Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Kati ya vitu ambavyo vimenisumbua binafsi na kunifanya kurudia tena wito wa kuifanyia marekebisho sheria ya Majukumu na Kazi za Mwanasheria Mkuu (Office of the Attorney General - Discharge of Duties - 2005) ni pale niliposikia kuwa Rais anamuagiza Mwanasheria Mkuu kufanya kazi yake ambayo aliapa kuifanya lilipokuja suala la uchunguzi wa EPA.
Binafsi nilikataa kabisa akilini kuwa Mwanasheria Mkuu anahitaji kuambiwa na Rais nini cha kufanya kana kwamba hajui mamlaka yake au hana uwezo wa kupima kitu yeye mwenyewe. Kitendo cha Rais Kikwete kukaa chini na kumuagiza Mwanasheria Mkuu kufanya uchunguzi wa EPA na kuchukua hatua za kisheria kwangu kiliashiria mambo/matatizo makubwa mawili yaliyopo katika kutekeleza utawala wa sheria nchini.
a. Mwanasheria Mkuu hana uwezo wa kuhakikisha sheria zinafuatwa
b. Mwanasheria Mkuu anamtegemea Rais katika kujua nini cha kufanya kesho yake. Kama Rais hatomwambia nini cha kufanya sijui kama anaweza kufikiria yeye mwenyewe pasipo kuuliza tena Ikulu ili kupata baraka.
Hivyo nikalazimika kukaa chini na kuipitia sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (ambayo nimeiambatanisha hapa). Ndani yake nikaona mambo yafuatayo ambayo naamini ndiyo kiini za uzugaji wa kisheria unaoendelea nchini.
Kwenye Madaraka ya Mwanasheria Mkuu na Kazi za Mwanasheria Mkuu (Ibara ya 6 na ya 8) inaonesha ni nini kiini cha matatizo yetu. Mwanasheria hana madaraka na majukumu ya KUSIMAMIA UTEKELEZWAJI WA SHERIA ZOTE nchini yaani yeye siyo Chief Law Enforcer.
Kwanini hili ni muhimu? Umuhimu wake unakuja na unaonekana pale ambapo kuna watu wanaofanya kana kwamba hakuna sheria nchini au sheria zilizopo ni kama maoni tu au mapendekezo ya aina fulani. Ukiangalia kwa ukaribu sakata la Benki Kuu ni udhihirisho wa mawazo ya namna hii. Mambo yaliyotokea Benki Kuu ni kana kwamba hakuna sheria nchini na hakuna aliyekuwa na majukumu ya kuangalia waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wanafuata sheria.
Ni kwa sababu hiyo basi natoa pendekezo kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na majukumu yake mengi, ipewe jukumu la kwanza nalo ni kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa na kila mtu na hasa na kwanza kabisa wale waliopewa dhamana ya kuongoza, kusimamia, au kutekeleza majukumu fulani kwa ajili ya wananchi.
Maana yake ni nini? Manake ni kwamba Gavana wa Benki Kuu atatakiwa kufuata sheria ya fedha na ya Benki na zinazohusiana hadi nukta ya mwisho. IGP hawezi kukurupuka na kwenda kukamata watu na kuwaweka kizuizini kwa muda nje ya sheria vinginevyo Mwanasheria Mkuu anamfungulia mashtaka ya uvunjaji wa sheria.
Inapotokea kiongozi wa kisiasa au mtendaji au mtunga sheria anadaiwa kuvunja sheria Mwanasheria Mkuu anatakiwa kuanzisha uchunguzi mara moja utakaofanywa kwa mtindo wa Grand Jury au kitu kama hicho.
Jambo jingine ambalo linatakiwa kufanyika ni kuweka trigger clauses katika sheria ya Mwanasheria Mkuu ili asisubiri tena kuambiwa au kuitwa na kuelekezwa cha kufanya.
Kwa mfano hivi sasa uchunguzi wa EPA peke yake umechukua miezi sita. Bado hatujaingia kwenye suala la Meremeta, Mwananchi, Deep Green, Tangold, n.k n.k Na huko ni Benki Kuu tu na tena mwaka mmoja tu. Kama Mwanasheria Mkuu atakuwa anasubiri aambiwe na Ikulu nini cha kufanyia uchunguzi kuna dalili kuwa hadi 2010 tutakuwa tumegusa labda mambo manne tu ( kama kila moja litafanywa peke yake litachukua miezi sita kama ya EPA)
Katika kuleta mabadiliko hayo, naamini ofisi zifuatazo ziwekwe chini ya Idara ya Mwanasheria Mkuu.
- Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (anapogundua uvunjaji wa sheria kunakuwa na smooth transition to prosecution badala ya kutoa ripoti ya kila mwaka)
- Ofisi ya Mwenesha Mashtaka Mkuu wa serikali
Na pia kuanzisha kitu ambacho hakipo sasa hivi; Ikulu iwe na Mwanasheria Mkuu wa Ikulu/Rais ambaye atakuwa mshauri mkuu wa kisheria wa Rais au Ikulu. Mwanasheria Mkuu wa Tanzania atakuwa ni mshauri pale tu anapoombwa lakini jukumu lake la kwanza na kubwa zaidi ni kusimamia utekelezaji wa sheria zote nchini. Hivyo wizara na idara mbalimbali za serikali zitakuwa na wanasheria wake ambao si lazima wawe watumishi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu (nadhani iko hivyo sasa hivi).
Haya ngoja niweke nukta maana naona sitakoma.....