Mwanasheria Mkuu: Jopo la Wanasheria lapambana kuokoa ndege ya Tanzania na mchakato wa Kimahakama upo katika hatua nzuri

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
SERIKALI imesema mchakato wa kimahakama wa kuachiwa kwa ndege mpya ya Tanzania, aina ya Bombardier Q400 iliyokamatwa nchini Canada hivi karibuni, uko katika hatua nzuri.

Mkulima, Hermanus Steyn aliikamata ndege hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita nchini Canada. Mzungu huyo aliwahi kuikamata ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 nchini Afrika Kusini mwezi Agosti mwaka huu.

Tanzania ilishinda kesi hiyo dhidi ya Steyn, baada ya serikali kutuma jopo la wanasheria wake Afrika Kusini. Lakini mkulima huyo ameibukia tena Canada na kuizuia ndege ya Bombardier Q400, ambayo ilikuwa tayari kuja nchini.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi alilieleza gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Uingereza, kuwa jopo la wataalamu wa Tanzania linaloongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Clement Mashamba liko nchini Canada, kuhakikisha ndege hiyo inaachiwa.

Alisema Wakili Mkuu wa Serikali na jopo lake, wanafanya kazi kubwa na hatua iliyofikiwa ili ndege hiyo iachiwe ni nzuri. Profesa Kilangi alisema kwa kuwa Steyn alipata amri ya kimahakama ya kuikamata ndege hiyo, Serikali ya Tanzania nayo imelazimika kufuata mchakato wa kimahakama ili amri hiyo itenguliwe na ndege iachiwe.

Kwa kuwa tukio la ndege za Tanzania kukamatwa nchini Canada, limejirudia mara ya pili baada ya tukio kama hilo kutokea mwaka 2017, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, alimweleza Rais John Magufuli mjini Dodoma kuwa aliamua kumuita Balozi wa Canada nchini ili kueleza kwa nini kila ndege za Tanzania zinapotaka kutoka nchini mwake, zinakamatwa.

Profesa Kabudi alisema alifanya mazungumzo marefu na Balozi huyo wa Canada jijini Dodoma na kumweleza kinagaubaga, bila kupepesa macho na bila tashwishwi kuwa Tanzania haifurahishwi na tabia na vitendo hivyo vya kila ndege ya Tanzania inapotakiwa kuondoka Canada kurudi hapa nchini, inakamatwa.

“Nimemwambia siyo tu kwamba tunasikitika, lakini pia tumekasirika, kwa maana hiyo tunafikiri Mheshimiwa Rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivi, siyo wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kwenda kununua ndege Canada, zipo nchi nyingine zinatengeneza ndege,” alisema.

Source: Habari Leo

My take;
Yule mzushi aliyeleta mada kuwa mkulima kashinda, sasa ameumbuka!
 
Kule Canada ni hatari tupu sio Africa kule hilo deni kama kweli mnadaiwa mtalilipa tu, wazungu wanajali sana haki kuliko tamaa ya pesa, na tena aliyepeleka kesi ni beberu mwenzao kama mzee meko asemavyo, mtafurahi ma show


Deni mtalilipa na kibao mtageuza kuwa kesi mmeshida
 
Kule hakuna mahakama ya kisutu wala amri kutoka juu. Wenzetu wanaangalia Sheria inasemaje!
Hata kama wataenda darasa zima la wanasheria kama kulipa tutalipa Tu hiyo mikwala yenu ya kishamba haitasaidia kitu
 
Dawa ya deni ni kulipa tu,sio kupambana.

Hizi habari za sijui kimwita balozi na kumwambia mmekasikirika hazina maana yoyoye ile.

Kasirika halafu lipa deni la watu,huyo sio mkulima wa korosho.
 
Kule Canada ni hatari tupu sio Africa kule hilo deni kama kweli mnadaiwa mtalilipa tu, wazungu wanajali sana haki kuliko tamaa ya pesa, na tena aliyepeleka kesi ni beberu mwenzao kama mzee meko asemavyo, mtafurahi ma show


Deni mtalilipa na kibao mtageuza kuwa kesi mmeshida
Tulia ww
utafikiri hilo deni unagawana na mzungu !!?
jinsi ulivyoshupalia na kutoa macho!!?
 
Mkulima ameni inspire na mimi nafikiria kuanza kulima matikiti :)
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Kumbe ilikuwa kweli!!!

Waseme tu wamelipa.. Haitowapunguzia kitu mafisiem majambazi..

Huku tunakula nyasi tu.
 
Wakulima wa Afrika Kusini wana akili sana, huku kwetu mkulima anadai muda wa Rais kutawala uongezwe
 
Back
Top Bottom