu gani. Muhimu ni kuwa mara tu anapokabidhiwa dhamana ya kuutumikia umma, anawacha ushabiki wake na kutenda majukumu yake kwa haki.
 
Kwenye Cv ya mwanasheria mkuu iliyopo kwenye kumbukumbu za bunge inaonyesha kwamba mwanasheria mkuu jaji Werema ni mwanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) sasa sijajua hivi hii ni sahihi kwa mwanasheria mkuu kuwa na chama cha siasa?
Katiba mpya inatakiwa i omit hii kitu kwa kupunguza madaraka ya mkulu kwanza na kuweka conditions za namna nzuri ambayo nchi itapata mwanasheria mkuu, mabalozi na wakuu wa taasisi zingine mbalimbali zinazoendeshwa na kodi za wananchi, si mbaya tukiwaiga wakenya walivyopata viongozi wa tume ya uchaguzi, interview ilifanyika na jopo la wataalam na ilikuwa live kwenye television and the best were selected and not the well known!
 
Bila kuwa mwanachama wa CCM nani ampe hiyo nafasi, si mnamshuhudia anavyotoa pumba wakati anavyosema Prof. Shivji ambaye ni mwalimu wake hajui lolote kuhusu katiba? Hicho ni kigezo cha kutumwa ki-chama kusema hayo lakini pia LLM yake ni online vile! AIBU KWAKE
Sikujua kama jamaa ni mpuuzi kiasi hicho. Kumdharau mwalimu aliyekupa maarifa?! Ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu.
 
Kwenye Cv ya mwanasheria mkuu iliyopo kwenye kumbukumbu za bunge inaonyesha kwamba mwanasheria mkuu jaji Werema ni mwanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) sasa sijajua hivi hii ni sahihi kwa mwanasheria mkuu kuwa na chama cha siasa?

Kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anayo haki ya kuwa mfuasi wa chama chochote cha siasa. Je Mwanasheria wa serikali asiwe mwanachama wa chama chochote? au atoke chama cha upinzani?
Mawazo mgando hayo. Hakuna sehemu inayotamka kuwa kiongozi wa serikali asiwe mwanachama wa chama cha sisa.
Unafikiri wabunge wanatawala wananchi ambao wanatoka vyama vyao pekee? kama si hivyo basi ingekuwepo sheria inayosema wabunge na wasiwe vyma kwa sababu wanaongoza watu ambao siyo wafuasi wa vyama vyao pekee.
 
Chuo chenyewe ni Fake unaweza pata digrii yako ndani ya 24 hrs pochi lako tu

Bila kuwa mwanachama wa CCM nani ampe hiyo nafasi, si mnamshuhudia anavyotoa pumba wakati anavyosema Prof. Shivji ambaye ni mwalimu wake hajui lolote kuhusu katiba? Hicho ni kigezo cha kutumwa ki-chama kusema hayo lakini pia LLM yake ni online vile! AIBU KWAKE
 
Kwenye Cv ya mwanasheria mkuu iliyopo kwenye kumbukumbu za bunge inaonyesha kwamba mwanasheria mkuu jaji Werema ni mwanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) sasa sijajua hivi hii ni sahihi kwa mwanasheria mkuu kuwa na chama cha siasa?

Nadhani wengi mnatishwa na hilo jina "mwanasheria mkuu", all in all hicho ni cheo cha kisiasa na ni kwa chama kinachotawala iwe Marekani, Australia, Belgium au Zimbabwe. Ndio maana kila chama kikichukua madaraka wanakuja na mwanasheria mkuu wao. Na si ajabu huyo Werema kuwa au kuwahi kuwa CCM. Tatizo tu ni pale ambapo maslahi ya chama yakiwekwa mbele kuliko yale ya Taifa and that is purely the bongo way.
 
Mimi sidhani kama kuwa mwanachama wa chama gani kunamfanya mtu akose sifa za kutumikia chombo cha umma. Baadaye tutaangalia anatoka dini gani, mkoa au kanda gani au anapendelea timu gani. Muhimu ni kuwa mara tu anapokabidhiwa dhamana ya kuutumikia umma, anawacha ushabiki wake na kutenda majukumu yake kwa haki.

kumbuka alikuwa jaji wa mahakama kuu kabla ya kuwa appointed katika nafasi ya sasa, kwa hiyo inaruhusiwa jaji wa mahakama kuwa na chama?
 
Kuhusu Werema, yote mia, jana alinifurahisha sana alipokuwa anawasilisha, alianza kwa vijembe kwa Lisu, bla bla bla!, lakini akajikuta najipa somo yeye mwenyewe na kujikuta anakubalina na alichokuwa amesema Lisu, kali zaidi Muda wa kuchangia ukawa umekwisha. Hao ndo wasomi wetu wa sheria. yaani kelele zote zile hata yeye anaona kitendawili cha muungano wetu. where is Tanganyika? nobody knows.

Kwa ufupi Werema ni janga la kitaifa.
 
hii nchi utakuta mkuu wa majeshi, wa polisi, usalama wa taifa, majaji na mahakimu zetu wote ni wanachama wa ccm sasa hapo jiulize kama wewe ni mwanachama wa upinzani utapata haki yoyote kweli?
 
kumbuka alikuwa jaji wa mahakama kuu kabla ya kuwa appointed katika nafasi ya sasa, kwa hiyo inaruhusiwa jaji wa mahakama kuwa na chama?
Kusema kweli sijui sheria wala kanuni za kuwa jaji wa mahakama kuu. Maelezo yangu ni ya hisia binafsi, nikizingatia professionalism ambapo mbali na elimu, mtu anatakiwa awe mkweli, mwadilifu na bila ya upendeleo katika maamuzi namatendo yake. Hata kama mtu hana chama (rasmi) lakini ikiwa katika matendo yake anapendelea chama fulani, huyo nafasi hiyo haimstahiki kama ambavyo Werema anatumia nafasi ya umma kwa misingi ya chama kwanza kuliko wajibu wake kwa umma, atakuwa amepotea na hatufai.
 
huo ndio ukweli mkuu, majaji hawatakiwi kuwa na chama ila kuna stor kuwa kuna jaji alipata nafasi za kisiasa na kugundulika kuwa alikuwa mwanachama wa ccm wa siku nyingi sitamtaja jina lakini yupo
 
huo ndio ukweli mkuu, majaji hawatakiwi kuwa na chama ila kuna stori kuwa kuna jaji alipata nafasi za kisiasa na kugundulika kuwa alikuwa mwanachama wa ccm wa siku nyingi sitamtaja jina lakini yupo
Mwengine atakuwa huyu werema ambaye kwenye CV yake imeoneshwa wazi kuwa ni mwanachama wa CCM. Mkuu, kwa Tanzania tegemea lolote lile, UDHAIFU kila pembe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom