Mwanasheria Mkuu ampigia pasi Ole Sendeka kuiua hoja ya Mnyika dakika za mwisho. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanasheria Mkuu ampigia pasi Ole Sendeka kuiua hoja ya Mnyika dakika za mwisho.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Feb 3, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Muswada wa sheria kuhusu fedha haramu uliendelea huku wabunge wakichangia hoja kwa kusuasua. Mwisho wa michango ndipo bunge lilipokaa kama kamati kupitia vifungu kwa ajili ya marekebisho na kuvipitisha. Hapo ndipo mh Mnyika alipotaka marekebisho katika kanuni ya adhabu ambapo mwanasheria mkuu pamoja na kutounga mkono hoja ya Mnyika lakini tayari bila kushituka ilikuwa imeshaingia kwenye hansad za bunge na kukubaliwa.

  Ishu ilishitukiwa na Ole Sendeka na kupeleka ujumbe kwa AG ambaye naye alisimama kumkumbusha mwenyekiti kuwa Ole Sendeka alikuwa na taarifa ya kutoa. Wakati huo kulikuwa na muhudumu wa bunge aliyepeleka ujumbe kwa mwenyekiti kitu ambacho tafsiri yake ilikuwa ni kumwambia mwenyekiti akubali kusikiliza taarifa ya Ole Sendeka ambayo mwanzo aliikataa kwa madai kuwa hoja ilisha pita na kuungwa mkono kwa hiyo hakuna taarifa wala mwongozo tena. Baada ya Ole Sendeka kupewa nafasi hiyo ki mazabemazabe ndipo alipomkumbusha mwenyekiti kuwa hoja ya Mnyika iliyokataliwa na AG imeingia kwenye hansad tayari. Ndipo Mwenyekiti alipoamua kuwa hiyo sasa inafutwa kwenye hansad mara moja kisha na joho lake haraka haraka akaahirisha bunge na kutoka kwenye kiti japo CDM waliomba mwongozo. Hilo ndilo bunge letu lilivyo. Upande wa serikali hauko makini kabisa.

  Kwa hili naona sasa watakuwa wanapanga kukutana Chako ni Chako kwa ajili ya kupongezana kwa vyuku na biere. Ngoja nami niende huko nikasake udaku.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kwani hansad si ni records tu kwanin waende kufuta logic ni nini ya kufuta? Sisi wananch tumeshaona wameirusha sasa huko kwenye hansad records nani anapelekewa?
   
 3. j

  jigoku JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Bunge kandamizi linaloongozwa na mafisadi wa CCM
   
 4. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sasa hawa jamaa si ndo wanaotunga sheria, na hansad si ndo kumbukumbu zinazotumika. Wakisha futa sisi wananchi hata kama tumeziweka kwenye bongo zetu haisaidii kitu.
   
 5. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hoja si kuingia kwenye Hansard,hoja ni kwamba kifungu kilipita pamoja na marekebisho ya Mnyika ambayo kimsingi AG alikuwa ameyakataa.Kimsingi wabunge wameonyesha udhaifu mkubwa kwa maana;
  1.Kwa nini waliitikia NDIYOO tena kwa ushabika bila kuzingatia kwamba Mwenyekiti Mabumba alitamka"pamoja na marekebisho yake"?
  2.Mabumba ameonyesha udhaifu pia.Kwa nini ana "lack concetration"katika wakati muhimu kama ule?Jamaa kiukweli anapwaya kwenye kile kiti.Na hapo ndipo tunaweza kuona umuhimu wa watu kama akina Sitta.Hii si mala ya kwanza kwa Mabumba kujichanganya,,,,,,,,,,,Hawa ndio wanaosababisha bunge lifananishwe na original komedi!,,,Ni sawa na kusema Mnyika kama mchezaji alifunga goli la mkono,Mabumba kama refa hakuliona na akalikubali,alipomalia dakika 90 za mpira ndipo Ole Sendeka kama mchezaji wa timu pinzani akamstua refa na refa akafuta goli wakati mpira ulishamalizika.Kimsingi ilitakiwa libakie kuwa GOLI halali!Ni mfano tu huo.
   
 6. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Hansard haina tofauti na 'minutes' za kikao chochote, its a written account juu ya kila kitu kinachojiri kwenye kikao. Kwa hili, bunge limekosea sana.

  Neno 'hansard' ni jina la mtu i.e Thomas Hansard ambaye alikuwa mtu wa mwanzoni mwanzoni na maarufu sana wa kuandika minutes za vikao vya bunge nchini UK miaka ya zamani. Nia ya kuja na hansard bungeni ilikuwa ni kuondokana na tabia ya serikali ya wakati ule ya kufanya baadhi ya mijadala kuwa siri kwa umma. Chini ya muundo huu wa sasa, hansard haipaswi kuamua what is 'right' and what is 'wrong', kwani ile ni rekodi tu ya matukio ndani ya Mijadala.
   
 7. t

  taranda Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapumba ovyo sana jamaa lile hamna kitu kabisa. Kajikaanga na mafuta yake
   
Loading...