Mwanasheria mkuu ama waziri, uwajibika kwa makosa yao, pasipo kusingizia ni agizo kutoka

Ngamanya Kitangalala

Verified Member
Sep 24, 2012
422
1,000
Hapo Chenge anazuga tu ana la kujitetea kwa kusingizia aliagizwa na bosi wake

Yeye kama mwanasheria mkuu wa serikali, ndio mshauri mkuu wa s erikali katika mambo yote yanayohusiana na sheria ikiwa na pamoja katika kuandaa miswada ya sheria na kuipeleka bungeni kwa ajili ya kuboreshwa zaidi, kabla ya kutiwa saini na mh Rais na kuwa sheria

Kwa uelewa wangu mdogo, ninavyoelewa
Ni kuwa mikataba yote mikubwa pamoja na miswada mbalimbali ya shera ufuata utaratibu ufuatao

Kwanza kabisa waraka au mkataba uanza katika level ya ngazi ya wizara, ambapo wataalamu wa wizara husika hukaa na kuujadili na kutoa mapendezo yao ya kitaalamu

Baada ya hapo, waraka huo upelekwa katika ngazo ya kikao cha makatibu wakuu(MTC) ambako katibu mkuu kiongozi ndiye mwenyekiti wa kikao hicho

Katika kukao hicho, makatibu wakuu ujadili waraka huo kwa kina kwa kuangalia maslahi mapana ya nchi na pia upata mawazo na mapendekezo ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wanaousiana na sekta husika

Baada ya hapo waraka huo au mkataba husika upelekwa katika kikao cha baraza la mawaziri na waziri husika
Katika kikao hicho wajumbe ni kama ifuatavyo
Mh Rais wa JMT( mwenyekiti wa kikao)

Makamu wa Rais wa JMT

Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar

Waziri mkuu wa JMT

Mawaziri wote wa JMT

katibu mkuu kiongozi (katibu wa kikao)

Mwanasheria mkuu wa serikali

Katika kikao hicho, waraka au mkataba husika, ujadiliwa kwa kina na kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali

Na katika kikao hicho waziri husika ndiye anayepaswa kumshauri mh Rais kwa kuweka mbele maslahi mapana ya nchi
Mh Rais ndiye mwenye kauli ya mwisho ya kukubali ama kukataa mapendekezo yaliyomo katika wakala huo au mkataba husika,

Sasa kama mh waziri husika na mwanasheria mkuu wa serikali, walifanya kazi yao kwa uhakika ni wazi mkataba au muswada husika utakuwa uko kwa kujali maslahi ya nchi

Labda itokee mh Rais alimuamrisha waziri na mwanasheria mkuu wa serikali waandae mkataba na waraka kutokana na mapendekezo yake pasipo kujali ushauri wa wataalamu

Na kama hivyo itatokea itabidi waziri na mwanasheria mkuu, wakatae kusaini mkataba au waraka huo
Hivyo itabidi wajiuzuru kutoka katika nyadhifa zao, hiyo ndio uwajibikaji

Lakini wakisaini, ni wazi waziri husika atabeba msalaba wake, pindi ikija kubainila mkataba huo una mapungufu fulani

Kwa ufafanuzi huu, mh Chenge na mawaziri husika
Wanawajibika kwa makosa yao walio fanya pasipo kusingizia waliagizwa na bosi wao kufanya hivyo
Kwani walikuwa na uwezo wa kukataa kwa kulinda maslahi mapana ya nchi yetu
Na kujiuzuru nyadhifa zao

Miaka ya nyuma gavana wa benki kuu Edwin Mtei, aliwahi kujiuzuru ugavana, baada ya kutofautiana na bosi wake Rais Nyerere wakati huo
Baada ya kuona ushauri wake umekataliwa na mwl Nyerere
Hiyo ndio inapaswa kufanywa na viongozi wetu
Tunao wakabidhi dhamana ya uongozi

Ngamanya kitangalala, 2017
 

Siyabonga101

JF-Expert Member
Mar 8, 2016
2,430
2,000
Tatizo kubwa la Viongozi wetu hapa nchini ni Suala la UWAJIBIKAJI.
Katika Elimu ya Utawala Bora somo la Uwajibikaji ilitakiwa liwe la Lazima.
Haingii akili kwa Kiongozi wa Serikali,Jamii au Mamlaka yoyote kutamka hadharani ya kuwa Alisaini au kufanya jambo fulani kwa maelezo kutoka kwa Boss wake.
Unaposaini mkataba au kitu chochote ina maana wewe Kama Kiongozi umepitia na kuafiki yaliyomo katika mkataba au Jambo husika. Vivyo hivyo ikitokea mambo yakaenda kombo huko mbeleni ina maana Uwe tayari KUWAJIBIKA bila shurti.
Tubadilike Tanzania mpya Imewadia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom